وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Teilnahme :
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchem
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Na matunda katika yale wanayoyatamani
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
(Wataabiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwasababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika sisi ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Na walipokuwa wakiambiwa Rukuuni (mswali), hawakuwa wakirukuu
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya hii (Qurani) watayaamini?