وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ
Na miongoni mwa watu wapo wanaosema[1] kuwa: “Tumemuamini Allah na Siku ya Mwisho” na[2] sio waumini (wa kweli)
1- - Kwa maneno tu.
2- - Ukweli ni kwamba…
يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ
Wanamhadaa Allah na wale walioamini. Na hawahadai isipokuwa nafsi zao tu na wao hawatambui
فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ
Ndani ya nyoyo zao kuna ugonjwa, na Allah akawaongezea ugonjwa. Na wanastahiki adhabu kali kwa uongo waliokuwa wanaufanya
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ قَالُوٓاْ إِنَّمَا نَحۡنُ مُصۡلِحُونَ
Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ardhini wanasema: Hapana, bali sisi niwafanyaji mazuri
أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡمُفۡسِدُونَ وَلَٰكِن لَّا يَشۡعُرُونَ
Elewa! Kwa yakini, wao ndio waharibifu hasa na lakini hawatambui
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ كَمَآ ءَامَنَ ٱلنَّاسُ قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ كَمَآ ءَامَنَ ٱلسُّفَهَآءُۗ أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلسُّفَهَآءُ وَلَٰكِن لَّا يَعۡلَمُونَ
Na wanapoambiwa: Kuweni wenye kuamini kama walivyoamini watu, wanasema: Ah! Hivi tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Elewa! Wao ndio wapumbavu hasa na lakini hawajui
وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوۡاْ إِلَىٰ شَيَٰطِينِهِمۡ قَالُوٓاْ إِنَّا مَعَكُمۡ إِنَّمَا نَحۡنُ مُسۡتَهۡزِءُونَ
Na wanapokutana na walioamini wanasema: Tumeamini. Na wanapokuwa faragha na mashetani wao wanasema: Sisi tuko pamoja nanyi, tunachokifanya sisi tunacheza shere tu
ٱللَّهُ يَسۡتَهۡزِئُ بِهِمۡ وَيَمُدُّهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Allah anawacheza shere wao, na anawapa muda zaidi katika kupotoka kwao huku wakiwa wanatangatanga
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَٰرَتُهُمۡ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ
Hao ndio walioununua upotevu kwa uongofu. Biashara yao haikuleta faida, na hawakuwa waongofu
وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ
Na miongoni mwa watu wapo ambao zinakuvutia kauli zao katika maisha ya dunia, na wanamshuhudisha Allah juu ya yaliyo moyoni mwake hali yeye ni mpingaji mno
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ
Na anapoondoka (kwako) anahangaika huku na kule ardhini ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na vizazi. Na Allah hapendi ufisadi
وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ
Na wanapoambiwa; Muogopeni Allah hupandwa na mori wa kufanya uovu. Basi kitakachowatosha ni Jahanamu na ni makazi mabaya mno
وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ نَافَقُواْۚ وَقِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ قَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوِ ٱدۡفَعُواْۖ قَالُواْ لَوۡ نَعۡلَمُ قِتَالٗا لَّٱتَّبَعۡنَٰكُمۡۗ هُمۡ لِلۡكُفۡرِ يَوۡمَئِذٍ أَقۡرَبُ مِنۡهُمۡ لِلۡإِيمَٰنِۚ يَقُولُونَ بِأَفۡوَٰهِهِم مَّا لَيۡسَ فِي قُلُوبِهِمۡۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يَكۡتُمُونَ
Na ili awapambanue wanafiki, na wakaambiwa: njooni mpigane katika njia ya Allah au lindeni. Wakasema: lau tungejua kuwa kuna mapigano bila ya shaka tungelikufuateni. wao siku ile walikuwa wako karibu zaidi na ukafiri kuliko imani, wanasema kwa midomo yao yasiyokuwemo nyoyoni mwao, na Allah ni mjuzi zaidi kwa yale wanayoyaficha
ٱلَّذِينَ قَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ وَقَعَدُواْ لَوۡ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُواْۗ قُلۡ فَٱدۡرَءُواْ عَنۡ أَنفُسِكُمُ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Hao ndio ambao walisema kuhusu ndugu zao na wao wakiwa wamekaa: Lau wangelitutii sisi wasingeuliwa sema: basi ziondoleeni nafsi zenu kifo ikiwa nyinyi ni wa kweli
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّـٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا
Je, hukuwaona wanaodai kuwa wameamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako wanataka wakahukumiane kwa Twaghuti[1], na ilhali wameamrishwa wamkatae? Na shetani anataka kuwapoteza upotevu wa mbali
1- - Twaghuti ni kila kinachoabudiwa na kutiiwa badala ya Allah ikiwa ni pamoja na shetani, sanamu, mzimu n.k.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيۡتَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودٗا
Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allah na (njooni) kwa Mtume, utawaona wanafiki wanakuwekea pingamizi nyingi
فَكَيۡفَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّآ إِحۡسَٰنٗا وَتَوۡفِيقًا
Basi itakuwaje msiba utakapowafika kwasababu ya yale yaliyotangulia kufanywa na mikono yao, kisha wakakujia huku wakiapa kwa Allah kwamba: Hatukukusudia ila tu kufanya yaliyo mazuri na kupatanisha?
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا
Hao ndio ambao Allah anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi wapuuze na wape mawaidha na waambie katika nafsi zao maneno mazito
وَإِنَّ مِنكُمۡ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنۡ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَالَ قَدۡ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيَّ إِذۡ لَمۡ أَكُن مَّعَهُمۡ شَهِيدٗا
Na hakika kabisa, wapo miongoni mwenu wanaosuasua (wanaobaki nyuma kwasababu ya kuona uzito wa kutoka kwenda vitani). Ukikupateni msiba wanasema: Hakika, Allah amenineemesha kwa kuwa sikuwa pamoja nao
وَلَئِنۡ أَصَٰبَكُمۡ فَضۡلٞ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمۡ تَكُنۢ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُۥ مَوَدَّةٞ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ مَعَهُمۡ فَأَفُوزَ فَوۡزًا عَظِيمٗا
Na ikikufikieni fadhila itokayo kwa Allah kwa hakika kabisa husema, kama vile hapakuwa na mapenzi yoyote baina yenu na baina yao, kwamba: Laiti nami ningekuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa
۞فَمَا لَكُمۡ فِي ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِئَتَيۡنِ وَٱللَّهُ أَرۡكَسَهُم بِمَا كَسَبُوٓاْۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهۡدُواْ مَنۡ أَضَلَّ ٱللَّهُۖ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا
Basi mna nini nyinyi mmegawanyika makundi mawili kuhusu wanafiki, na ilhali Allah amewageuza (na kurudi kwenye ukafiri) kwasababu ya yale waliyo-yachuma? Hivi mnataka kuwaongoa ambao Allah amewapoteza? Na yeyote ambaye Allah amempoteza hutapata njia (ya kumuongoza)
وَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَآءٗۖ فَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ أَوۡلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡۖ وَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرًا
Wametamani lau mngekufuru kama walivyokufuru wao ili muwe sawa. Basi msiwafanye marafiki wa karibu miongoni mwao mpaka wahame kwa ajili ya dini ya Allah. Basi kama wakikengeuka washikeni (mateka) na waueni popote mtakapowakuta, na msifanye miongoni mwao rafiki wa karibu wala msaidizi
إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٌ أَوۡ جَآءُوكُمۡ حَصِرَتۡ صُدُورُهُمۡ أَن يُقَٰتِلُوكُمۡ أَوۡ يُقَٰتِلُواْ قَوۡمَهُمۡۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمۡ عَلَيۡكُمۡ فَلَقَٰتَلُوكُمۡۚ فَإِنِ ٱعۡتَزَلُوكُمۡ فَلَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ وَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سَبِيلٗا
Isipokuwa wale ambao wana-husiana na watu ambao kati yenu na wao kuna mkataba au wamekujieni huku nyoyo zao zikiona tabu kupigana nanyi au kupigana na watu wao. Na Allah angetaka angeliwapa nguvu dhidi yenu wakakupigeni. Basi wakiachana nanyi na wasipigane nanyi na wakakuleteeni amani (wakakutangazieni amani), basi Allah hakukupeni njia (ruhusa ya kupiganana nao)
سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأۡمَنُوكُمۡ وَيَأۡمَنُواْ قَوۡمَهُمۡ كُلَّ مَا رُدُّوٓاْ إِلَى ٱلۡفِتۡنَةِ أُرۡكِسُواْ فِيهَاۚ فَإِن لَّمۡ يَعۡتَزِلُوكُمۡ وَيُلۡقُوٓاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡۚ وَأُوْلَـٰٓئِكُمۡ جَعَلۡنَا لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا
Mtawakuta wengine wanataka kukaa nanyi kwa amani (kwa kuonesha kuwa nao wameamini) na kukaa kwa amani na watu wao (kwa kuwaonesha kuwa bado wao ni makafiri). Kila wanaporudishwa kwenye fitina (ukafiri) wanaporomoshwa (wanaburuzwa na kurudi kwa kasi kubwa) kwenye ukafiri huo. Basi kama hawakukuacheni na hawakukutangazieni amani na hawakuizuia mikono yao (wakaacha kukupigeni), basi wakamateni na waueni popote mtakapowakuta, na hao tumekupeni hoja ya wazi (ya kuwashambulia, kuwapiga, kuwaua na kuwakamata mateka)
بَشِّرِ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ بِأَنَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمًا
Wape bishara[1] wanafiki kwamba wanayo adhabu iumizayo mno
1- - Bishara ni taarifa ya jambo jema linaloleta faraja. Adhabu sio jambo jema la kutia faraja, lakini hapa limetumika kwa wanafiki kwa madhumuni ya kuwakejeli na kuwadhihaki.
ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا
(Wanafiki) Ambao wanawafanya makafiri kuwa marafiki badala ya Waumini (wenzao). Hivi wanatafuta heshima kwao? Basi hakika, heshima yote ni miliki ya Allah tu
وَقَدۡ نَزَّلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أَنۡ إِذَا سَمِعۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ يُكۡفَرُ بِهَا وَيُسۡتَهۡزَأُ بِهَا فَلَا تَقۡعُدُواْ مَعَهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦٓ إِنَّكُمۡ إِذٗا مِّثۡلُهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡكَٰفِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا
Na kwa hakika, (Allah) amekuteremshieni katika kitabu (Qur’ani) kwamba msikiapo Aya za Allah zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao (hao wafanyao hivyo), mpaka waingie katika mazungumzo mengine[1]. Hakika, mkikaa nao nanyi mtakuwa kama wao. Hakika, Allah atawakusanya Wanafiki na Makafiri wote katika Jahanamu
1- - Allah ametaja suala hili katika Aya ya 68 ya Sura Al-an-aam (6) inayosema kwamba “Na ukiwaona wanaozisema vibaya Aya zetu usikae nao…”.
ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا
Ambao wanakuvizieni. Mkipata ushindi unaotoka kwa Allah wanasema: Si tulikuwa pamoja na nyinyi? Na ikiwa makafiri wamepata sehemu ndogo ya ushindi wanasema: Si tulikusimamieni na kukukingeni dhidi ya Waislamu? Basi Allah atahukumu baina yenu Siku ya Kiama. Na Allah hatawapa makafiri njia (ya kuwashinda) Waislamu
إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمۡ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلٗا
Hakika, wanafiki wanamhadaa Allah, naye ni mwenye kuwahadaa (pia). Na wanaposimama kwenda kuswali wanasimama wakiwa wavivu, wanajionyesha kwa watu (kwamba nao ni Waislamu) na hawamtaji Allah isipokuwa kidogo sana
مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا
Wanayumba yumba baina ya hayo (ya hali mbili za imani na unafiki). Hawako kwa hawa (Waislamu) na hawako kwa hawa (makafiri). Na yeyote ambaye Allah amempoteza hutampatia njia yoyote (ya kumuongoa)