يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِيٓ أُوفِ بِعَهۡدِكُمۡ وَإِيَّـٰيَ فَٱرۡهَبُونِ
Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu ambazo nimekuneemesheni, na tekelezeni ahadi zangu, nami nitekeleze ahadi zenu, naniogopeni mimi tu
وَءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلۡتُ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُمۡ وَلَا تَكُونُوٓاْ أَوَّلَ كَافِرِۭ بِهِۦۖ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗا وَإِيَّـٰيَ فَٱتَّقُونِ
Na yaaminini yale niliyo-yateremsha yakiwa yanasadikisha hayo mliyonayo, na msiwe wa kwanza kuyakufuru, na msizi-badilishe Aya zangu kwa thamani ndogo, na mniogope mimi tu
وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na msichanganye haki na batili na msifiche haki na ilhali mnajua
وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ
Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wanaorukuu
۞أَتَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبِرِّ وَتَنسَوۡنَ أَنفُسَكُمۡ وَأَنتُمۡ تَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Je, mnaamrisha watu kutenda wema na mnajisahau, na ilhali nyinyi mnakisoma kitabu? Je, hamtumii akili?
وَٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلۡخَٰشِعِينَ
Na ombeni msaada kwa kusubiri na kuswali. Na kwa hakika kabisa, hiyo Swala ni nzito mno isipokuwa kwa wanyenyekevu tu
ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَأَنَّهُمۡ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ
Ambao wana yakini kwamba watakutana na Mola wao, na kwamba kwake tu watarejea
يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu nilizo kuneemesheni, na kwamba mimi nimekufanyeni bora kuliko walimwengu (wa zama zenu)
وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا يُؤۡخَذُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaisaidia chochote nafsi nyingine, na wala hautakubaliwa uombezi wowote kwa nafsi hiyo (kumuombea mwengine), na wala haitachukuliwa fidia yoyote kwa nafsi hiyo, nao hawatanusuriwa
وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kutoka kwenye mateso ya Firauni na watu wake waliokupeni adhabu mbaya kabisa; wakiwauwa watoto wenu wanaume kwa kuwachinjachinja na wakiwaacha hai watoto wenu wanawake. Na katika hayo kuna mtihani mkubwa sana kwenu kutoka kwa Mola wenu
وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ
Na (kumbukeni) tulipokut-enganishieni bahari tukakuokoeni na tukawazamisha watu wa Firauni na nyinyi mkitazama
وَإِذۡ وَٰعَدۡنَا مُوسَىٰٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ
Na (kumbukeni) tulipoahidiana na Musa siku arobaini, kisha nyinyi mkamfanya ndama (kuwa Mungu) baada ya hapo, na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)”
ثُمَّ عَفَوۡنَا عَنكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Kisha tukakusameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru
وَإِذۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡفُرۡقَانَ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na (kumbukeni) tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِنَّكُمۡ ظَلَمۡتُمۡ أَنفُسَكُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلۡعِجۡلَ فَتُوبُوٓاْ إِلَىٰ بَارِئِكُمۡ فَٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ عِندَ بَارِئِكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Na (kumbukeni) Musa alip-owaambia watu wake (kuwa): Enyi watu wangu, kwa hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kumfanya kwenu ndama Mungu. Basi tubieni kwa Mola wenu na uaneni. Hilo ni bora kwenu mbeleya Muumba wenu. Allah akakubali toba yenu. Kwa hakika, yeye ni Mwingi wa kukubali toba, Mwingi wa rehema
وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡكُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ
Na (kumbukeni) mliposema (kumwambia Mtume Musa kuwa): Ewe Musa, hatutakuamini mpaka tumuone Allah waziwazi. Basi ukakuchukueni (ukakuteketezeni) moto wa radi na hali mnatazama
ثُمَّ بَعَثۡنَٰكُم مِّنۢ بَعۡدِ مَوۡتِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru
وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡغَمَامَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Na tukakufunikeni kivuli cha mawingu na tukakuteremshieni Mana na Salwa, (na kukuambieni): Kuleni katika vitu vizuri tulivyokuruzukuni, na hawakutudhulumu sisi, lakini walikuwa wanajidhulumu wenyewe
وَإِذۡ قُلۡنَا ٱدۡخُلُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ فَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ رَغَدٗا وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُولُواْ حِطَّةٞ نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطَٰيَٰكُمۡۚ وَسَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na (kumbuka) tuliposema (kuwaambia Wana wa Israili kuwa): Ingieni katika mji huu. Kuleni humo mtakavyo (na) kwa wasaa, naingieni katika lango mkiwa mmesujudu, na sememeni: “Ombi letu ni kusamehewa dhambi”, tutakusameheni makosa yenu. Na tutawazidishia watendao mazuri
فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَنزَلۡنَا عَلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Basi waliodhulumu walibadilisha kauli (nyingine) sio ile waliyoambiwa. Kwa sababu hiyo, tuliwateremshia waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya uovu waliokuwa wakiufanya
۞وَإِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ فَقُلۡنَا ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنفَجَرَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۖ كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ مِن رِّزۡقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Na kumbuka Musa alipo-waombea maji watu wake tukam-wambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. (Alipolipiga) Zikabubujika kutoka katika jiwe hilo chemchemi kumi na mbili. Kila watu walijua mahali pao pa (kuchota maji ya) kunywa. (Tuliwaambia:) Kuleni na kunyweni katika riziki za Allah, na msifanye uovu katika ardhi
وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نَّصۡبِرَ عَلَىٰ طَعَامٖ وَٰحِدٖ فَٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُخۡرِجۡ لَنَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۢ بَقۡلِهَا وَقِثَّآئِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَاۖ قَالَ أَتَسۡتَبۡدِلُونَ ٱلَّذِي هُوَ أَدۡنَىٰ بِٱلَّذِي هُوَ خَيۡرٌۚ ٱهۡبِطُواْ مِصۡرٗا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلۡتُمۡۗ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ وَٱلۡمَسۡكَنَةُ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ
Na (kumbukeni) mliposema: Ewe Musa, hatutaweza kuvumilia (kula) chakula cha aina moja tu. Basi tuombee kwa Mola wako atutolee katika vile ambavyo ardhi inaotesha, ikiwa ni pamoja na mboga mboga zake na matango yake na vitunguu saumu vyake na dengu zake na vitunguu maji vyake. Musa akasema: Hivi, mnataka kubadilisha ambacho ni duni sana kwa ambacho ni bora zaidi? Shukeni mjini. Huko mtapata hivyo mlivyovitaka. Na wakapigwa chapa ya udhalili na umaskini na wakastahiki ghadhabu za Allah. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikufuru Aya za Allah na wakiwaua Mitume pasina haki yoyote. Hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao, na walikuwa wakichupa mipaka
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلنَّصَٰرَىٰ وَٱلصَّـٰبِـِٔينَ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Hakika, Walioamini na Waya-hudi na Wanasara na Wasabai; waliomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wakatenda matendo mema basi hao wanamalipo mbele ya Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika
وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi zenu na tukanyanyua (mlima) Turi juu yenu (tukakuambieni kuwa): Kichukueni kwanguvu tulichokupeni na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kuwa Wacha Mungu
ثُمَّ تَوَلَّيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۖ فَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَكُنتُم مِّنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Kisha mkageuka baada ya hayo. Na lau kama sio fadhila za Allah na rehema zake kwenu mngekuwa miongoni mwa wenye hasara
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِي ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ
Na, kwa hakika kabisa, mmewajua waliovuka mipaka miongoni mwenu katika (siku ya) Jumamosi, tukawaambia: Kuweni nyani dhalili
فَجَعَلۡنَٰهَا نَكَٰلٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهَا وَمَا خَلۡفَهَا وَمَوۡعِظَةٗ لِّلۡمُتَّقِينَ
Tukalifanya tukio hilo onyo kwa waliopo na wajao baada yake, na ni mazingatio kwa Wacha Mungu
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تَذۡبَحُواْ بَقَرَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَتَّخِذُنَا هُزُوٗاۖ قَالَ أَعُوذُ بِٱللَّهِ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Na (wakumbushe watu wako) pale Musa alipowaambia watu wake kuwa: Hakika, Allah anakuamrisheni kuchinja ng’ombe. Wakasema: Je, unatufanyia mzaha? Akasema: Naomba kinga kwa Allah anilinde nisiwe miongoni mwa wajinga
قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا فَارِضٞ وَلَا بِكۡرٌ عَوَانُۢ بَيۡنَ ذَٰلِكَۖ فَٱفۡعَلُواْ مَا تُؤۡمَرُونَ
Wakasema: Tuombee (kwa) Mola wako atubainishie ni ng’ombe gani? Akasema: Hakika yeye (Allah) anasema: Ni ng’ombe ambaye sio mpevu sana wala sio mchanga sana. Ni wakati baina ya sifa hizo. Basi tekelezeni mnayoamriwa
قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوۡنُهَاۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ صَفۡرَآءُ فَاقِعٞ لَّوۡنُهَا تَسُرُّ ٱلنَّـٰظِرِينَ
Wakasema: Tuulizie (kwa) Mola wako atubainishie ni warangi gani? Akasema: Hakika yeye (Allah) anasema: Ni ng’ombe wa rangi ya manjano iliyokoza anayewafurahisha wanaomtazama