فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّي مَغۡلُوبٞ فَٱنتَصِرۡ
Basi akamwita Mola wake mlezi kwamba: Hakika mimi nimeshindwa (nimezidiwa nguvu) basi ni Nusuru
فَفَتَحۡنَآ أَبۡوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٖ مُّنۡهَمِرٖ
Tukafungua milango ya mbingu kwa maji yanayofoka na kumiminika kwa nguvu
وَفَجَّرۡنَا ٱلۡأَرۡضَ عُيُونٗا فَٱلۡتَقَى ٱلۡمَآءُ عَلَىٰٓ أَمۡرٖ قَدۡ قُدِرَ
Na tukaipasua ardhi yote kwa chemchem, na yakakutana maji kwa pamoja kwa jambo lililokadiriwa
وَحَمَلۡنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلۡوَٰحٖ وَدُسُرٖ
Na Tukambeba kwenye ile (jahazi) yenye mbao na misumari
تَجۡرِي بِأَعۡيُنِنَا جَزَآءٗ لِّمَن كَانَ كُفِرَ
Kikienda haraka tukikitazama kwa macho yetu ikiwa ni malipo kwa ambaye alikuwa amekufuru
وَلَقَد تَّرَكۡنَٰهَآ ءَايَةٗ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na kwa yakini Tumeiacha iwe ni mazingatio, Je, basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu?
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na Hakika Tumeirahisisha Qur’an Kwa Ajili Ya Ukumbusho Je Kuna Mwenye kukumbuka?
كَذَّبَتۡ عَادٞ فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Kina ‘Aad walikadhibisha, basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu?
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا صَرۡصَرٗا فِي يَوۡمِ نَحۡسٖ مُّسۡتَمِرّٖ
Hakika Sisi Tumewapelekea upepo wa kimbunga wenye sauti kali na baridi kali katika siku korofi yenye kuendelea mfululizo
تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٖ مُّنقَعِرٖ
Unawang’oa watu kana kwamba vigogo vya mtende vilong’olewa
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu?
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na Hakika Tumeirahisisha Qur’an Kwa Ajili Ya Ukumbusho Je Kuna Mwenye kukumbuka?
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ
Kina Thamuwd waliwakadhibisha Waonyaji
فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٗا مِّنَّا وَٰحِدٗا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٍ
Wakasema: Ah! Tumfuate binaadamu miongoni mwetu? Hakika hapo sisi tutakuwa katika upotofu na wazimu
أَءُلۡقِيَ ٱلذِّكۡرُ عَلَيۡهِ مِنۢ بَيۡنِنَا بَلۡ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٞ
Ah! Ameteremshiwa ukumbusho (Wahyi) baina yetu? Bali yeye ni muongo mkubwa mwenye kiburi mno
سَيَعۡلَمُونَ غَدٗا مَّنِ ٱلۡكَذَّابُ ٱلۡأَشِرُ
Watakuja kujua kesho nani muongo mkubwa mwenye kiburi mno
إِنَّا مُرۡسِلُواْ ٱلنَّاقَةِ فِتۡنَةٗ لَّهُمۡ فَٱرۡتَقِبۡهُمۡ وَٱصۡطَبِرۡ
Hakika Sisi Tutawapelekea ngamia jike awe jaribio kwao, basi (Ee Nabiy Swaalih) watazame na vuta subira
وَنَبِّئۡهُمۡ أَنَّ ٱلۡمَآءَ قِسۡمَةُۢ بَيۡنَهُمۡۖ كُلُّ شِرۡبٖ مُّحۡتَضَرٞ
Na wajulishe kwamba maji ni mgawanyo baina yao (ngamia na wao), kila sehemu ya maji itahudhuriwa (kwa zamu)
فَنَادَوۡاْ صَاحِبَهُمۡ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ
Wakamuita Mtu Wao Akajipa Ushujaa Na Kumchinja
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi Vipi Ilikua Adhabu Yangu Na Maonyo yangu?
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ
Hakika Sisi Tulipeleka Kwao Ukelele Moja tu, wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na Hakika Tumeirahisisha Qur’an Kwa Ajili Ya Ukumbusho Je Kuna Mwenye kukumbuka
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ
Wamekadhibisha Watu wa Luutwi Mitume waonyaji
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ
Hakika Sisi Tumewapelekea Upepo Uliyo Na Mchanga Ispokua Watu Wa Luutwi Waliyomuamini Tuliwaokoa Wakati Wa Theluthi Ya Mwisho Ya Usiku
نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ
Neema kutoka Kwetu, hivyo ndivyo Tunavyomlipa ambaye ameshukuru
وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ
Na Hakika Aliwaonya Kuhusiana Na Adhabu Yetu Wakatia Shaka Na Maonyo Hayo
وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Na kwa yakini walimshawishi awape wageni wake, basi Tukawapofoa macho yao. Basi onjeni adhabu Yangu na maonyo Yangu
وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ
Hakika Iliwafika Wao Adhabu Yenye Kudumu Asubuhi Mapema
فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi Onjeni Adhabu Yangu na Maonyo