Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 34

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na (kumbuka) tulipowaambia Malaika (kuwa): Msujudieni Adamu. Wakasujudu, isipokuwa Ibilisi alikataa na kuleta kiburi na akawa miongoni mwa makafiri



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 36

فَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ عَنۡهَا فَأَخۡرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِۖ وَقُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ

Shetani akawatelezesha kwenye Pepo hiyo, hivyo akawatoa katika hali waliyokuwa nayo. Na tukasema: Teremkeni. Nyinyi kwa nyinyi mtakuwa maadui. Na mtakuwa na makazi na starehe ardhini mpaka muda maalumu



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 168

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٌ

Enyi watu, kuleni vilivyomo katika ardhi vikiwa halali na vizuri. Na msifuate nyendo za shetani kwa sababu, bila ya shaka, yeye kwenu ni adui aliye wazi



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 169

إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ وَٱلۡفَحۡشَآءِ وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Yeye anakuamrisheni mambo mabaya na machafu tu na …kumsingizia Allah msiyoyajua



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 208

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِي ٱلسِّلۡمِ كَآفَّةٗ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Enyi mlioamini, ingieni kwenye Uislamu wote (wazima wazima), na msifuate nyayo za shetani, hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 268

ٱلشَّيۡطَٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلۡفَقۡرَ وَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغۡفِرَةٗ مِّنۡهُ وَفَضۡلٗاۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Shetani anakutieni hofu ya ufukara na anakuamrisheni uovu, na Allah anakuahidini msamaha utokao kwake na ziada, na Allah ni Mwenye wasaa sana, Mwenye kujua mno



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 155

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ مِنكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ إِنَّمَا ٱسۡتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ بِبَعۡضِ مَا كَسَبُواْۖ وَلَقَدۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Hakika Wale waliorudi miongoni mwenu siku ambayo majeshi mawili yalipokutana, hakika shetani (ndiye) aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya, na kwa hakika Allah amewasamehe. Hakika Allah ni Msamehevu sana Mpole Mno



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 175

إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ يُخَوِّفُ أَوۡلِيَآءَهُۥ فَلَا تَخَافُوهُمۡ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Hakika huyo ni shetani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope wao, bali niogopeni mimi mkiwa nyinyi ni waumini



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 38

وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا

Na ambao wanatoa mali zao kwa kujionesha (na kujitangaza) kwa watu, na hawamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayemfanya shetani kuwa rafiki yake, basi (ajue kuwa huyo ni) rafiki mbaya sana



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 60

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّـٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا

Je, hukuwaona wanaodai kuwa wameamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako wanataka wakahukumiane kwa Twaghuti[1], na ilhali wameamrishwa wamkatae? Na shetani anataka kuwapoteza upotevu wa mbali


1- - Twaghuti ni kila kinachoabudiwa na kutiiwa badala ya Allah ikiwa ni pamoja na shetani, sanamu, mzimu n.k.


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 76

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱلطَّـٰغُوتِ فَقَٰتِلُوٓاْ أَوۡلِيَآءَ ٱلشَّيۡطَٰنِۖ إِنَّ كَيۡدَ ٱلشَّيۡطَٰنِ كَانَ ضَعِيفًا

Walioamini wanapigana katika njia ya Allah, na waliokufuru wanapigana katika njia ya Twaghuti. Basi wapigeni marafiki wa shetani. Hakika, hila za shetani zimekuwa dhaifu sana



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 117

إِن يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَٰثٗا وَإِن يَدۡعُونَ إِلَّا شَيۡطَٰنٗا مَّرِيدٗا

Hawaombi (hawaabudu) badala yake isipokuwa tu wanawake (masanamu)[1], na hawamuombi isipokuwa shetani (Ibilisi) aliyechupa mipaka (katika uasi)


1- - Masanamu hapa yameitwa wanawake sio kwa lengo la kudhalilisha wanawake lakini ni kunukuu hali halisi ya masanamu hayo kwa mujibu wa makafiri wenyewe waliyoyatengeneza. Wanachuoni wametoa ufafanuzi kwamba, masanamu hapa yameitwa wanawake kwa tafsiri mbili.
1. Tafsiri ya kwanza ni kwamba makafiri waliyapa masanamu yao majina ya kike, kama vile Lata, Uza, Manata n.k.
2. Tafsiri ya pili ni kwamba masanamu yameitwa wanawake kwa sababu ya udhaifu wake wa kutoweza kujihami kama ilivyo kwa wanawake.


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 118

لَّعَنَهُ ٱللَّهُۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنۡ عِبَادِكَ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا

Allah amemlaani (shetani). Na amesema (baada ya kulaaniwa): Kwa yakini kabisa, nitachukua katika waja wako fungu lililokadiriwa



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 119

وَلَأُضِلَّنَّهُمۡ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمۡ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلۡقَ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيۡطَٰنَ وَلِيّٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدۡ خَسِرَ خُسۡرَانٗا مُّبِينٗا

Na kwa hakika kabisa, nitawa-poteza na nitawatia matumaini na nitawaamrisha wakate masikio ya wanyama[1], na nitawaamrisha (na) watabadilisha maumbile aliyoyaumba Allah. Na yeyote atakayemfanya shetani mlinzi (wake) badala ya Allah hakika amehasirika hasara inayodhihirisha (uovu wao)


1- - Ukataji wa masikio ya wanyama unaokatazwa hapa ni ule unaombatana na uharibifu na itikadi potofu. Ama utoboaji au upasuaji wa uwekaji wa alama za utambuzi haukatazwi.


Capítulo: ANNISAI 

Verso : 120

يَعِدُهُمۡ وَيُمَنِّيهِمۡۖ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ إِلَّا غُرُورًا

(Shetani) Anawaahidi na anawatumainisha. Na hakuna anachowaahidi shetani isipokuwa hadaa tu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 90

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi mlioamini, ilivyo ni kwamba, ulevi na kamari na masanamu na Ramli ni uchafu utokanao na vitendo vya Shetani, basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 91

إِنَّمَا يُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُوقِعَ بَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ فِي ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِ وَيَصُدَّكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَعَنِ ٱلصَّلَوٰةِۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّنتَهُونَ

Ilivyo ni kwamba, Shetani anataka kuweka uadui na chuki baina yenu kwasababu ya ulevi na kamari, na kukuzuieni kumkumbuka Allah na kuswali. Basi je, mmeacha?



Capítulo: AL-AN’AAM 

Verso : 43

فَلَوۡلَآ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَا تَضَرَّعُواْ وَلَٰكِن قَسَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Basi walau ilipowajia adhabu yetu wangekuwa wanyenyekevu, lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na shetani aliwapambia yale waliyokuwa wanayatenda



Capítulo: AL-AN’AAM 

Verso : 68

وَإِذَا رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَلَا تَقۡعُدۡ بَعۡدَ ٱلذِّكۡرَىٰ مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na utakapowaona wanaozizungumza vibaya Aya zetu, basi wapuuze (na jitenge nao) hadi waingie katika mazungumzo mengine. Na kama shetani atakusahaulisha, basi baada ya kukumbushwa usikae pamoja na watu madhalimu.[1]


1- - Aya hii inawataka Waislamu wahakikishe kuwa maandiko ya dini yao yanaheshimiwa. Pale watakapo ona yanakejiliwa, yanachezewa, yanabezwa au kupotoshwa wasikae kimya bali wakemee na ikibidi waondoke sehemu inapofanyika kejeli hiyo.


Capítulo: AL-AN’AAM 

Verso : 142

وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Na miongoni mwa Wanyama (Allah ameumba) wabebao mizigo na wasiobeba mizigo. Kuleni katika vile Allah alivyokuruzukuni na msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika kabisa, yeye (shetani) kwenu ni adui wa dhahiri



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 11

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَٰكُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ

Na kwa hakika kabisa, tulikuumbeni, kisha tulikutieni sura, kisha tuliwaambia Malaika: Msujudieni Adamu. Walisujudu isipokuwa Ibilisi tu, hakuwa miongoni mwa waliosujudu



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 12

قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ

(Allah) Alisema (akimuuliza Ibilisi): Kipi kilichokuzuia usisujudu pale nilipokuamrisha? (Ibilisi) Alisema: Mimi ni bora zaidi kuliko yeye; umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 13

قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ

(Allah) Akasema: Basi teremka humo. Haikustahiki kwako kufanya kiburi humo. Basi toka. Hakika, wewe ni miongoni mwa walio duni kabisa



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 14

قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

(Ibilisi) Alisema: Nibakishe mpaka Siku (waja wako) wataka-pofufuliwa



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 15

قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

(Allah) Akasema: Hakika, wewe ni miongoni mwa watakaobakishwa



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 16

قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

(Ibilisi) Akasema: Basi kwa sababu umenipotosha (umeniacha nipotoke), nina apa kwamba, nitawakalia (nitawawekea vikwazo) katika njia yako ya sawa



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 17

ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ

Kisha, kwa yakini kabisa, nitawaendea mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao[1]. Na hutapata wengi wao wenye kushukuru


1- - Hapa Ibilisi anakusudia kwamba, atamfuatilia mwanadamu kila alipo. Hii ni sawa na ule msemo wa Kiswahili wa mtaani usemao “Nitakula naye sahani moja”.


Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 18

قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ

(Allah) Akasema (kumwambia Ibilisi kwamba): Toka humo (Peponi) ukiwa umechukiwa, umelaaniwa. Kwa yakini kabisa, yeyote atakayekufuata wewe miongoni mwao hakika nitaijaza Jahanamu kwa (kukutumbukizeni humo) nyinyi nyote



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 19

وَيَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na ewe Adamu, kaa wewe na mkeo Peponi. Basi kuleni katika mpendavyo na msiusogelee mti huu, mtakuwa miongoni mwa madhalimu



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 20

فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ

Basi shetani akawashawishi wawili hao ili awafunulie tupu zao zilizohifadhiwa na kusema (akiwaambia): Mola wenu hakukukatazeni mti huu isipokuwa tu msije mkawa Malaika wawili au mkawa miongoni mwa watakaoishi milele