يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَرُدُّوكُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ كَٰفِرِينَ
Enyi ambao mmeamini, kama mtalitii kundi katika wale waliopewa Kitabu watakurudisheni muwe makafiri baada ya kuamini kwenu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَرُدُّوكُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَٰبِكُمۡ فَتَنقَلِبُواْ خَٰسِرِينَ
Enyi mlioamini, ikiwa mtawatii wale waliokufuru[1] watakurudisheni nyuma, na mtageuka kuwa wenye hasara
1- - Utii unaokatazwa hapa ni ule unaohusu masuala ya kuabudu na kupinga sheria za Allah na sio masuala ya maendeleo ya mazingira ya dunia.
وَإِن تُطِعۡ أَكۡثَرَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ
Na ikiwa utawatii walio wengi humu duniani watakupoteza katika njia ya Allah[1]. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa wao isipokuwa tu wanaongopa
1- - Usemi wa Kiswahili wa “Wengi wape” katika Uislamu hauna nafasi. Kinachotakiwa katika Uislamu ni haki na uadilifu. Haki haipimwi kwa wingi au uchache.
وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ
Na msile (nyama ya mnyama) ambaye halikutajwa jina la Allah juu yake (wakati wa kuchinjwa), na hakika hilo (la kula nyama ya mnyama ambaye hakuchinjwa kwa taratibu za Kiislamu) ni uasi. Na hakika, mashetani wanatia ushawishi kwa marafiki zao (wa kibinadamu) ili wajadiliane nanyi (katika ulaji wa nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu). Na kama mkiwatii (katika kuhalalisha nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu) kwa hakika kabisa nyinyi ni washirikina (makafiri)
وَٱصۡبِرۡ نَفۡسَكَ مَعَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ وَلَا تَعۡدُ عَيۡنَاكَ عَنۡهُمۡ تُرِيدُ زِينَةَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَا تُطِعۡ مَنۡ أَغۡفَلۡنَا قَلۡبَهُۥ عَن ذِكۡرِنَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ وَكَانَ أَمۡرُهُۥ فُرُطٗا
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi zake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimtii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka
فَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَجَٰهِدۡهُم بِهِۦ جِهَادٗا كَبِيرٗا
Basi usiwat’ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa
وَوَصَّيۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ بِوَٰلِدَيۡهِ حُسۡنٗاۖ وَإِن جَٰهَدَاكَ لِتُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَآۚ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watakushikilia unishirikishe Mimi na usiyo kuwa na ujuzi nayo, basi usiwat’ii. Kwangu Mimi ndio marejeo yenu, na nitakwambieni mliyokuwa mkiyatenda
وَإِن جَٰهَدَاكَ عَلَىٰٓ أَن تُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَاۖ وَصَاحِبۡهُمَا فِي ٱلدُّنۡيَا مَعۡرُوفٗاۖ وَٱتَّبِعۡ سَبِيلَ مَنۡ أَنَابَ إِلَيَّۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda
يَوۡمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمۡ فِي ٱلنَّارِ يَقُولُونَ يَٰلَيۡتَنَآ أَطَعۡنَا ٱللَّهَ وَأَطَعۡنَا ٱلرَّسُولَا۠
Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt’ii Allah, na tungeli mt’ii Mtume!
وَقَالُواْ رَبَّنَآ إِنَّآ أَطَعۡنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَآءَنَا فَأَضَلُّونَا ٱلسَّبِيلَا۠
Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat’ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia
فَٱسۡتَخَفَّ قَوۡمَهُۥ فَأَطَاعُوهُۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ
Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu
فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ
Basi usiwatii wanao kadhibisha
وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ
Wala usimtii kila mwapaji sana, aliye dhalili,
فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعۡ مِنۡهُمۡ ءَاثِمًا أَوۡ كَفُورٗا
Basi ngojea hukumu ya Mola wako wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kukufuru
كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩
Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!