أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?
وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ
Na hakika alimuona (Jibriyl) kwa mara nyingine
عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ
Karibu yake kuna Jannatu Al-Ma-waa
إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ
Ulipoufunika mkunazi huo hicho kilicho ufinika
مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Jicho lake halikukengeuka wala halikupindukia mipaka
لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ
Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Bwana wake kubwa kabisa
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّـٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ
Je, mmeona (masanamu) Laata na ‘Uzzaa?
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ
Na Manaata mwengine wa tatu?
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ
Je, nyinyi mna wana wa kiume Naye Ana wana wa kike?
تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ
Huo basi ni mgao wa dhulma!
إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ
Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali imekwishawajia kutoka kwa Bwana wao mwongozo
أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
Kwani kila Mtu anapata kila anayoyatamani?
فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ
Na Allah ndiye mmiliki wa Akhera na Dunia
۞وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ
Na kuna malaika wengi mbinguni hainufaishi chochote uombezi wao ila baada ya kupewa idhini na Allah kwa amtakaye na amridhie
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ
Hakika wale wasioamini Aakhirah bila shaka wanawaita Malaika kwa majina ya kike
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا
Na wala hawana ujuzi wowote ule wa hayo; hawafuati isipokuwa dhana, na hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki
فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Basi achana naye ambaye ameupa mgongo ukumbusho Wetu na wala hataki isipokuwa maisha ya dunia
ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Huo ndio upeo wao wa elimu. Hakika Bwana wako ni Mjuzi zaidi wa ambaye amepotoka njia Yake, Naye Mjuzi zaidi wa ambaye ameongoka
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَـٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى
Na ni vya Allah Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, ili Awalipe wale waliofanya uovu kwa yale waliyoyatenda, na Awalipe wale waliofanya mema kwa mema zaidi
ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ
Wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogo-madogo. Hakika Bwana wako ni Mwingi wa msamaha. Yeye Anakujueni vyema, tangu Alipokuanzisheni kutoka katika ardhi, na pale mlipokuwa mimba changa matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa
أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ
Hivi umemuona yule ambaye amekengeuka
وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ
Na Akatoa kidogo, kisha akazuia.?
أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
hivi yeye ana elimu ya ghaibu basi kwa elimu hiyo yeye anaona?
أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ
Au hawajaambiwa kwa ambayo yamo kwenye kitabu cha Mussa?
وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ
Na Ibraahim aliyetimiza (ahadi)
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ
Na kwamba mbebaji dhambi hatobeba mzigo wa mwengine
وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Na kwamba Mtu hatopata malipo isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi
وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ
Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana
ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ
Kisha atalipwa malipo yake kamilifu