Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 3

ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Ambao wanaamini Ghaibu na wanasimamisha swala na baadhi ya tulivyowapa wanatoa



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 43

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wanaorukuu



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 45

وَٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلۡخَٰشِعِينَ

Na ombeni msaada kwa kusubiri na kuswali. Na kwa hakika kabisa, hiyo Swala ni nzito mno isipokuwa kwa wanyenyekevu tu



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 110

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka, na heri yoyote muitanguliziayo kwa ajili yenu mtaikuta mbele ya Allah. Hakika, Allah anayaona mno mnayoyatenda



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 153

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Enyi mlioamini, ombeni msaada kwa uvumilivu (subra) na kuswali. Bila shaka, Allah yupo pamoja na wenye uvumilivu



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 238

حَٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوَٰتِ وَٱلصَّلَوٰةِ ٱلۡوُسۡطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَٰنِتِينَ

Zichungeni swala zote (tano) na (ichungeni) swala ya kati. Na simameni kwa ajili ya Allah mkiwa wanyenyekevu



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 101

وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا

Na mnaposafiri ardhini[1], basi hakuna ubaya wowote kwenu kupunguza Swala[2] ikiwa mtahofia kupata mitihani ya makafiri (kwa kukudhuruni). Hakika makafiri wamekuwa maadui wa dhahiri kwenu


1- - Hapa imetajwa kusafiri ardhini kwa sababu sehemu kubwa ya usafiri kwa wakati Qur’ani inashuka ilikuwa kwa njia ya ardhini na majini. Ama ruhusa hii inahusu pia usafiri wa anga abao umeshamiri hivi sasa.


2- - Swala zinazokusudiwa kupunguzwa hapa ni zile zenye rakaa nne. Zinapunguzwa na kuswaliwa rakaa mbili. Swala hizo ni Adhuhuri, Alasiri na Isha.


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 102

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمۡ فَأَقَمۡتَ لَهُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَلۡتَقُمۡ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُم مَّعَكَ وَلۡيَأۡخُذُوٓاْ أَسۡلِحَتَهُمۡۖ فَإِذَا سَجَدُواْ فَلۡيَكُونُواْ مِن وَرَآئِكُمۡ وَلۡتَأۡتِ طَآئِفَةٌ أُخۡرَىٰ لَمۡ يُصَلُّواْ فَلۡيُصَلُّواْ مَعَكَ وَلۡيَأۡخُذُواْ حِذۡرَهُمۡ وَأَسۡلِحَتَهُمۡۗ وَدَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ تَغۡفُلُونَ عَنۡ أَسۡلِحَتِكُمۡ وَأَمۡتِعَتِكُمۡ فَيَمِيلُونَ عَلَيۡكُم مَّيۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن كَانَ بِكُمۡ أَذٗى مِّن مَّطَرٍ أَوۡ كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَن تَضَعُوٓاْ أَسۡلِحَتَكُمۡۖ وَخُذُواْ حِذۡرَكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ أَعَدَّ لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Na unapokuwa nao ukawa-simamishia Swala, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na washike silaha zao. Wanaposujudu, (walioshika silaha) wawe nyuma yenu. Na (likimaliza kundi hili) lije kundi jingine ambalo halijaswali liswali pamoja na wewe na wachukue tahadhari zao na silaha zao. Waliokufuru wanapenda lau mngesahau silaha zenu na mizigo yenu ili wakushukieni (wakushambulieni kwa) shambulio moja tu (na kukumalizeni). Na hakuna ubaya wowote kwenu, kama mtakuwa katika hali ya udhia utokanao na mvua au mkiwa wagonjwa kutochukua silaha zenu. Na chukueni tahadhari zenu. Hakika Allah amewaandalia makafiri adhabu yenye kudhalilisha



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 103

فَإِذَا قَضَيۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمۡۚ فَإِذَا ٱطۡمَأۡنَنتُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا

Mmalizapo kuswali basi mtajeni Allah mkiwa mmesimama na mkiwa mmekaa na mkiwa mmejilaza ubavu. Mnapokuwa katika utulivu (amani), basi simamisheni Swala (kwa ukamilifu na bila ya kupunguza). Kwa hakika, Swala kwa Waislamu ni jambo liliofaradhishwa, lililowekewa wakati maaulumu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قُمۡتُمۡ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغۡسِلُواْ وُجُوهَكُمۡ وَأَيۡدِيَكُمۡ إِلَى ٱلۡمَرَافِقِ وَٱمۡسَحُواْ بِرُءُوسِكُمۡ وَأَرۡجُلَكُمۡ إِلَى ٱلۡكَعۡبَيۡنِۚ وَإِن كُنتُمۡ جُنُبٗا فَٱطَّهَّرُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُم مِّنۡهُۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجۡعَلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ حَرَجٖ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمۡ وَلِيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Enyi mlioamini, mnaposimama kwenda kuswali[1], basi (tawadheni) osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka viwikoni na pakeni (maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni[2]. Na mkiwa wenye Janaba basi jitwaharisheni (kwa kuoga au kutayamamu ikishindikana kuoga). Na mkiwa wagonjwa au mpo safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmegusana (mmejamiiana) na wanawake (wake zenu)[3] na hamkupata maji, basi tayamamuni (kusudieni) mchanga ulio safi[4] na mpake nyuso zenu na mikono yenu kwa mchanga huo[5]. Allah hataki kukuwekeeni tabu yoyote (uzito na usumbufu kwa kulazimisha kujitwaharisha kwa maji wakati maji hayapo au haiwezekani kuyatumia kwasababu ya ugonjwa au baridi kali); bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake kwenu ili mpate kushukuru.[6]


1- - Hii ina maana hata kwa anayeswali kwa kuketi au kwa kulala ujumbe na utaratibu huu unamhusu pia.


2- - Kwenye Aya hii kuna visomo vikuu viwili vinavyokubalika: “Arjulakum” kwa Nasbu. Na kisomo cha pili ni “Arjulikum” kwa Jarri. Hii inamaanisha kwamba, kwa mujibu wa Qur’an na Suna sahihi za Mtume wa Allah uoshaji wa miguu una hukumu za aina mbili: (a) Kama miguu ikiwa wazi (haijavikwa kitu) faradhi yake ni kuoshwa kwa maji. (b) Kama miguu imevikwa khofu/soksi faradhi yake ni kupakwa maji.


3- - Muradi wa kugusana hapa ni kujamiiana. Kugusana tu kwa Ngozi na Ngozi hakulazimishi kutawadha.


4- - Kitendo hiki cha kutumia mchanga ulio safi na kupaka vumbi lake usoni na mikononi kinaitwa Tayamamu katika sheria ya Kiislamu.


5- - Kwa pigo la kwanza pakeni usoni na kwa pigo la pili pakeni mikononi.


6- - Aya hapa inaonesha kuwa ni lazima Muislamu kila anapotaka kuswali atawadhe. Lakini ulazima huu ni kwa yule ambaye hana Udhu. Ama mtu mwenye Udhu halazimiki kutawadha, lakini ni jambo zuri kama
atatawadha tena.


Capítulo: AL-AN’AAM 

Verso : 72

وَأَنۡ أَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّقُوهُۚ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Na (tumeamrishwa kwamba): Simamisheni Swala, na mumche yeye (Allah), na yeye ndiye ambaye kwake tu ndiko mtakapokusanywa



Capítulo: AL-AN’AAM 

Verso : 92

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَاۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, kilochobarikiwa, kinachosadikisha (kitabu) kilichoko mbele yake na (tumekiteremsha) ili uwaonye (kwacho watu wa mji wa) Mama wa Miji (Makkah) na walioko (katika miji iliyopo) pembezoni mwake[1]. Na wale wanaoamini Akhera (kuwa ipo) wanakiamini kitabu hicho, nao wanadumisha Swala zao


1- - Kinachokusudiwa hapa ni maeneo mengine ya dunia. Qur’ani imeteremka kwa ajili ya watu wote duniani. Rejea Aya ya 41 ya sura Azzumar (39). Pia rejea Aya ya 51-52 ya Sura Alqalam (68).


Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 170

وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Na ambao wanakishika vilivyo kitabu (bila ya kukipuuza au kukifanyia mzaha) na wakadumisha Swala, hakika sisi hatupotezi ujira wa watengenezao (mambo ya kumridhisha Allah)



Capítulo: AN-FAL 

Verso : 3

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

(Waumini) Ambao wanasi-mamisha Swala (wanadumu katika kuswali kwa kukidhi vigezo na masharti ya Swala) na katika vile tulivyowaruzuku wanavitoa (katika njia za heri)



Capítulo: AN-FAL 

Verso : 35

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمۡ عِندَ ٱلۡبَيۡتِ إِلَّا مُكَآءٗ وَتَصۡدِيَةٗۚ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Na haikuwa (Swala) ibada yao kwenye Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miruzi na makofi tu. Basi (enyi Washirikina) onjeni adhabu (ya duniani kwa kupigwa kwenye vita vya Badri) (na adhabu ya huko Akhera inawangojeni) kwa vile mlivyokuwa mnakufuru



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 5

فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلۡأَشۡهُرُ ٱلۡحُرُمُ فَٱقۡتُلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡ وَخُذُوهُمۡ وَٱحۡصُرُوهُمۡ وَٱقۡعُدُواْ لَهُمۡ كُلَّ مَرۡصَدٖۚ فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّواْ سَبِيلَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Basi inapokwisha Miezi (minne) Mitukufu (ambayo mliwapa amani makafiri) basi (tengueni ahadi na) waueni washirikina popote mnapowakuta, na washikeni (watieni mbaroni) na wazingireni, na wakalieni (wadhibitini) katika kila njia (kila kona). Basi iwapo watatubu (wataacha ukafiri) nawakasimamisha Swala na wakatoa Zaka, basi waachieni (kwakuwa wameshakuwa ndugu zenu katika imani). Hakika Allah ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 11

فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِۗ وَنُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Basi (Makafiri) wakitubu (wakiacha ukafiri na kuingia katika Uislamu) na wakasimamisha Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazifafanua Aya kwa watu wanaojua



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 18

إِنَّمَا يَعۡمُرُ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمۡ يَخۡشَ إِلَّا ٱللَّهَۖ فَعَسَىٰٓ أُوْلَـٰٓئِكَ أَن يَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ

Hakika ilivyo ni kwamba, wanaoamirisha misikiti ya Allah ni wale wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na wakasimamisha Swala na wakatoa Zaka na wala hawamuogopi (yeyote) ila Allah tu. Basi huwenda hao wakawa miongoni mwa walioongoka



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 71

وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ سَيَرۡحَمُهُمُ ٱللَّهُۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki (wa kusaidiana na kuungana mkono katika kheri) wao kwa wao. Wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha Swala na wanatoa Zaka na wanamtii Allah na Mtume wake. Hao Allah atawashushia rehema. Hakika, Allah ni Mwenye nguvu mno, Mwenye hekima sana



Capítulo: YUNUS 

Verso : 87

وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّءَا لِقَوۡمِكُمَا بِمِصۡرَ بُيُوتٗا وَٱجۡعَلُواْ بُيُوتَكُمۡ قِبۡلَةٗ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na tulimpa Wahyi Musa na ndugu yake (Haruna) ya kuwa: Wawekeeni makazi (wajengeeni nyumba) watu wenu (katika mji wa) Misri na zifanyeni nyumba zenu ziwe na mahala pa ibada na simamisheni Swala na wape bishara Waumini



Capítulo: HUUD 

Verso : 114

وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّـٰكِرِينَ

Na simamisha swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huo ni ukumbusho kwa wale wanaokumbuka



Capítulo: AR-RA’D 

Verso : 22

وَٱلَّذِينَ صَبَرُواْ ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِمۡ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

Na ambao husubiri kwa kutaka radhi za Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika tulivyowaruzuku kwa siri na kwa uwazi, na wakayaondoa maovu kwa mema. Hao ndio watakaopata malipo ya nyumba ya Akhera



Capítulo: IBRAHIM 

Verso : 31

قُل لِّعِبَادِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خِلَٰلٌ

Waambie waja wangu walioa-mini, wasimamishe Swala, na watoe katika tulivyowaruzuku, kwa siri na dhahiri, kabla haijafika Siku isiyofaa kitu fidia wala urafiki



Capítulo: IBRAHIM 

Verso : 37

رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ

Mola wetu Mlezi, hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu (Ismaili na mama yake) kwenye bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili wasimamishe Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku kila aina ya matunda, ili wapate kushukuru



Capítulo: IBRAHIM 

Verso : 40

رَبِّ ٱجۡعَلۡنِي مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِيۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلۡ دُعَآءِ

(Ewe) Mola wangu Mlezi, nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swala, na katika watoto dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu



Capítulo: AL-ISRAA 

Verso : 78

أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمۡسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيۡلِ وَقُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِۖ إِنَّ قُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِ كَانَ مَشۡهُودٗا

Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur’ani ya alfajiri. Hakika Qur’ani ya alfajiri inashuhudiwa daima



Capítulo: AL-ISRAA 

Verso : 110

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱللَّهَ أَوِ ٱدۡعُواْ ٱلرَّحۡمَٰنَۖ أَيّٗا مَّا تَدۡعُواْ فَلَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَلَا تَجۡهَرۡ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتۡ بِهَا وَٱبۡتَغِ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلٗا

Sema: Mwombeni Allah (Allah), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usidhihirishe Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati (baina ya hizo)



Capítulo: MARYAM 

Verso : 31

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيۡنَ مَا كُنتُ وَأَوۡصَٰنِي بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ مَا دُمۡتُ حَيّٗا

Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu nipo hai



Capítulo: MARYAM 

Verso : 55

وَكَانَ يَأۡمُرُ أَهۡلَهُۥ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِۦ مَرۡضِيّٗا

Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa ni mwenye kuridhiwa mbele ya Mola wake Mlezi



Capítulo: MARYAM 

Verso : 59

۞فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٌ أَضَاعُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّبَعُواْ ٱلشَّهَوَٰتِۖ فَسَوۡفَ يَلۡقَوۡنَ غَيًّا

Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya