Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 27

۞وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَيۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانٗا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأٓخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Na wasomee, kwa haki, habari za wana wawili wa Adamu walipotoa sadaka, basi ikakubaliwa ya mmoja wao, na ya mwingine haikukubaliwa. (Aliyekataliwa sadaka yake) Aka-sema: Kwa Yakini kabisa, nitakuua. (Yule aliyekubaliwa sadaka yake) Akasema: Ilivyo ni kwamba, Allah anawakubalia wacha Mungu[1]


1- - Hapa hakuyasema haya kumwambia ndugu yake kwa lengo la majigambo na majivuno. Lakini aliyasema hayo kwa lengo la kumshawishi ndugu yake aache uovu na amuelekee Allah kwa unyenyekevu ili akubaliwe ibada zake.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 28

لَئِنۢ بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقۡتُلَنِي مَآ أَنَا۠ بِبَاسِطٖ يَدِيَ إِلَيۡكَ لِأَقۡتُلَكَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ukininyooshea mkono wako ili kuniua, mimi sitakunyooshea mkono wangu nikuue. Kwa hakika, mimi ninamuogopa Allah, Mola wa walimwengu wote



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 29

إِنِّيٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثۡمِي وَإِثۡمِكَ فَتَكُونَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِۚ وَذَٰلِكَ جَزَـٰٓؤُاْ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Mimi ninataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako ili uwe miongoni mwa watu wa motoni. Na hayo ndio malipo ya madhalimu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 30

فَطَوَّعَتۡ لَهُۥ نَفۡسُهُۥ قَتۡلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Basi nafsi yake ikamshawishi kumuua ndugu yake na akamuua na akajikuta ni miongoni mwa waliokula hasara



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 31

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابٗا يَبۡحَثُ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُۥ كَيۡفَ يُوَٰرِي سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٰرِيَ سَوۡءَةَ أَخِيۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ

Basi hapo Allah akampeleka kunguru anayefukua ardhini ili amuoneshe namna ya kusitiri (kuzika) mwili wa nduguye. Akasema: “Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa kama huyu kunguru nikasitiri mwili wa ndugu yangu?”. Basi akawa ni miongoni mwa wenye kujuta