وَتَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَأَكۡلِهِمُ ٱلسُّحۡتَۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na utawaona wengi kati yao wanakimbilia kwenye dhambi na uadui na ulaji wao wa vya haramu. Kwa yakini kabisa, ni maovu mno hayo waliyokuwa wanayatenda
لَوۡلَا يَنۡهَىٰهُمُ ٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ عَن قَوۡلِهِمُ ٱلۡإِثۡمَ وَأَكۡلِهِمُ ٱلسُّحۡتَۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ
Mbona wachamungu (wao) na wanazuoni (wao) hawawakatazi kusema maneno ya dhambi na ulaji wao wa vya haramu? Kwa yakini kabisa, ni maovu mno hayo waliyokuwa wanayafanya
وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ يَدُ ٱللَّهِ مَغۡلُولَةٌۚ غُلَّتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْۘ بَلۡ يَدَاهُ مَبۡسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيۡفَ يَشَآءُۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ طُغۡيَٰنٗا وَكُفۡرٗاۚ وَأَلۡقَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ كُلَّمَآ أَوۡقَدُواْ نَارٗا لِّلۡحَرۡبِ أَطۡفَأَهَا ٱللَّهُۚ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادٗاۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Na Wayahudi walisema: Mkono wa Allah umefumba (kwa ubahili). Mikono yao ndio iliyofumba na wamelaaniwa (kwasababu ya hayo) waliyoyasema. Bali mikono yake (Allah) ni yenye kukunjuka; anatoa atakavyo. Na kwa yakini kabisa, yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidisha wengi wao uasi na ukafiri. Na tumerusha baina yao uadui na chuki mpaka Siku ya Kiama. Kila wanapowasha moto wa vita, Allah anauzima. Na wanakimbilia kufanya uovu katika ardhi. Na Allah hawapendi wafanyao uovu
وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَكَفَّرۡنَا عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَلَأَدۡخَلۡنَٰهُمۡ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Na lau kama Watu wa Kitabu wangeamini na wakawa wachamungu bila shaka tungewafutia makosa yao, na tungewaingiza kwenye Pepo za neema
وَلَوۡ أَنَّهُمۡ أَقَامُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِم مِّن رَّبِّهِمۡ لَأَكَلُواْ مِن فَوۡقِهِمۡ وَمِن تَحۡتِ أَرۡجُلِهِمۚ مِّنۡهُمۡ أُمَّةٞ مُّقۡتَصِدَةٞۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ سَآءَ مَا يَعۡمَلُونَ
Na lau kama wangeliisimamisha Taurati na Injili na yote waliyo-teremshiwa kutoka kwa Mola wao Mlezi (kwa kuyafanyia kazi), bila shaka wangekula vitokavyo juu yao na vya chini ya miguu yao (wangepata riziki zao kwa wasaa na maisha yao kuwa ya furaha). Miongoni mwao wapo wenye msimamo wa wastani, na wengi miongoni mwao wayafanyayo ni mabaya sana
۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ بَلِّغۡ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۖ وَإِن لَّمۡ تَفۡعَلۡ فَمَا بَلَّغۡتَ رِسَالَتَهُۥۚ وَٱللَّهُ يَعۡصِمُكَ مِنَ ٱلنَّاسِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Ewe Mtume, fikisha uliyotere-mshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na usipofanya (hivyo) basi (utakuwa) hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda dhidi ya watu. Hakika, Allah hawaongozi (njia ya sawa) watu makafiri
قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَسۡتُمۡ عَلَىٰ شَيۡءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ طُغۡيَٰنٗا وَكُفۡرٗاۖ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu, hamna lolote (la maana) mpaka muisimamishe Taurati na Injili na yote mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na hakika ulioteremshiwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na kwa yakini kabisa, yale uliyoteremshiwa na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلصَّـٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Hakika, walioamini na Wayahudi na Wasabai[1] na Wanaswara (Wakristo); waliomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wakatenda mema, basi hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika.[2]
1- - Ni watu wanaoabudu Malaika/nyota
2- - Aya hapa inawatangazia watu wa dini zote kwamba salama yao huko Akhera ni kuwa na Imani sahihi ya Uislamu inayosisitiza kumuamini Allah kwa usahihi wake na Siku ya Kiama na kutenda amali njema. Aya haimaanishi kuwa dini zote ni sahihi kama baadhi ya watu wanavyodhani. Ikumbukwe kuwa Aya ya 85 ya Sura Aal-imran (3) inaweka wazi kuwa dini inayokubalika ni Uislamu tu na asiyekuwa na Imani hiyo atakuwa katika hasara huko Akhera.
لَقَدۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ رُسُلٗاۖ كُلَّمَا جَآءَهُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُهُمۡ فَرِيقٗا كَذَّبُواْ وَفَرِيقٗا يَقۡتُلُونَ
Kwa hakika kabisa, tulichukua ahadi ya Wana wa Israili[1] na tuliwapelekea Mitume. Kila alipowajia Mtume na yale ambayo nafsi zao haziyapendi wengine waliwapinga na wengine waliwauwa
1- - Ya kumuamini Allah na Mtume wake.
وَحَسِبُوٓاْ أَلَّا تَكُونَ فِتۡنَةٞ فَعَمُواْ وَصَمُّواْ ثُمَّ تَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ ثُمَّ عَمُواْ وَصَمُّواْ كَثِيرٞ مِّنۡهُمۡۚ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ
Na walidhani kuwa hakutakuwa na mtihani (adhabu yoyote); kwasababu hiyo wakawa vipofu (wa kutoiona haki) na viziwi (wa kutoisikia haki). Kisha Allah akapokea Toba yao. Kisha wengi katika wao wakawa tena vipofu na viziwi. Na Allah ni Mwenye kuyaona hayo wayatendayo
لَقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۖ إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ
Kwa hakika kabisa, wamekufuru waliosema: Hakika, Allah ni Masihi Mwana wa Mariamu. Na Masihi (mwenyewe) alisema: Enyi Wana wa Israili, muabuduni Allah, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Ilivyo ni kwamba, yeyote anayemfanyia ushirika Allah, hakika Allah amemharamishia Pepo, na makazi yake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na watetezi wowote
لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَٰثَةٖۘ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّآ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ وَإِن لَّمۡ يَنتَهُواْ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Kwa hakika kabisa, wamekufuru waliosema: Allah ni Watatu wa utatu. Na (ilivyo ni kwamba) hakuna yeyote mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Muabudiwa Mmoja tu. Na wasipokoma (kusema) hayo wanayoyasema, kwa yakini kabisa itawashika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo sana
أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى ٱللَّهِ وَيَسۡتَغۡفِرُونَهُۥۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hivi, ni kwanini hawatubu kwa Allah na kumuomba msamaha? Na Allah ni Mwingi wa kusamehe mwenye kurehemu
مَّا ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٞۖ كَانَا يَأۡكُلَانِ ٱلطَّعَامَۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ ٱنظُرۡ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ
Hakuwa Masihi Mwana wa Mariamu isipokuwa ni Mtume tu. Walishapita Mitume (wengi) kabla yake, na mama yake ni mwanamke msadikishaji mno. (Wote wawili) Walikuwa wanakula chakula (kama binadamu wengine). Angalia namna tunavyowabainishia (watu) hoja (mbalimbali), kisha angalia namna wanavyopotoshwa!
قُلۡ أَتَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗاۚ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Sema: Hivi, mnaaabudu, badala ya Allah, wale (Miungu) ambao hawawezi kukuleteeni madhara wala manufaa? Na Allah ndiye hasa Msikiaji sana, Mwenye kujua
قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓاْ أَهۡوَآءَ قَوۡمٖ قَدۡ ضَلُّواْ مِن قَبۡلُ وَأَضَلُّواْ كَثِيرٗا وَضَلُّواْ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu, msivuke mipaka katika dini yenu bila ya haki, na msifuate utashi wa nafsi wa watu waliokwishapotea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia ya sawa
لُعِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُۥدَ وَعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ
Wamelaaniwa waliokufuru miongoni mwa Wana wa Israili kupitia ulimi wa Daudi na Issa Mwana wa Mariamu. Hayo ni kwasababu waliasi na walikuwa wanachupa mipaka
كَانُواْ لَا يَتَنَاهَوۡنَ عَن مُّنكَرٖ فَعَلُوهُۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Walikuwa hawakatazani maovu waliyokuwa wakiyafanya. Kwa yakini kabisa, ni maovu makubwa sana hayo waliyokuwa wanayafanya!
تَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يَتَوَلَّوۡنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ لَبِئۡسَ مَا قَدَّمَتۡ لَهُمۡ أَنفُسُهُمۡ أَن سَخِطَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَفِي ٱلۡعَذَابِ هُمۡ خَٰلِدُونَ
Utawaona wengi wao wana-wafanya makafiri marafiki (wao) wa ndani. Kwa yakini kabisa, ni maovu sana hayo yaliyotangulia kufanywa na nafsi zao hadi Allah amewakasirikia, na watadumu milele katika adhabu
وَلَوۡ كَانُواْ يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلنَّبِيِّ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مَا ٱتَّخَذُوهُمۡ أَوۡلِيَآءَ وَلَٰكِنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ
Na lau wangelimwamini Allah, na (huyu) Nabii, na yaliyoteremshwa kwake, wasingewafanya hao (makafiri) wapenzi wa ndani, lakini wengi katika wao ni waovu