قُلۡ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Sema: Mtiini Allah na Mtume. Kama mkikengeuka, basi kwa hakika Allah hawapendi makafiri
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na mtiini Allah na Mtume ili mpate kupewa rehema
تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Hiyo ndiyo mipaka ya Allah na yeyote mwenye kumtii Allah na Mtume wake atamuingiza katika Pepo itiririkayo mito chini yake, watabaki humo milele na huko ndiko kufaulu kuliko kukubwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَأُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنكُمۡۖ فَإِن تَنَٰزَعۡتُمۡ فِي شَيۡءٖ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلًا
Enyi mlioamini, mtiini Allah na mtiini Mtume, na wenye mamlaka katika nyinyi. Basi iwapo mtavutana[1] katika jambo lolote, lirudisheni kwa Allah na (kwa) Mtume, ikiwa mnamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Hilo ni bora zaidi na ni mwisho mzuri sana
1- - Kuvutana ni kubishana kuhusu jambo fulani kati ya pande mbili au zaidi na kila upande huvutia kwake.
وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّـٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَـٰٓئِكَ رَفِيقٗا
Na wenye kumtii Allah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allah amewaneemesha ikiwa ni pamoja na Manabii na Wenye kusadikisha (Maswahaba) na Mashahidi na Watu Wema.[1] Na ni uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!
1- - Aya hapa inawabainisha walioneemeshwa na ambao katika Aya ya 6 na ya 7 ya Sura Alfaatiha (1) Waislamu wametakiwa kuwaiga na kufuata njia, muongozo na sera zao. Swahaba, wakiongozwa na Abubakar, Umar, Uthman na Ali (Allah awawie radhi) wanahusika katika Aya hii kwa sababu kuna Hadithi kadhaa za Mtume (Allah amshushie rehema na amani, zinazowataja kuwa wamo Mashahidi na Wasadikishaji.
مَّن يُطِعِ ٱلرَّسُولَ فَقَدۡ أَطَاعَ ٱللَّهَۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظٗا
Yeyote anayemtii Mtume basi hakika (atakuwa) amemtii Allah, na yeyote atakaye kengeuka basi (ni juu yake, kwa sababu) hatukukupeleka kwao uwe mtunzaji (wa matendo yao)
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَٱحۡذَرُواْۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na mtiini Allah na mtiini Mtume, na jihadharini (na dhambi). Na mkikengeuka basi jueni ya kuwa jukumu la Mtume wetu ni kufikisha ujumbe wenye kufafanua
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَنفَالِۖ قُلِ ٱلۡأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَصۡلِحُواْ ذَاتَ بَيۡنِكُمۡۖ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
(Ewe Nabii) Wanakuuliza kuhusu (utaratibu wa ugawaji wa) Ngawira. Sema: Ngawira ni za Allah na Mtume (wao ndio watoaji wa utaratibu wa mgao wake). Basi mcheni Allah (kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake) na tatueni migogoro baina yenu, na mtiini Allah na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَأَنتُمۡ تَسۡمَعُونَ
Enyi mlioamini, mtiini Allah na Mtume wake (kwa wanayo kuamrisheni au kukukatazeni), na msiigeuke (msiipinge) amri hiyo (ya kumtii Allah na Mtume wake) na ilhali mnasikia (wanayokuambieni)
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُواْ فَتَفۡشَلُواْ وَتَذۡهَبَ رِيحُكُمۡۖ وَٱصۡبِرُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Na mtiini Allah na Mtume wake, wala msizozane mtasambaratika (na woga utakutawaleni) na nguvu zenu zitatoweka. Na vumilieni. Hakika Allah yupo pamoja na wavumilivu
وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ سَيَرۡحَمُهُمُ ٱللَّهُۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki (wa kusaidiana na kuungana mkono katika kheri) wao kwa wao. Wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha Swala na wanatoa Zaka na wanamtii Allah na Mtume wake. Hao Allah atawashushia rehema. Hakika, Allah ni Mwenye nguvu mno, Mwenye hekima sana
إِنَّمَا كَانَ قَوۡلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ أَن يَقُولُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۚ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Allah na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumetii! Na hao ndio wenye kufanikiwa
وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخۡشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقۡهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ
Na wenye kumtii Allah na Mtume wake, na wakamwogopa Allah na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu
قُلۡ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيۡكُم مَّا حُمِّلۡتُمۡۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهۡتَدُواْۚ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Sema: Mtiini Allah, na mtiini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni aliyo bebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyo bebeshwa nyinyi. Na mkimtii yeye mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi
وَقَرۡنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجۡنَ تَبَرُّجَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ ٱلۡأُولَىٰۖ وَأَقِمۡنَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتِينَ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِعۡنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُذۡهِبَ عَنكُمُ ٱلرِّجۡسَ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِ وَيُطَهِّرَكُمۡ تَطۡهِيرٗا
Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt’iini Allah na Mtume wake. Hakika Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni barabara
يُصۡلِحۡ لَكُمۡ أَعۡمَٰلَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدۡ فَازَ فَوۡزًا عَظِيمًا
Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt’ii Allah na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa
۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبۡطِلُوٓاْ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Enyi mlio amini! Mtiini Allah, na mtiini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu
لَّيۡسَ عَلَى ٱلۡأَعۡمَىٰ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡأَعۡرَجِ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرِيضِ حَرَجٞۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبۡهُ عَذَابًا أَلِيمٗا
Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumtii Allah na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Na atakaye geuka upande atamuadhibu kwa adhabu chungu
۞قَالَتِ ٱلۡأَعۡرَابُ ءَامَنَّاۖ قُل لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ وَلَٰكِن قُولُوٓاْ أَسۡلَمۡنَا وَلَمَّا يَدۡخُلِ ٱلۡإِيمَٰنُ فِي قُلُوبِكُمۡۖ وَإِن تُطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَا يَلِتۡكُم مِّنۡ أَعۡمَٰلِكُمۡ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Walisema warabu tumeamini, sema hamjaamini lakini sema tumesilimu na bado haijaingia imani kwenye nyoyo zenu, na endapo mtamtii Allah na mtume wake hatowapunguzia kwenye malipo yenu chochote hakika Allah ni mwingi wakusamehe mwingi wa rehema
ءَأَشۡفَقۡتُمۡ أَن تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَٰتٖۚ فَإِذۡ لَمۡ تَفۡعَلُواْ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ
Je, mnakhofu kutanguliza hiyo swadaka kabla ya kusemezana kwenu? Ikiwa hamjafanya hayo, na Allah Akapokea toba yenu; basi simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Allah na Mtume Wake; na Allah ni Mwenye khabari kwa yale myatendayo
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na mtiini Allah, na mt’iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ وَٱسۡمَعُواْ وَأَطِيعُواْ وَأَنفِقُواْ خَيۡرٗا لِّأَنفُسِكُمۡۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Basi mcheni Allah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allah) itakuwa kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili (tamaa ya uchu wa nafsi yake), basi hao ndio wenye kufaulu (kufanikiwa)