سَابِقُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا كَعَرۡضِ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أُعِدَّتۡ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ
Kimbilieni kuomba msamaha kwa Mola wenu na Pepo (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale walio muamini Allah na Mtume Wake. Hiyo ni fadhila ya Allah, Humpa Amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa
مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مِّن قَبۡلِ أَن نَّبۡرَأَهَآۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ
Hautokei msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatuja utokezesha (hatujauumba). Hakika hayo kwa Allah ni mepesi
لِّكَيۡلَا تَأۡسَوۡاْ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمۡ وَلَا تَفۡرَحُواْ بِمَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٖ فَخُورٍ
Ili msihuzunike juu ya yale yaliyo kuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allah); na Allah Hapendi kila mwenye kujivuna, anaye jifakharisha
ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ
Ambao wanaofanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekengeuka, basi hakika Allah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote
لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَنزَلۡنَا مَعَهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمِيزَانَ لِيَقُومَ ٱلنَّاسُ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَنزَلۡنَا ٱلۡحَدِيدَ فِيهِ بَأۡسٞ شَدِيدٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُۥ وَرُسُلَهُۥ بِٱلۡغَيۡبِۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ
Kwa yakini Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa hoja zilizo wazi wazi, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Mizani (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Allah Ajue nani atakayeinusuru (Dini Yake) na Mtume Wake hali ya kuwa ni ghaibu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye kushinda
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحٗا وَإِبۡرَٰهِيمَ وَجَعَلۡنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا ٱلنُّبُوَّةَ وَٱلۡكِتَٰبَۖ فَمِنۡهُم مُّهۡتَدٖۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ
Na hakika tulimpeleka Nuhu na Ibrahim na tukajaalia kwenye kizazi chao Mitume na Vitabu. Basi miongoni mwao kuna waliyoongoka na wengi kati yao mafasiki
ثُمَّ قَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيۡنَا بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡإِنجِيلَۖ وَجَعَلۡنَا فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأۡفَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَرَهۡبَانِيَّةً ٱبۡتَدَعُوهَا مَا كَتَبۡنَٰهَا عَلَيۡهِمۡ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ رِضۡوَٰنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوۡهَا حَقَّ رِعَايَتِهَاۖ فَـَٔاتَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۡهُمۡ أَجۡرَهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ
Kisha Tukafuatisha baada yao, Mitume Wetu, na Tukamfuatisha ‘Issa mwana wa Maryam, na Tukampa Injili. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rahmah. Na uruhubani (maisha ya utawa wa Mapadri); wameyaanzisha wao wenyewe Hatukuwawajibishia hayo juu yao, isipokuwa ni kutafuta radhi za Allah. Lakini hawakuufuata ipasavyo kuufuata. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao malipo yao, na wengi wao ni mafasiki
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَءَامِنُواْ بِرَسُولِهِۦ يُؤۡتِكُمۡ كِفۡلَيۡنِ مِن رَّحۡمَتِهِۦ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ نُورٗا تَمۡشُونَ بِهِۦ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Enyi walioamini! Mcheni Allah, na muaminini Mtume Wake. (Allah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakusameheni; na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu
لِّئَلَّا يَعۡلَمَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ أَلَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱلۡفَضۡلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ
Ili wajue waliopewa Kitabu kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allah, Humpa Amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa