وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Na hakika kwa bwana wako ndio marejeo
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ
Na kwamba Yeye Ndiye Anayesababisha kwa Mtu kicheko (furaha) na kilio
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا
Na hakika yeye ndiye anafisha na ndiye anayehuisha
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ
Na hakika yeye ameumba aina mbili ya viumbe Dume Na Jike
مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ
Kutokana na tone la manii linapomiminwa
وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ
Na kwamba ni juu Yake uanzishaji mwengine (kufufua)
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ
Na kwamba Yeye Ndiye Atoshelezaye na Akinaishaye
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye Mola wa nyota ya Ash-Shi’-raa (inayoabudiwa).[1]
1- - Ash-Shi’-raa:- Hii ni Nyota maarufu, na Allah ameihusisha kuitaja hapa, ijapokuwa yeye ni Mola wa kila kitu kwasababu hii Nyota ni katika zilizokuwa zikiabudiwa katika zama za Kijaahiliyya, kwahiyo Allah akabainisha kila chochote wanacho kiabudu Washirikina basi hicho kimeumbwa na Allah, na hakistahiki kuabudiwa.
وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ
Na kwamba Yeye Ndiye Aliyeangamiza kina ‘Aad Mwanzo
وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ
Na Watu wa Thamuwd kisha Hakuwabakisha
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ
Na Watu wa Nuwh hapo kabla, hakika wao walikuwa madhalimu zaidi na wapindukaji mipaka zaidi wa kuasi
وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ
Na miji iliyopinduliwa ni yeye Allah aliyeipindulia mbali
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ
Na ikawafunika ambacho kimewafunika
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
Basi neema gani za Bwana wako unazitilia shaka?
هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ
Huyu (Mtume þ) ni muonyaji miongoni mwa waonyaji wa awali
أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ
Kimekaribia kinachokaribia
لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ
Hakuna asiyekuwa Allah mwenye uwezo wa kukibainisha
أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ
Je, mnastaajabu kwa Mazungumzo haya (ya Qur-aan)?
وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ
Na mnacheka na wala hamlii?
وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ
Na hali nyinyi mnaghafilika, mnadharau na kushughulika na anasa?
فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩
Basi msujudieni Allah na mwabuduni Yeye tu
ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ
Kimekaribia Kiyama na mwezi umepasuka
وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ
Na (Makafiri kila) wanapoona Aya yoyote (ishara/muujiza) wanakengeuka na kusema: (Huu) Ni uchawi endelevu
وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ
Na wamekadhibisha (haki) na wamefuata utashi wa nafsi zao. Na kila jambo (la kheri au la shari) litatulia (mahali pake. Watu wema watalipwa wema na watu wabaya watalipwa ubaya)
وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ
Na kwa yakini kabisa, katika habari muhimu, imekwishawajia habari ambayo ndani yake mna makemeo makali
حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ
Ni hekima ya kiwango cha juu kabisa, lakini maonyo (wanayopewa) hayasaidii kitu
فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَيۡءٖ نُّكُرٍ
Basi wapuuze (na waache waingoje) siku (ya Kiyama ambapo) mnadi (mtangazaji) atanadi (atatangaza ili watu waende) kwenye jambo la kutisha sana
خُشَّعًا أَبۡصَٰرُهُمۡ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ كَأَنَّهُمۡ جَرَادٞ مُّنتَشِرٞ
Macho yao yakiwa dhalili, watatoka katika makaburi kama kwamba wao ni nzige waliosambaa
مُّهۡطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِۖ يَقُولُ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَسِرٞ
Wenye kukimbia mbio huku wakibinua shingo zao wakielekea kwa muitaji; makafiri watasema: Hii ni siku ngumu!
۞كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ فَكَذَّبُواْ عَبۡدَنَا وَقَالُواْ مَجۡنُونٞ وَٱزۡدُجِرَ
Walikadhibisha kabla yao watu wa nuhu na wakamkadhibisha mja wetu wakasema mwendawazimu na akafanyiwa maudhi