Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 178

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِصَاصُ فِي ٱلۡقَتۡلَىۖ ٱلۡحُرُّ بِٱلۡحُرِّ وَٱلۡعَبۡدُ بِٱلۡعَبۡدِ وَٱلۡأُنثَىٰ بِٱلۡأُنثَىٰۚ فَمَنۡ عُفِيَ لَهُۥ مِنۡ أَخِيهِ شَيۡءٞ فَٱتِّبَاعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيۡهِ بِإِحۡسَٰنٖۗ ذَٰلِكَ تَخۡفِيفٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٞۗ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Enyi mlioamini, mmeandikiwa kulipa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Na aliyesamehewa jambo na ndugu yake (mtendewa jinai) basi fidia ifuatiliwe kwa wema na atekelezewe kwa uzuri. Hiyo ni tahafifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Na atakayekiuka baada ya hayo, basi yeye atapata adhabu iumizayo



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 179

وَلَكُمۡ فِي ٱلۡقِصَاصِ حَيَوٰةٞ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na mtakuwa na uhai (ulio bora) katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili muogope (msalimike)



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 190

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na piganeni na wanaokupigeni katika njia ya Allah, na msivuke mipaka (mkawashambulia wasiohusika), kwa sababu Allah hawapendi wavukao mipaka



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 191

وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِيهِۖ فَإِن قَٰتَلُوكُمۡ فَٱقۡتُلُوهُمۡۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na waueni popote mtaka-powakuta, na wafukuzeni popote watakapo kufukuzeni. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na msipigane nao mbele ya Msikiti Mtukufu mpaka wao wapigane nanyi humo. Wakipigana nanyi humo, basi waueni. Hivyo ndivyo yatakiwavyo kuwa malipo ya makafiri



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 192

فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ikiwa wataacha[1] basi Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu


1- - Kukuchokozeni au kupambana nanyi


Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 194

ٱلشَّهۡرُ ٱلۡحَرَامُ بِٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡحُرُمَٰتُ قِصَاصٞۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱعۡتَدُواْ عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu. Na kila kilicho kitukufu kitalipiwa kisasi. Na yeyote atakaye fanya uadui juu yenu, basi mlipeni sawa na uadui alioufanya kwenu. Na mcheni Allah na jueni kwamba Allah yupamoja na wamchao



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 15

وَٱلَّـٰتِي يَأۡتِينَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مِن نِّسَآئِكُمۡ فَٱسۡتَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِنَّ أَرۡبَعَةٗ مِّنكُمۡۖ فَإِن شَهِدُواْ فَأَمۡسِكُوهُنَّ فِي ٱلۡبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّىٰهُنَّ ٱلۡمَوۡتُ أَوۡ يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلٗا

Na wale wafanyao zinaa katika wake zenu[1] wawekeeni ushahidi wanaume wane miongoni mwenu, wakishuhudia (kwa macho yao), basi wazuieni majumbani mpaka kifo kiwakute au Allah awape njia nyingine[2]


1- - Neon Wake zenu hapa lina maana jinsia kwa maana kila mwanamke aliye chini ya himaya yako sawa awe mke dada, shangazi ama mtoto na sio wake tu kwa mana mliowaoa jumuhuri ya watu wa fiqih wamesema hivi


2- - Aya hii imebadilishwa hukumu yake na Aya ya pili ya Sura Annour (24) Aya ya 2


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 16

وَٱلَّذَانِ يَأۡتِيَٰنِهَا مِنكُمۡ فَـَٔاذُوهُمَاۖ فَإِن تَابَا وَأَصۡلَحَا فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابٗا رَّحِيمًا

Na wawili[1] wafanyao zinaa kati yenu waadhibuni, na kama watatubu na kujirekebisha basi waacheni, hakika Allah ni mwingi wa kupokea toba mwenye huruma sana


1- - Shekh Siidy katika tafsiri Almuyassar alipotafsiri aya hii ametaja rai tatu tofauti mwisho akasema kauli ya wanazuoni walio wengi ni kuwa kilichokusudiwa hapa ni Mwanamke ambaye hajaolewa na mwanaume ambaye hajaoa, sababu katika aya hii zimetaja hukumu mbili 1-kuwafungia majumbani 2-kuwakera na bila shaka aliyepata huku ya kwanza siye aliyepata hukumu ya pili na kawaida hukumu hukhafifishwa kwa bikra na kuwa kali kwa asiye bikra na kwa maana hiyo ilipoondolewa sheria iliyo katika hii ikawa kwa aliye bikra kuchapwa viboko na aliyeoa au kuolewa kupigwa mawe hadi kufa.


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 25

وَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ مِنكُمۡ طَوۡلًا أَن يَنكِحَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُم مِّن فَتَيَٰتِكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِكُمۚ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذۡنِ أَهۡلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِ مُحۡصَنَٰتٍ غَيۡرَ مُسَٰفِحَٰتٖ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخۡدَانٖۚ فَإِذَآ أُحۡصِنَّ فَإِنۡ أَتَيۡنَ بِفَٰحِشَةٖ فَعَلَيۡهِنَّ نِصۡفُ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ مِنَ ٱلۡعَذَابِۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَشِيَ ٱلۡعَنَتَ مِنكُمۡۚ وَأَن تَصۡبِرُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na asiyekuwa na uwezo wa kutosha miongoni mwenu (wa) kuoa wanawake waumini wenye kujihifadhi (waungwana), basi (oeni) wasichana (vijakazi)[1] wenu waumini mnaowamiliki. Na Allah anaijua sana imani yenu; nyinyi kwa nyinyi. Basi waoeni kwa idhini ya familia zao (zenye mamlaka ya kisheria ya kuwaozesha) na wapeni malipo (mahari) yao kwa wema wakiwa na lengo la kujihifadhi, wasio na lengo la kufanya uchafu (wa zinaa) wala kutengeneza wapenzi kinyume na sheria (mahawara). Basi wakishaingia katika hifadhi (ya ndoa), kama wakifanya uchafu (wa zinaa), basi adhabu yao ni nusu ya adhabu ya wanawake waungwana. Hayo ni kwa yule anayeogopa Zinaa miongoni mwenu. Na kama mtavumilia ni bora zaidi kwenu. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, mwenye huruma


1- - Kijakazi ni mtumwa wa kike. Mtumishi wa ndani wa kike nje ya utumwa hazingatiwi kuwa ni kijakazi.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 33

إِنَّمَا جَزَـٰٓؤُاْ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓاْ أَوۡ يُصَلَّبُوٓاْ أَوۡ تُقَطَّعَ أَيۡدِيهِمۡ وَأَرۡجُلُهُم مِّنۡ خِلَٰفٍ أَوۡ يُنفَوۡاْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِۚ ذَٰلِكَ لَهُمۡ خِزۡيٞ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Kwa hakika kabisa, malipo ya wale wanaopigana vita na Allah na Mtume wake[1] na wanakwenda kasi katika kufanya uharibifu duniani ni kuuawa bila ya huruma au kusulubiwa au kukatwa katwa mikono yao na miguu yao kwa kupishana au kutolewa katika nchi (na kupelekwa uhamishoni). Hiyo ni kwa sababu wanastahiki hizaya (fedheha) duniani, na huko Akhera watapata adhabu kubwa mno


1- - Kinachokusudiwa hapa ni kuupiga vita Uislamu na Waislamu.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 34

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِن قَبۡلِ أَن تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهِمۡۖ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Isipokuwa wale waliotubu kabla hamjawatia nguvuni. Basi jueni kwamba, kwa hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 38

وَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقۡطَعُوٓاْ أَيۡدِيَهُمَا جَزَآءَۢ بِمَا كَسَبَا نَكَٰلٗا مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, ikiwa ni malipo ya waliyoyachuma (waliyoyatenda) (na) ni adhabu ifundishayo kutoka kwa Allah. Na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 45

وَكَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفۡسَ بِٱلنَّفۡسِ وَٱلۡعَيۡنَ بِٱلۡعَيۡنِ وَٱلۡأَنفَ بِٱلۡأَنفِ وَٱلۡأُذُنَ بِٱلۡأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلۡجُرُوحَ قِصَاصٞۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٞ لَّهُۥۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na humo (ndani ya Taurati) tumewaandikia ya kwamba, roho kwa roho na jicho kwa jicho na pua kwa pua na sikio kwa sikio na jino kwa jino na majeraha ni kisasi. Basi atakayetoa sadaka (ya kusamehe haki yake kulipa kisasi) hiyo ni kafara yake (ya madhambi yake). Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio madhalimu



Capítulo: YUSUF 

Verso : 85

قَالُواْ تَٱللَّهِ تَفۡتَؤُاْ تَذۡكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوۡ تَكُونَ مِنَ ٱلۡهَٰلِكِينَ

Walisema: Wallahi, (hivi) huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walioangamia?



Capítulo: ANNAHLI 

Verso : 126

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّـٰبِرِينَ

Na mkilipiza (kisasi), basi lipizeni sawa na vile mlivyoonewa, na kama mkisubiri, hakika hilo ni bora kwa wanaosubiri



Capítulo: AL-ISRAA 

Verso : 33

وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَمَن قُتِلَ مَظۡلُومٗا فَقَدۡ جَعَلۡنَا لِوَلِيِّهِۦ سُلۡطَٰنٗا فَلَا يُسۡرِف فِّي ٱلۡقَتۡلِۖ إِنَّهُۥ كَانَ مَنصُورٗا

Wala msiuwe nafsi ambayo Allah amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa



Capítulo: AL-HAJJ 

Verso : 60

۞ذَٰلِكَۖ وَمَنۡ عَاقَبَ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِيَ عَلَيۡهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٞ

Ndio namna hivi. Na anaye lipiza mfano wa alivyo adhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hapana shaka Allah atamsaidia. Hakika Allah ni Msamehevu (tena) ni Mwingi wa msamaha



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 2

ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِي فَٱجۡلِدُواْ كُلَّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا مِاْئَةَ جَلۡدَةٖۖ وَلَا تَأۡخُذۡكُم بِهِمَا رَأۡفَةٞ فِي دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ وَلۡيَشۡهَدۡ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, watandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Allah, ikiwa nyinyi mnamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Na kundi la Waumini lishuhudie adhabu yao



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 4

وَٱلَّذِينَ يَرۡمُونَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَأۡتُواْ بِأَرۡبَعَةِ شُهَدَآءَ فَٱجۡلِدُوهُمۡ ثَمَٰنِينَ جَلۡدَةٗ وَلَا تَقۡبَلُواْ لَهُمۡ شَهَٰدَةً أَبَدٗاۚ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na wanao wasingizia wanawake mahashumu (wema), kisha wasilete mashahidi wane, basi watandikeni bakora thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena. Na hao ndio wapotovu



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 5

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Allah ni Msamehevu, Mwenye kurehemu



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 6

وَٱلَّذِينَ يَرۡمُونَ أَزۡوَٰجَهُمۡ وَلَمۡ يَكُن لَّهُمۡ شُهَدَآءُ إِلَّآ أَنفُسُهُمۡ فَشَهَٰدَةُ أَحَدِهِمۡ أَرۡبَعُ شَهَٰدَٰتِۭ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Allah ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 7

وَٱلۡخَٰمِسَةُ أَنَّ لَعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Na mara ya tano kwamba laana ya Allah iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 8

وَيَدۡرَؤُاْ عَنۡهَا ٱلۡعَذَابَ أَن تَشۡهَدَ أَرۡبَعَ شَهَٰدَٰتِۭ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Allah ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 9

وَٱلۡخَٰمِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَآ إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Allah iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli



Capítulo: ASH-SHUURAA 

Verso : 40

وَجَزَـٰٓؤُاْ سَيِّئَةٖ سَيِّئَةٞ مِّثۡلُهَاۖ فَمَنۡ عَفَا وَأَصۡلَحَ فَأَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Allah. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu



Capítulo: ASH-SHUURAA 

Verso : 41

وَلَمَنِ ٱنتَصَرَ بَعۡدَ ظُلۡمِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَا عَلَيۡهِم مِّن سَبِيلٍ

Na wanao jitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu