لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ
Katika Siku iliyo kuu,
Teilnahme :
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Siku watu watakaposimama (simamishwa) kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote?
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ
Unajua nini Sijjin?
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Kitabu kilicho andikwa
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ
Wala haikadhibishi (siku hiyo) isipokuwa kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi
إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu katika nyoyo zao hayo waliyokuwa wakiyachuma
كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi
ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ
Kisha wataingia Motoni!
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I’liyyin
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Na nini kitakacho kujulisha nini I’liyyin?
Ni Kitabu kilicho andikwa
يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wanakishuhudia walio kurubishwa (na Allah)
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia
تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Utatambua katika nyuso zao mng’aro wa neema,
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kilichotiwa muhuri,
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ
Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini
وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ
Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ
Na wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi
وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio hasa walio potea
وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao
فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,