وَإِذۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ لَمَآ ءَاتَيۡتُكُم مِّن كِتَٰبٖ وَحِكۡمَةٖ ثُمَّ جَآءَكُمۡ رَسُولٞ مُّصَدِّقٞ لِّمَا مَعَكُمۡ لَتُؤۡمِنُنَّ بِهِۦ وَلَتَنصُرُنَّهُۥۚ قَالَ ءَأَقۡرَرۡتُمۡ وَأَخَذۡتُمۡ عَلَىٰ ذَٰلِكُمۡ إِصۡرِيۖ قَالُوٓاْ أَقۡرَرۡنَاۚ قَالَ فَٱشۡهَدُواْ وَأَنَا۠ مَعَكُم مِّنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Na (kumbuka) Allah alipochukua ahadi ya Manabii ya kuwa kitabu chochote na hekima yoyote niliyokupeni kisha akakujieni Mtume anayesadikisha kile mlichonacho kwamba kwa yakini kabisa mtamkubali na kumnusuru. (Allah) Akasema: Je, mmekubalina mmechukua ahadi yangu juu ya hilo? Wakasema: Tumeikubali. (Allah) Akasema: Shuhudieni kwamba, na mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kushuhudia
فَمَن تَوَلَّىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ
Basi watakaokengeuka baada ya (makubaliano) hayo basi hao ni waovu tu
۞وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na yeyote anayehama katika njia ya Allah atapata faida nyingi ardhini na ukunjufu. Na yeyote anayetoka nyumbani kwake akahama kwa ajili ya Allah na Mtume wake, kisha kifo kikamfika, hakika ujira wake umeshathibiti kwa Allah. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Enyi mlioamini, endeleeni kumuaminini Allah na Mtume wake na kitabu (Qur’ani) alichokiteremsha kwa Mtume wake na vitabu alivyoviteremsha kabla yake (kabla ya Qur’ani). Na yeyote anayempinga Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu wa mbali kabisa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Enyi watu, hakika amekujieni Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, iwe kheri kwenu. Na mkikufuru basi hakika ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allah ni Mjuzi sana, Mwenye hekima
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ وَلَا تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلۡقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرۡيَمَ وَرُوحٞ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُواْ ثَلَٰثَةٌۚ ٱنتَهُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٞۘ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا
Enyi Watu wa Kitabu, msichupe mipaka katika dini yenu na msimsemee Allah isipokuwa haki tu. Hakika, ilivyo ni kwamba Masihi, Issa Mwana wa Mariamu ni Mtume wa Allah na neno lake alilompelekea Mariamu, na ni roho iliyotoka kwake. Basi muaminini Allah na Mitume wake, na msiseme: Miungu ni watatu. Acheni (kuamini hivyo) itakuwa kheri kwenu. Hakika, ilivyo ni kwamba, Allah ni Mungu mmoja tu, ametakasika (kwa) kutokuwa na mwana. Ni vyake yeye tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na imetosha kwamba, Allah ni Mwenye kutegemewa
ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلرَّسُولَ ٱلنَّبِيَّ ٱلۡأُمِّيَّ ٱلَّذِي يَجِدُونَهُۥ مَكۡتُوبًا عِندَهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ يَأۡمُرُهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَىٰهُمۡ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡخَبَـٰٓئِثَ وَيَضَعُ عَنۡهُمۡ إِصۡرَهُمۡ وَٱلۡأَغۡلَٰلَ ٱلَّتِي كَانَتۡ عَلَيۡهِمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِهِۦ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَٱتَّبَعُواْ ٱلنُّورَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ مَعَهُۥٓ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Ambao wanamfuata Mtume, Nabii, hasomi kilichoandikwa, ambaye kwao wanamkuta amean-dikwa katika Taurati na Injili, anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vilivyo vizuri, na anawaharamishia vilivyo vibaya, na anawaondoshea mazito yao (sheria zao ngumu) na makongwa (minyororo ya dhambi) waliyokuwa nayo. Basi wale waliomuamini (Mtume huyo) na wakamheshimu na wakamsaidia na wakaifuata nuru aliyoteremshiwa, hao tu ndio waliofanikiwa
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Sema: Enyi watu, hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyote[1]. (Allah) Ambaye ni wake pekee ufalme wa mbinguni na ardhini. Hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu. Anahuisha na anafisha. Basi muaminini Allah na Mtume wake, Nabii ambaye hasomi kilichoandikwa, ambaye anamuamini Allah na maneno yake, na mfuateni ili mpate kuongoka
1- - Aya hii ni tangazo rasmi kwamba, Uislamu ni dini ya ulimwengu wote na sio ya taifa fulani, kabila fulani au jamii fulani.
وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ سَيَرۡحَمُهُمُ ٱللَّهُۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki (wa kusaidiana na kuungana mkono katika kheri) wao kwa wao. Wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha Swala na wanatoa Zaka na wanamtii Allah na Mtume wake. Hao Allah atawashushia rehema. Hakika, Allah ni Mwenye nguvu mno, Mwenye hekima sana
ٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ أَوۡ لَا تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ إِن تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ سَبۡعِينَ مَرَّةٗ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Waombee msamaha au usiwaombee (yote ni sawa). Hata ukiwaombea msamaha mara sabini (au zaidi), katu Allah hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu wamemkufuru Allah na Mtume wake. Na Allah hawaongoi watu waovu
إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَإِذَا كَانُواْ مَعَهُۥ عَلَىٰٓ أَمۡرٖ جَامِعٖ لَّمۡ يَذۡهَبُواْ حَتَّىٰ يَسۡتَـٔۡذِنُوهُۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ فَإِذَا ٱسۡتَـٔۡذَنُوكَ لِبَعۡضِ شَأۡنِهِمۡ فَأۡذَن لِّمَن شِئۡتَ مِنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمُ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakika Waumini wa kweli ni walio muamini Allah na Mtume wake; na wanapo kuwa pamoja naye kwa jambo la kuwahusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa. Kwa hakika wale wanao kuomba ruhusa, hao ndio wanao muamini Allah na Mtume wake. Na wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya kazi zao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa Allah. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemmu
وَلَمَّا رَءَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ قَالُواْ هَٰذَا مَا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَصَدَقَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥۚ وَمَا زَادَهُمۡ إِلَّآ إِيمَٰنٗا وَتَسۡلِيمٗا
Na Waumini walipoyaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Allah na Mtume wake. Na Allah na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut’iifu
يَٰقَوۡمَنَآ أَجِيبُواْ دَاعِيَ ٱللَّهِ وَءَامِنُواْ بِهِۦ يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُجِرۡكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ
Enyi watu wetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Allah, na muaminini, Allah atakusameheni, na atakukingeni na adhabu chungu
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٖ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡ كَفَّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ
Na wale walioamini na wakatenda mema, na wakayaamini yaliyoteremshwa kwa Muhammad, nayo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi, (Allah) amewafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao
وَمَن لَّمۡ يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ فَإِنَّآ أَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ سَعِيرٗا
Na asiye muamini Allah na Mtume wake, basi kwa hakika Sisi tumewaandalia makafiri Moto mkali
إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ لَمۡ يَرۡتَابُواْ وَجَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ
Hakika waumini ni wale tu waliomuamini Allah na mtume wake kisha hawakuogopa, na wakapigana kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allah hao ndio wenye kusadikisha
ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَأَنفِقُواْ مِمَّا جَعَلَكُم مُّسۡتَخۡلَفِينَ فِيهِۖ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَأَنفَقُواْ لَهُمۡ أَجۡرٞ كَبِيرٞ
Muaminini Allah na Mtume Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa ni waangalizi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, watapata ujira mkubwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَءَامِنُواْ بِرَسُولِهِۦ يُؤۡتِكُمۡ كِفۡلَيۡنِ مِن رَّحۡمَتِهِۦ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ نُورٗا تَمۡشُونَ بِهِۦ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Enyi walioamini! Mcheni Allah, na muaminini Mtume Wake. (Allah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakusameheni; na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu
لَّا تَجِدُ قَوۡمٗا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ يُوَآدُّونَ مَنۡ حَآدَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَوۡ كَانُوٓاْ ءَابَآءَهُمۡ أَوۡ أَبۡنَآءَهُمۡ أَوۡ إِخۡوَٰنَهُمۡ أَوۡ عَشِيرَتَهُمۡۚ أُوْلَـٰٓئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡإِيمَٰنَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٖ مِّنۡهُۖ وَيُدۡخِلُهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ رَضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُۚ أُوْلَـٰٓئِكَ حِزۡبُ ٱللَّهِۚ أَلَآ إِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Hutokuta watu wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allah) Ameandika katika nyoyo zao Imani, na Akawatia nguvu kwa Roho (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza kwenye Mabustani yapitayo chini yake mito humo watakaa milele. Allah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allah. Zindukeni! Hakika kundi la Allah ndio lenye kufaulu
تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Muaminini Allah na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Allah kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua
فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Basi muaminini Allah na Mtume Wake na Nuru (Qurani) Tuliyoiteremsha, na Allah anazo khabari za mnayo yatenda
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ
Kwa hakika hii (Qur’ani) ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye heshima