وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na ambao wamekufuru na wakazikadhibisha Aya zetu, hao ni watu wa motoni, wataishi humo milele
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Hao ndio walionunua uhai wa dunia kwa Akhera, kwahiyo hawatapunguziwa adhabu na wala hawatanusuriwa
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٌ أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Hakika, waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao wanastahiki laana ya Allah, na ya Malaika na (laana) ya watu wote
خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Humo watakaa daima. Hawatapunguziwa adhabu na hawatapewa muda (wa kuomba radhi)
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا
Hakika wale wanaokula mali za Yatima kwa dhulma kwa hakika wanakula moto (kutia) matumboni mwao na watauingia Motoni
وَمَن يَقۡتُلۡ مُؤۡمِنٗا مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَٰلِدٗا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمٗا
Na yeyote anayemuua Muumini (Muislamu) kwa kukusudia basi malipo yake ni Jahanamu, ataishi humo milele na Allah amemghadhibikia na amemlaani na amemuandalia adhabu kubwa kabisa
وَقَدۡ نَزَّلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أَنۡ إِذَا سَمِعۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ يُكۡفَرُ بِهَا وَيُسۡتَهۡزَأُ بِهَا فَلَا تَقۡعُدُواْ مَعَهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦٓ إِنَّكُمۡ إِذٗا مِّثۡلُهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡكَٰفِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا
Na kwa hakika, (Allah) amekuteremshieni katika kitabu (Qur’ani) kwamba msikiapo Aya za Allah zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao (hao wafanyao hivyo), mpaka waingie katika mazungumzo mengine[1]. Hakika, mkikaa nao nanyi mtakuwa kama wao. Hakika, Allah atawakusanya Wanafiki na Makafiri wote katika Jahanamu
1- - Allah ametaja suala hili katika Aya ya 68 ya Sura Al-an-aam (6) inayosema kwamba “Na ukiwaona wanaozisema vibaya Aya zetu usikae nao…”.
إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا
Hakika, wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa la Moto, na hutampata yeyote wa kuwanusuru
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Na waliokufuru na kuzikanusha Aya zetu (tulizoziteremsha kwa Mitume wetu), hao ndio watu wa Motoni
لَقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۖ إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ
Kwa hakika kabisa, wamekufuru waliosema: Hakika, Allah ni Masihi Mwana wa Mariamu. Na Masihi (mwenyewe) alisema: Enyi Wana wa Israili, muabuduni Allah, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Ilivyo ni kwamba, yeyote anayemfanyia ushirika Allah, hakika Allah amemharamishia Pepo, na makazi yake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na watetezi wowote
قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ
(Allah) Akasema (kumwambia Ibilisi kwamba): Toka humo (Peponi) ukiwa umechukiwa, umelaaniwa. Kwa yakini kabisa, yeyote atakayekufuata wewe miongoni mwao hakika nitaijaza Jahanamu kwa (kukutumbukizeni humo) nyinyi nyote
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wale waliokadhibisha Aya zetu na kuzifanyia kiburi hao ni watu wa motoni, watakaa humo milele
قَالَ ٱدۡخُلُواْ فِيٓ أُمَمٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِكُم مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ فِي ٱلنَّارِۖ كُلَّمَا دَخَلَتۡ أُمَّةٞ لَّعَنَتۡ أُخۡتَهَاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا ٱدَّارَكُواْ فِيهَا جَمِيعٗا قَالَتۡ أُخۡرَىٰهُمۡ لِأُولَىٰهُمۡ رَبَّنَا هَـٰٓؤُلَآءِ أَضَلُّونَا فَـَٔاتِهِمۡ عَذَابٗا ضِعۡفٗا مِّنَ ٱلنَّارِۖ قَالَ لِكُلّٖ ضِعۡفٞ وَلَٰكِن لَّا تَعۡلَمُونَ
(Allah) Atasema: Ingieni Motoni (nyinyi) pamoja na mataifa yaliyopita kabla yenu, ambao ni majini na watu. Kila umma unapoingia utawalaani (umma) ndugu yake (mwenzake) mpaka watakapokusanyika humo wote kwa pamoja, watasema wa mwisho wao (kuwashitaki) wa mwanzo wao (kwamba): “Ewe Mola wetu Mlezi, hawa ndio waliotupoteza, basi wape adhabu ya moto maradufu”. (Allah) Atasema: Kila mmoja wenu ana (adhabu) mara dufu na lakini hamjui
وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ
Na watasema wa mwanzo wao kuwaambia wa mwisho wao (kwamba): Nyinyi hamkuwa na fadhila yoyote kwetu, basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدٗا فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡخِزۡيُ ٱلۡعَظِيمُ
Je, hawajui ya kwamba anayemfanyia uadui Allah na Mtume wake, basi huyo atapata Moto wa Jahanamu adumu humo? Hiyo ndiyo hasa hizaya kubwa kabisa
وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ هِيَ حَسۡبُهُمۡۚ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ
Allah amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahanamu wakidumu humo milele. Hilo ndilo linalowatosha, na Allah amewalaani na watapata adhabu ya kudumu
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa tu wale Mola wako mlezi amewarehemu (wakaamini); na Allah amewaumba hivyo. Na neno la Mola wako mlezi litatimia: Kwe hakika nitaijaza Jahannam miongoni mwa majini na watu wote kwa pamoja
مَّن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعَاجِلَةَ عَجَّلۡنَا لَهُۥ فِيهَا مَا نَشَآءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلۡنَا لَهُۥ جَهَنَّمَ يَصۡلَىٰهَا مَذۡمُومٗا مَّدۡحُورٗا
Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa
ثُمَّ نُنَجِّي ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّنَذَرُ ٱلظَّـٰلِمِينَ فِيهَا جِثِيّٗا
Kisha tutawaokoa wale walio mcha Allah; na tutawaacha mad-haalimu humo wamepiga magoti
إِنَّهُۥ مَن يَأۡتِ رَبَّهُۥ مُجۡرِمٗا فَإِنَّ لَهُۥ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Hakika atakayemjia Mola wake Mlezi naye ni muovu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi
۞وَمَن يَقُلۡ مِنۡهُمۡ إِنِّيٓ إِلَٰهٞ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجۡزِيهِ جَهَنَّمَۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu
إِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمۡ لَهَا وَٰرِدُونَ
Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Allah ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu
لَوۡ كَانَ هَـٰٓؤُلَآءِ ءَالِهَةٗ مَّا وَرَدُوهَاۖ وَكُلّٞ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Wangekuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo
وَٱلَّذِينَ سَعَوۡاْ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Na wanao jitahidi kuzipinga Aya zetu hao ndio watu wa Motoni
فَكُبۡكِبُواْ فِيهَا هُمۡ وَٱلۡغَاوُۥنَ
Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
وَجُنُودُ إِبۡلِيسَ أَجۡمَعُونَ
Na majeshi ya Ibilisi yote
إِنَّ ٱللَّهَ لَعَنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمۡ سَعِيرًا
Hakika Allah amewalaani makafiri na amewaandalia Moto unao waka kwa nguvu
خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ لَّا يَجِدُونَ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Watadumu humo milele. Hawampati mlinzi wala wa kuwa-nusuru
هَٰذَاۚ وَإِنَّ لِلطَّـٰغِينَ لَشَرَّ مَـَٔابٖ
Ndiyo hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marejeo mabaya kabisa;
جَهَنَّمَ يَصۡلَوۡنَهَا فَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ
Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia