فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na endapo watakengeuka basi hakika huna jukumu isipokuwa kufikisha (ujumbe) waziwazi tu
يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Wanazijua neema za Allah kisha wanazipinga na wengi wao ni makafiri
وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ
Na (wakumbushe ewe Mtume) siku tutakapofufua shahidi (Mtume wao) kwa kila umma, kisha wale waliyokufuru hawataruhusiwa (kujisahihisha kutokana na waliyoyafanya) na hawata kubaliwa udhuru
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلۡعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawata punguziwa (adhabu) na hawatasubiriwa
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ شُرَكَآءَهُمۡ قَالُواْ رَبَّنَا هَـٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدۡعُواْ مِن دُونِكَۖ فَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلَ إِنَّكُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na pindi wale washirikina watakapo waona washirika wao (walio washirikisha na Allah), watasema: Mola wetu mlezi, hao ndio washirika wetu ambao tulikuwa tunawaabudu badala yako. Basi watawatupia neno (kwa kusema): hakika ninyi ni waongo kabisa
وَأَلۡقَوۡاْ إِلَى ٱللَّهِ يَوۡمَئِذٍ ٱلسَّلَمَۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Na siku hiyo (washirikishaji) watadhihirisha utii mbele ya Allah, na yatawapotea yote waliyokuwa wakiyatunga
ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدۡنَٰهُمۡ عَذَابٗا فَوۡقَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يُفۡسِدُونَ
(Ama) wale waliokufuru na wakawazuia (watu) njia ya Allah, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa yale waliokuwa wakiyaharibu
وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ
Na siku tutakayomfufua shahidi (Mtume) katika kila umma kutoka miongoni mwao atakayethibitisha (kuwa aliwafikishia ujumbe wa Allah wakampinga), na tutakuleta wewe kuwa shahidi wa (watu) hawa. Na tumekuteremshia kitabu kikibainisha kila kitu, na rehema na bishara kwa Waislamu
۞إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka
وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ
Na timizeni ahadi ya Allah mnapoahidi; na msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, na hakika mlishamfanya Allah kuwa mdhamini wenu. Hakika Allah anayajua mnayoyafanya
وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِي نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثٗا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
Na (msirudi katika viapo vyenu ikawa) kama yule mwanamke aliyekata uzi wake vipandevipande baada ya (kuusokota) kuwa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu ili lisije likawa kundi moja la watu kuwa na nguvu zaidi kuliko kundi lingine. Hakika Allah anawajaribuni kwa njia hiyo, na bila shaka atawabainishieni Siku ya Kiyama mliyokuwa mkikhitilafiana
وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na Allah angelitaka, kwa yakini angeliwafanyeni umma moja; lakini anayetaka (upotevu) anampoteza, na anayetaka (mwongozo) anamwongoza; na hakika mtaulizwa yale mliyokuwa mkiyafanya
وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ فَتَزِلَّ قَدَمُۢ بَعۡدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُواْ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَكُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Wala msivifanye viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu, usije mguu ukateleza baada ya kuuimarisha, na mkaonja ubaya kwasababu ya wale mliowazuia katika njia ya Allah, na nyinyi mna adhabu kubwa mno
وَلَا تَشۡتَرُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na msiuze ahadi ya Allah kwa thamani ndogo. Hakika si vingine (kilicho) kwa Allah ni bora kwenu ikiwa mnajua (hayo)
مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Allah ndivyo vibakiavyo; na kwa yakini sisi tutawapa waliosubiri ujira wao sawa na matendo mazuri waliyokuwa wakiyatenda
مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Atakayefanya mema, mwana-mume au mwanamke, ilhali ni muumini, basi kwa hakika tutampa maisha mema na kwa yakini tutawapa ujira wao kwa uzuri zaidi kuliko yale waliokuwa wakiyatenda
فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Na pindi unapotaka kusoma Qur’ani, basi jikinge kwa Allah (akulinde) na shetani aliyelaaniwa
إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Hakika yeye hana nguvu juu ya wale walioamini na kwa Mola wao mlezi tu wanategemea
إِنَّمَا سُلۡطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوۡنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشۡرِكُونَ
Hakika nguvu yake ni juu ya wale tu wanaomfanya kuwa rafiki na wale wanaomshirikisha (Allah)
وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na pindi tunapobadilisha Aya mahali pa Aya (nyingine), Allah ndiye mjuzi zaidi kwa anachoteremsha (na alichokiondoa), walisema: Hakika wewe ni mzushi tu. Bali wengi wao hawajui
قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ
Sema: Ameiteremsha Roho mtakatifu (Jibrili) kutoka kwa Mola wako mlezi kwa haki kabisa, ili kuwaimarisha wale walioamini, na kuwa mwongozo na habari njema kwa Waislamu
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّهُمۡ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُۥ بَشَرٞۗ لِّسَانُ ٱلَّذِي يُلۡحِدُونَ إِلَيۡهِ أَعۡجَمِيّٞ وَهَٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيّٞ مُّبِينٌ
Na bila shaka tunajua kwamba (washirikina) wanasema kuwa: Hakika (Muhammad) anafundishwa na mtu hii (Qura’ani. Huo ni uongo kwasababu) mtu wanayedai kumfundisha, lugha yake ni ya kigeni na hii ni lugha ya kiarabu kilicho wazi
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَا يَهۡدِيهِمُ ٱللَّهُ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Hakika wale wasioziamini Aya za Allah, Allah hatawaongoza, na wana adhabu iumizayo
إِنَّمَا يَفۡتَرِي ٱلۡكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ
Hakika sivingine wanaozua uongo ni wale tu wasioziamini Aya za Allah, na hao ndio waongo (hasa)
مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Hakika anayezusha uongo ni Yule aliyetamka neno la ukafiri baada ya imani isipokuwa tu yule aliyeshurutishwa, ilhali moyo wake unabaki imara katika imani. Lakini wale ambao mioyo yao imeridhika na ukafiri, basi ghadhabu za Allah zitawashukia, na watapata adhabu kubwa
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hayo ni kwa sababu wame-yapenda zaidi maisha ya dunia kuliko Akhera, na kwa hakika Allah hawaongozi watu makafiri
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ
Hao ndio Allah amepiga muhuri juu ya mioyo yao (haizingatii haki na kuifuata) na masikio yao (hawasiki neno la haki) na macho yao (hawaoni haki), na hao ndio walioghafilika
لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Hakuna shaka kwamba hao ndio wataokhasirika Akhera
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا فُتِنُواْ ثُمَّ جَٰهَدُواْ وَصَبَرُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Kisha hakika Mola wako mlezi, kwa wale waliohama baada ya kuteswa, kisha wakajitahidi na wakasubiri, bila shaka Mola wako mlezi baada ya hayo ni msamehevu sana, mwenye rehema
۞يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Siku ambayo kila nafsi itakuja kujitetea yenyewe, na kila nafsi itapewa sawa na iliyoyafanya, nao hawatadhulumiwa