كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Vipi mnamkufuru Allah, na ilhali mlikuwa wafu akakupeni uhai? Kisha atakufisheni, kisha atakupeni uhai. Na kisha ni kwake tu ndiko mtakakorejeshwa
وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتُۢۚ بَلۡ أَحۡيَآءٞ وَلَٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ
Na msiseme kuwa, waliouawa katika njia ya Allah ni wafu. Bali wapo hai, lakini hamtambui
وَلَكُمۡ فِي ٱلۡقِصَاصِ حَيَوٰةٞ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na mtakuwa na uhai (ulio bora) katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili muogope (msalimike)
تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ
Unauingiza usiku ndani ya mchana[1], na unauingiza mchana ndani ya usiku, na unatoa (kiumbe) hai kutoka katika (kiumbe) mfu, na unatoa (kiumbe) mfu kutoka katika (kiumbe) hai. Na unampa riziki umtakaye bila ya hesabu
1- - Allah anauingiza usiku katika mchana na unakuwa mrefu katika kipindi fulani na pia anauingiza mchana
katika usiku na unakuwa mrefu katika kipindi kingine. Allah anaelezea uweza wake mkubwa unaotoa
kiumbe hai kutoka katika kinachoonekana kama kiumbe mfu, na anatoa kiumbe mfu katika kiumbe hai!
Hapa Allah anelezea uwezo wake mkubwa katika kinachoitwa “Mfuatano na muendelezo wa maisha ya
viumbe hai”.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَقَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ إِذَا ضَرَبُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَوۡ كَانُواْ غُزّٗى لَّوۡ كَانُواْ عِندَنَا مَا مَاتُواْ وَمَا قُتِلُواْ لِيَجۡعَلَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ حَسۡرَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Enyi mlioamini msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kuhusu ndugu zao waliposafiri ardhini au walipokuwa vitani; kama wangekuwa kwetu wasingekufa na wasingeuwawa ili Allah afanye hilo kuwa ni majuto katika nyoyo zao, na Allah anahuisha na anafisha na Allah kwa munayoyatenda ni Mwenye kuyaona mno
وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتَۢاۚ بَلۡ أَحۡيَآءٌ عِندَ رَبِّهِمۡ يُرۡزَقُونَ
Na kamwe msiwadhanie waliouliwa katika njia ya Allah kuwa ni wafu, bali wako hai kwa Mola wao wanaruzukiwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَٰرَةً عَن تَرَاضٖ مِّنكُمۡۚ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمٗا
Enyi mlioamini, msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa tu kama mali hizo ni biashara (inayofanyika) kwa maridhiano yenu. Na msijiue. Hakika, Allah ni mwenye rehema kwenu
مِنۡ أَجۡلِ ذَٰلِكَ كَتَبۡنَا عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ أَنَّهُۥ مَن قَتَلَ نَفۡسَۢا بِغَيۡرِ نَفۡسٍ أَوۡ فَسَادٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ ٱلنَّاسَ جَمِيعٗا وَمَنۡ أَحۡيَاهَا فَكَأَنَّمَآ أَحۡيَا ٱلنَّاسَ جَمِيعٗاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم بَعۡدَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡأَرۡضِ لَمُسۡرِفُونَ
Kwa sababu ya hayo[1], tume-waandikia (tumewafaradhishia) Wana wa Israil ya kwamba, aliyeua nafsi (ya mtu) bila ya (yeye kuua) nafsi au kufanya uovu katika nchi, basi ni kama ameua watu wote. Na mwenye kuihuisha (kuiokoa nafsi isife) ni kama ameokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja za wazi, kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wakawa wenye kufanya yaliyovuka mipaka katika ardhi
1- - Kosa la mauaji yaliyofanywa na mmoja wa watoto wa Mtume Adamu.
وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ
Na msile (nyama ya mnyama) ambaye halikutajwa jina la Allah juu yake (wakati wa kuchinjwa), na hakika hilo (la kula nyama ya mnyama ambaye hakuchinjwa kwa taratibu za Kiislamu) ni uasi. Na hakika, mashetani wanatia ushawishi kwa marafiki zao (wa kibinadamu) ili wajadiliane nanyi (katika ulaji wa nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu). Na kama mkiwatii (katika kuhalalisha nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu) kwa hakika kabisa nyinyi ni washirikina (makafiri)
۞قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Sema: Njooni nisome yale Mola wenu aliyokuharamishieni (nayo ni) msikishirikishenaye kitu chochote na wazazi wawili wafanyieni yaliyo mazuri na msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara (umasikini kwa sababu) sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Na msiyakaribie mambo machafu yaliyo dhihiri kati ya hayo na yaliyo ya siri. Na msiiue nafsi ambayo Allah ameharamisha (kuiua) ila kwa haki tu. Hayo amekuusieni (Allah) ili myatie akilini
هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Yeye (Allah) anahuisha na anafisha, na kwake tu mtarejeshwa
وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ
Na kwa hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi (wa viumbe na huu ulimwengu)
وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ خَشۡيَةَ إِمۡلَٰقٖۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُهُمۡ وَإِيَّاكُمۡۚ إِنَّ قَتۡلَهُمۡ كَانَ خِطۡـٔٗا كَبِيرٗا
Wala msiwauwe watoto wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni hatia (kosa) kubwa sana
وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَمَن قُتِلَ مَظۡلُومٗا فَقَدۡ جَعَلۡنَا لِوَلِيِّهِۦ سُلۡطَٰنٗا فَلَا يُسۡرِف فِّي ٱلۡقَتۡلِۖ إِنَّهُۥ كَانَ مَنصُورٗا
Wala msiuwe nafsi ambayo Allah amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa
أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ كَانَتَا رَتۡقٗا فَفَتَقۡنَٰهُمَاۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَيۡءٍ حَيٍّۚ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ
Je! Hao walio kufuru hawa-kuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabadua? Na tukajaalia kutokana na maji kila kitu chenye uhai? Basi je, hawaamini?
وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَحۡيَاكُمۡ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡۗ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَكَفُورٞ
Na Yeye ndiye aliye kuhuisheni kisha akakufisheni, na kisha atakufufueni. Hakika mwanaadamu hana fadhila
وَهُوَ ٱلَّذِي يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَلَهُ ٱخۡتِلَٰفُ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na ni yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu?
يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَيُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۚ وَكَذَٰلِكَ تُخۡرَجُونَ
Hukitoa kilicho hai kutokana na kilicho kufa, na hukitoa kilicho kufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyo fufuliwa
إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيۡنَا ٱلۡمَصِيرُ
Hakika sisi ndiyo tunaohuisha na tunafisha na kwetu sisi tu ndiyo marejeo
لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na yeye Muweza wa kila kitu
ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ
Ambaye ameumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye kutenda (vitendo) vizuri zaidi? Na yeye (Allah) ndiye hasa Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kusamehe sana