Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 141

۞وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّـٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Na yeye (Allah) ndiye ambaye ameanzisha (ameumba) mabustani yenye vichanja (vibanda vya kupumzikia) na yasiyokuwa na vichanja na mitende na mimea yenye ladha tofauti na mizaituni na makomamanga yanayofanana na yasiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapotoa matunda na toeni haki yake (Zaka yake) siku ya kuyavuna, na msifanye ubadhirifu. Hakika, yeye (Allah) hawapendi wafanyao ubadhirifu



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 142

وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Na miongoni mwa Wanyama (Allah ameumba) wabebao mizigo na wasiobeba mizigo. Kuleni katika vile Allah alivyokuruzukuni na msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika kabisa, yeye (shetani) kwenu ni adui wa dhahiri



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 143

ثَمَٰنِيَةَ أَزۡوَٰجٖۖ مِّنَ ٱلضَّأۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡمَعۡزِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ نَبِّـُٔونِي بِعِلۡمٍ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

(Ameumba) pea nane; wawili katika kondoo (dume na jike) na wawili katika mbuzi. Sema: Je, ni madume wawili (Allah) aliyoharamisha au majike wawili au vilivyobebwa ndani ya matumbo ya majike mawili? Niambieni kwa (hoja ya) kielimu kama nyinyi ni wakweli



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 144

وَمِنَ ٱلۡإِبِلِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ وَصَّىٰكُمُ ٱللَّهُ بِهَٰذَاۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا لِّيُضِلَّ ٱلنَّاسَ بِغَيۡرِ عِلۡمٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na katika ngamia (kaumba) wawili (dume na jike) na katika ng’ombe wawili. Sema: Je, ni madume mawili (Allah) alioharamisha au majike mawili au kilichobebwa katika matumbo ya majike mawili? Au nyinyi mlikuwepo wakati Allah amekuusieni haya? Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzushia Allah uongo ili awapoteze watu bila ya elimu yoyote. Hakika, Allah hawaongoi watu madhalimu



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 145

قُل لَّآ أَجِدُ فِي مَآ أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٖ يَطۡعَمُهُۥٓ إِلَّآ أَن يَكُونَ مَيۡتَةً أَوۡ دَمٗا مَّسۡفُوحًا أَوۡ لَحۡمَ خِنزِيرٖ فَإِنَّهُۥ رِجۡسٌ أَوۡ فِسۡقًا أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Sema: Katika yale niliyofunuliwa (niliyopewa Wahyi) sipati kilichoharamishwa kwa mlaji anayekila isipokuwa tu kama kitakuwa nyamafu au damu yenye kuchirizika au nyama ya nguruwe, kwa sababu hivyo ni najisi, au kilichochinjwa kwa minajili ya kutajwa asiyekuwa Allah katika kuchinjwa kwake.[1] Basi aliyeshikika pasipo kupenda wala kuchupa mipaka (anaruhusiwa kula hivyo vilivyoharamishwa kwakuwa) Mola wako Mlezi ni Msamehevu sana, Mwenye kurehemu


1- - Hapa Qur’ani imemtaka Mtume ataje baadhi ya vitu vilivyoharamishwa. Hivi ni baadhi tu. Vingine amevitaja Mtume kupitia Hadithi zake. Watu wa Suna na Jamaa (Suna) wanavikubali vilivyotajwa na Mtume kupitia maagizo ya Allah kwamba, anayotuagiza Mtume tuyafuate na anayotukataza tuyaache. Rejea Aya ya 7 ya Sura Alhashri (59).


Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 146

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٖۖ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ وَٱلۡغَنَمِ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتۡ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلۡحَوَايَآ أَوۡ مَا ٱخۡتَلَطَ بِعَظۡمٖۚ ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِبَغۡيِهِمۡۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na kwa Wayahudi, tumeharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na kondoo na mbuzi tumewaharamishia mafuta yao isipokuwa tu kile kilichobeba migongo yao au matumbo au kilichogandana na mifupa. Hayo tumewalipa kwa sababu ya uasi wao. Na kwa yakini kabisa, sisi tu ndio wakweli



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 147

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمۡ ذُو رَحۡمَةٖ وَٰسِعَةٖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُهُۥ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Basi wakikupinga waambie: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema yenye kuenea, na adhabu yake kwa watu waovu haizuiliki



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 148

سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشۡرَكۡنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ حَتَّىٰ ذَاقُواْ بَأۡسَنَاۗ قُلۡ هَلۡ عِندَكُم مِّنۡ عِلۡمٖ فَتُخۡرِجُوهُ لَنَآۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا تَخۡرُصُونَ

Watasema waliomshirikisha Allah kwamba: Lau kama angetaka Allah tusingefanya ushirikina sisi wala baba zetu, na tusingeharamisha kitu chochote. Kama hivyo walipinga waliokuwepo kabla yao mpaka wakaonja adhabu yetu. Sema (uwaulize): Je, mnayo elimu (ushahidi na hoja) yoyote ya hilo mtutolee (mtuoneshe)? Hamna chochote mkifuatacho isipokuwa dhana tu, na hamkuwa nyinyi ila mnaropoka tu



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 149

قُلۡ فَلِلَّهِ ٱلۡحُجَّةُ ٱلۡبَٰلِغَةُۖ فَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Sema: Basi Allah ana hoja madhubuti. Basi lau kama angetaka, kwa hakika kabisa angekuongoeni nyote



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 150

قُلۡ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشۡهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَٰذَاۖ فَإِن شَهِدُواْ فَلَا تَشۡهَدۡ مَعَهُمۡۚ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ

Sema: waleteni mashahidi wenu ambao watashuhudia kuwa Allah ameharamisha kula (Wanyama) hawa. Basi kama watashuhudia wewe usishuhudie pamoja nao. Na usifuate utashi wa nafsi za wale ambao wamezipinga Aya zetu, na wale wasioamini Akhera na ilhali wanamlinganisha Mola wao (kwamba yuko sawa na vitu vingine, kama vile masanamu, mizimu n.k.)



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 151

۞قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Sema: Njooni nisome yale Mola wenu aliyokuharamishieni (nayo ni) msikishirikishenaye kitu chochote na wazazi wawili wafanyieni yaliyo mazuri na msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara (umasikini kwa sababu) sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Na msiyakaribie mambo machafu yaliyo dhihiri kati ya hayo na yaliyo ya siri. Na msiiue nafsi ambayo Allah ameharamisha (kuiua) ila kwa haki tu. Hayo amekuusieni (Allah) ili myatie akilini



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 152

وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۖ وَإِذَا قُلۡتُمۡ فَٱعۡدِلُواْ وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰۖ وَبِعَهۡدِ ٱللَّهِ أَوۡفُواْۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Na msizisogelee mali za Yatima ila kwa njia iliyo nzuri sana hadi afikie utu uzima wake. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Hatuilazimishi nafsi (jambo lolote) isipokuwa kwa kadiri ya vile iwezavyo. Na msemapo semeni kwa uadilifu hata ikiwa (ni dhidi ya) ndugu. Na ahadi za Allah zitekelezeni. Hayo amekuusieni (Allah) ili mpate kukumbuka



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 153

وَأَنَّ هَٰذَا صِرَٰطِي مُسۡتَقِيمٗا فَٱتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمۡ عَن سَبِيلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na kwa hakika, hii ni njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na msifuate njia nyingine zikaku-farakanisheni muiache njia yake. Hayo amekuusieni (Allah) ili muwe wachaMungu



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 154

ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ

Kisha tulimpa Musa kitabu ikiwa ni kutimiza neema kwa aliyefanya mazuri na ni ufafanuzi zaidi wa kila kitu na ni muongozo na rehema ili wapate kuamini kukutana na Mola wao



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 155

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, chenye baraka. Basi kifuateni na mcheni Allah ili mpate kushushiwa rehema



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 156

أَن تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلۡكِتَٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيۡنِ مِن قَبۡلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمۡ لَغَٰفِلِينَ

(Allah amekuteremshieni Qur’ani) Ili msije kusema: Ilivyo ni kwamba, vitabu vimeteremshwa kwa makundi mawili ya (waliokuwepo) kabla yetu, na kwamba hakika tulikuwa hatuyajui kamwe waliyokuwa wakiyasoma



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 157

أَوۡ تَقُولُواْ لَوۡ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡكِتَٰبُ لَكُنَّآ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمۡۚ فَقَدۡ جَآءَكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنۡهَاۗ سَنَجۡزِي ٱلَّذِينَ يَصۡدِفُونَ عَنۡ ءَايَٰتِنَا سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يَصۡدِفُونَ

Au (msije) mkasema: Lau kama tungeteremshiwa sisi kitabu tungekuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi kwa hakika kabisa, umekujieni ubainifu kutoka kwa Mola wenu Mlezi na muongozo na rehema. Sasa ni nani dhalimu zaidi (katika suala zima la itikadi) kuliko yule aliyepinga Aya za Allah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aya zetu adhabu mbaya kwa sababu ya yale waliyokuwa wakijitenga nayo



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 158

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ

Hakuna wanacho kingoja isipokuwa tu wanangoja wawajie Malaika au aje Mola wako Mlezi au zije baadhi ya ishara za Mola wako. Siku zitakapokuja baadhi ya ishara za Mola wako haitamfaa mtu imani yake ikiwa hakuamini kabla ya hapo au hakuchuma kheri yoyote katika kuamini kwake. Sema: Ngojeni, nasi (pia) ni wenye kungoja



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 159

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمۡ وَكَانُواْ شِيَعٗا لَّسۡتَ مِنۡهُمۡ فِي شَيۡءٍۚ إِنَّمَآ أَمۡرُهُمۡ إِلَى ٱللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Hakika, wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi huna lawama yoyote kwao. Ilivyo ni kwamba, shauri lao liko kwa Allah kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 160

مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشۡرُ أَمۡثَالِهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَا وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Yeyote atendae (jambo) zuri atapata mfano wa zuri hilo mara kumi, na atendae baya hatalipwa isipokuwa mfano wake, na wao (waja) hawatadhulumiwa



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 161

قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ دِينٗا قِيَمٗا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Kwa hakika, mimi ameniongoza Mola wangu Mlezi kwenye njia iliyo nyooka; dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahimu aliyeacha itikadi zote potofu na hakuwa miongoni mwa washirikina



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 162

قُلۡ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحۡيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sema: Hakika, Swala yangu na ibada zangu (zote) na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allah, Mola wa viumbe wote



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 163

لَا شَرِيكَ لَهُۥۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرۡتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

(Allah ambaye) Hana mshirika. Na hayo ndio niliyoamrishwa na mimi ni Muislamu wa kwanza (katika umma huu)



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 164

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِي رَبّٗا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيۡءٖۚ وَلَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٍ إِلَّا عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ

Sema: Je nitafute Mola mlezi asiekuwa Allah! na ilhali yeye (Allah) ni Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haitachuma (jambo la kheri au la shari) isipokuwa litarudi kwake mwenyewe. Na hatabeba mtu yeyote mzigo wa (dhambi za) mwengine. Kisha (nyote) marejeo yenu ni kwa Mola wenu tu, na atakuelezeni yote mliyokuwa mkitofautiana



Sure: AL-AN’AAM 

Vers : 165

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَـٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Na yeye (Allah) ndiye aliyekufanyeni mnaopokezana duniani, na akawanyanyua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja ili akujaribuni katika yale aliyokupeni. Hakika, Mola wako Mlezi ni Mwepesi sana wa kuadhibu na, kwa hakika kabisa, yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Sure: AL-AARAAF 

Vers : 1

الٓمٓصٓ

Allah ndiye Mjuzi zaidi wa alichokikusudia katika herufi hizi



Sure: AL-AARAAF 

Vers : 2

كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

(Hii Qur’ani ni) Kitabu ulichoteremshiwa. Basi kusiwe na uzito wowote ndani ya kifua chako juu yake (usikose raha katika kukiamini na kukitangaza). (Umeteremshiwa kitabu hiki) Ili kwacho uwaonye (watu) na (ili kiwe) ukumbusho kwa waumini



Sure: AL-AARAAF 

Vers : 3

ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Fuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi na msifuate wapenzi wengine badala yake. Ni machache mno mnayowaidhika nayo



Sure: AL-AARAAF 

Vers : 4

وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ

Na ni miji mingi tumeiangamiza; iliwajia adhabu yetu wakiwa wamelala usiku au wakiwa wamejipumzisha mchana



Sure: AL-AARAAF 

Vers : 5

فَمَا كَانَ دَعۡوَىٰهُمۡ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَآ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Basi hayakuwa madai yao (majuto yao) pale adhabu yetu ilipowafika isipokuwa tu walisema: Hakika, sisi tulikuwa madhalimu