Sure: ANNAHLI 

Vers : 112

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا قَرۡيَةٗ كَانَتۡ ءَامِنَةٗ مُّطۡمَئِنَّةٗ يَأۡتِيهَا رِزۡقُهَا رَغَدٗا مِّن كُلِّ مَكَانٖ فَكَفَرَتۡ بِأَنۡعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلۡجُوعِ وَٱلۡخَوۡفِ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ

Na Allah amepiga mfano wa mji (wa Makkah) ambao ulikuwa na amani na utulivu, riziki iliwajia kwa wingi na wepesi kutoka kila mahali, lakini wakazikufuru neema za Allah (kwa kumshirikisha), Allah akawaonjesha vazi la njaa na hofu (kuogopa vikosi vya jeshi la Mtume Allah amshushie rehema na amani) kwasababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya (ya ukafiri)



Sure: ANNAHLI 

Vers : 113

وَلَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡهُمۡ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ

Na kwa hakika aliwajia Mtume anayetokana na wao, basi wakam-kadhibisha, na adhabu ikawashika ilhali wao ni wadhalimu



Sure: ANNAHLI 

Vers : 114

فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ

Na kuleni katika vile alivyo-waruzukuni Allah, vilivyo halali na vizuri na shukuruni neema za Allah ikiwa nyinyi mnamuabudu yeye tu



Sure: ANNAHLI 

Vers : 115

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika (Allah) amewa-haramishia (katika wanyama) mzoga na damu (iliyomwagika baada ya mnyama kuchinjwa) na nyama ya nguruwe na (mnyama) aliyechinjwa si kwa ajili ya Allah (kama kuchinja kwa ajili ya mashetani). Lakini atakayelazimika (kula nyama hiyo kwa njaa asife kwa kukosa mbadala), bila kuasi wala kuchupa mipaka, basi hakika Allah ni msamehevu, mwenye rehema



Sure: ANNAHLI 

Vers : 116

وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

Na msiseme (enyi washirikina), kwa uongo ambao usemwao na ndimi zenu kuwa, hii halali (kwanini Allah ameiharamisha) na hii haramu (kwanini ameihalalisha), ili kumzulia Allah uongo. Hakika wale wamzuliao Allah uongo hawatafaulu[1]


1- - Katika Aya hii Allah anabainisha kuwa uhalali wa kitu na uharamu hatokani na utashi wa mtu ama watu, bali ni msingi uliyowekwa na Allah mwenyewe kwa viumbe wake, hivyo anawakemea washirikishaji na Makafiri kwa ujumla, wasihalalishe au kuharamisha kitu kwa utashi wa nafsi zao. Kilicho halali ni kile alicha halalisha Allah, na haramu ni kile alicho kiharamisha Allah.


Sure: ANNAHLI 

Vers : 117

مَتَٰعٞ قَلِيلٞ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

(watapata) starehe ndogo (hapa duniani) na wana adhabu iumizayo (Akhera)



Sure: ANNAHLI 

Vers : 118

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Na kwa wale ambao ni Wayahudi, tuliwaharamishia yale tuliyokuhadithia hapo kabla. Na sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakizidhulumu nafsi zao



Sure: ANNAHLI 

Vers : 119

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ

Kisha hakika Mola wako mlezi kwa wale waliofanya ubaya (dhambi) kwa kutokujua, kisha wakatubu baada ya hayo na waka-tenda mema, hakika bila shaka Mola wako baada ya hayo ni mwingi wa kusamehe, mwenye rehema



Sure: ANNAHLI 

Vers : 120

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةٗ قَانِتٗا لِّلَّهِ حَنِيفٗا وَلَمۡ يَكُ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Hakika Ibrahimu alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Allah, muongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina



Sure: ANNAHLI 

Vers : 121

شَاكِرٗا لِّأَنۡعُمِهِۚ ٱجۡتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

(Ibrahimu alikuwa) daima mwenye kushukuru neema zake (Allah) akamchagua na akamuon-goza kwenye njia iliyonyooka



Sure: ANNAHLI 

Vers : 122

وَءَاتَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na tukampa wema duniani, na hakika yeye Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema



Sure: ANNAHLI 

Vers : 123

ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Kisha tukakufunulia (ewe Muhammad) kwamba ufuate mila (dini) ya Ibrahimu (aliyekuwa) mtiifu kamili, wala hakuwa miongoni mwa washirikina



Sure: ANNAHLI 

Vers : 124

إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Hakika siku ya Sabato (jumamosi) iliwekwa kwa wale waliohitilafiana kuhusu yeye (Ibrahimu) na dini yake. Na kwa hakika Mola wako atahukumu baina yao Siku ya Kiyama kuhusu yale waliyokuwa wakihitilafiana



Sure: ANNAHLI 

Vers : 125

ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Waite (walinganie watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako mlezi yeye anamjua zaidi aliyepotea katika njia yake, na yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka



Sure: ANNAHLI 

Vers : 126

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّـٰبِرِينَ

Na mkilipiza (kisasi), basi lipizeni sawa na vile mlivyoonewa, na kama mkisubiri, hakika hilo ni bora kwa wanaosubiri



Sure: ANNAHLI 

Vers : 127

وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ

Na subiri, na haiwi subira yako isipokuwa ni kwa ajili Allah tu, na usihuzunike kwa ya ajili yao, na usiwe katika dhiki kwa sababu ya vitimbi wanavyovifanya



Sure: ANNAHLI 

Vers : 128

إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ

Kwa hakika Allah yupo pamoja na wale wanaomcha (Allah), na wale wafanyao wema