بَلَىٰۚ مَن كَسَبَ سَيِّئَةٗ وَأَحَٰطَتۡ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Hali si kama wanavyodai. (Hali iko hivi): Wote watendao dhambi na dhambi zao zikawazunguka[1] hao ndio watu wa Motoni; wataishi humo milele
1- - Wakabobea katika kutenda dhambi.
ثُمَّ أَنتُمۡ هَـٰٓؤُلَآءِ تَقۡتُلُونَ أَنفُسَكُمۡ وَتُخۡرِجُونَ فَرِيقٗا مِّنكُم مِّن دِيَٰرِهِمۡ تَظَٰهَرُونَ عَلَيۡهِم بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَإِن يَأۡتُوكُمۡ أُسَٰرَىٰ تُفَٰدُوهُمۡ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيۡكُمۡ إِخۡرَاجُهُمۡۚ أَفَتُؤۡمِنُونَ بِبَعۡضِ ٱلۡكِتَٰبِ وَتَكۡفُرُونَ بِبَعۡضٖۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفۡعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ إِلَّا خِزۡيٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلۡعَذَابِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Kisha nyinyi hao hao mnauana, na mnalitoa kundi kati yenu katika nyumba zao, mkisaidiana dhidi yao, kwa dhambi na uhasama. Na kama wakikujieni ilhali wakiwa mateka mnawakomboa wakati imeharamishwa kwenu kuwafukuza. Je, mnaamini baadhi ya maandiko na mengine mnayakataa? Basi hakuna malipo kwa mwenye kuyafanya hayo kati yenu isipokuwa tu hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watarejeshwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allah si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda
فَمَنۢ بَدَّلَهُۥ بَعۡدَ مَا سَمِعَهُۥ فَإِنَّمَآ إِثۡمُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Na atakayeubadilisha wasia huo baada ya kuusikia, basi ilivyo ni kwamba dhambi yake ipo kwa wale watakaoubadilisha. Hakika, Allah ni Msikiaji mno[1], Mjuzi mno[2]
1- - Wa kauli ya mtoa wasia.
2- - Wa kitendo chake na atamlipa.
فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصٖ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمٗا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na mwenye kuchelea kwa mtoa wasia kupotoka au dhambi akarekebisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu
وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ وَتُدۡلُواْ بِهَآ إِلَى ٱلۡحُكَّامِ لِتَأۡكُلُواْ فَرِيقٗا مِّنۡ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلۡإِثۡمِ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na msile mali zenu baina yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na ilhali mnajua
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ
Na anapoondoka (kwako) anahangaika huku na kule ardhini ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na vizazi. Na Allah hapendi ufisadi
وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ
Na wanapoambiwa; Muogopeni Allah hupandwa na mori wa kufanya uovu. Basi kitakachowatosha ni Jahanamu na ni makazi mabaya mno
۞يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِۖ قُلۡ فِيهِمَآ إِثۡمٞ كَبِيرٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَإِثۡمُهُمَآ أَكۡبَرُ مِن نَّفۡعِهِمَاۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلِ ٱلۡعَفۡوَۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ
Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo kuna dhambi kubwa mno na manufaa kwa watu. Na dhambi za viwili hivyo ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza: Watoe nini? Sema: (Toeni) Kilichozidi mahitaji. Kama hivi Allah anakubainishieni Aya zake ili mpate kutafakari
۞وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ
Na kama mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, basi (mdai) apewe (kitu) kiwe rehani mikononi mwake. Na kama mtaaminiana, basi aliyeaminiwa atekeleze uaminifu wake, na amche Allah, Mola wake Mlezi. Na msifiche ushahidi. Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Allah ni mwenye kuyajua mno yote mnayoyatenda
كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
Sawa na mwenendo wa watu wa Firauni na wale waliokuwepo kabla yao; walizipinga Aya zetu, basi Allah akawaadhibu kwa sababu ya madhambi yao na Allah ni Mkali sana wa kuadhibu
قُلۡ إِن كُنتُمۡ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِي يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allah, basi nifuateni, Allah atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu. Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu
وَٱلَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةً أَوۡ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ ذَكَرُواْ ٱللَّهَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ لِذُنُوبِهِمۡ وَمَن يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ إِلَّا ٱللَّهُ وَلَمۡ يُصِرُّواْ عَلَىٰ مَا فَعَلُواْ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Na ambao wafanyapo uovu (wamadhambi makubwa) au wakazidhulumu nafsi zao (kwa kufanya madhambi madogo) wanamkumbuka Allah na kuomba msamaha kwa dhambi zao (hizo) na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Allah tu, na hawaendelei kufanya (madhambi) waliyoyafanya na ilhali wanajua
وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ خَيۡرٞ لِّأَنفُسِهِمۡۚ إِنَّمَا نُمۡلِي لَهُمۡ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِثۡمٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Na kamwe wasidhani wale waliokufuru kwamba huu muda tunaowapa ni kheri kwao, hakika tunawapa muda ili wazidi kutenda dhambi, na wana adhabu yenye kudhalilisha
وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّي تُبۡتُ ٱلۡـَٰٔنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ كُفَّارٌۚ أُوْلَـٰٓئِكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا
Na haikubaliwi toba kwa wale ambao wanafanya mabaya hadi mmoja wao umauti umfike (ndipo) anasema: Mimi sasa nimetubu, na wala wale wanaokufa wakiwa makafiri. Hao tumewaandalia adhabu yenye maumivu makali mno
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا
Hakika, Allah hatoi msamaha (wa dhambi ya) kushirikishwa na anasamehe (dhambi) isiyokuwa hiyo kwa amtakaye. Na yeyote amshirikishaye Allah basi hakika amezua dhambi kubwa kabisa
ٱنظُرۡ كَيۡفَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثۡمٗا مُّبِينًا
Tazama jinsi wanavyomtungia Allah uongo. Na hayo yanatosha kuwa dhambi zilizo dhahiri
مَّن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةً حَسَنَةٗ يَكُن لَّهُۥ نَصِيبٞ مِّنۡهَاۖ وَمَن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةٗ سَيِّئَةٗ يَكُن لَّهُۥ كِفۡلٞ مِّنۡهَاۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقِيتٗا
Yeyote atakayeombea maombezi mazuri (atakayeingilia kati katika kufanikisha jambo jema) atapata fungu katika jambo zuri hilo, na yeyote atakayeombea maombezi maovu (atakayeingilia kati katika kufanikisha jambo ovu) atapata fungu katika jambo ovu hilo. Na Allahni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu
يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا
Wanajificha wasionekane na watu na wala hawamstahi Allah kuwaona (wanapofanya dhambi) ilhali yeye yuko pamoja nao wakati wanapopanga njama usiku za (kusema) kauli zisizoridhiwa (na Allah). Na Allah anayajua vilivyo yote wayafanyayo
وَمَن يَعۡمَلۡ سُوٓءًا أَوۡ يَظۡلِمۡ نَفۡسَهُۥ ثُمَّ يَسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na yeyote mwenye kutenda baya au kudhulumu nafsi yake, kisha akamuomba msamaha Allah, atamkuta Allah ni Msamehevu sana, Mwenye kurehem
وَمَن يَكۡسِبۡ إِثۡمٗا فَإِنَّمَا يَكۡسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Na yeyote anayechuma dhambi, basi hakika anazichuma kwa (kuidhuru) nafsi yake. Na Allah ni Mjuzi mno, Mwenye hekima nyingi
وَمَن يَكۡسِبۡ خَطِيٓـَٔةً أَوۡ إِثۡمٗا ثُمَّ يَرۡمِ بِهِۦ بَرِيٓـٔٗا فَقَدِ ٱحۡتَمَلَ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا
Na yeyote anayetenda kosa au dhambi kisha akamsingizia asiyekuwa na hatia, basi hakika amebeba uzushi na dhambi inayobainisha (uovu wake)
وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ وَٱلنَّصَٰرَىٰ نَحۡنُ أَبۡنَـٰٓؤُاْ ٱللَّهِ وَأَحِبَّـٰٓؤُهُۥۚ قُلۡ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُمۖ بَلۡ أَنتُم بَشَرٞ مِّمَّنۡ خَلَقَۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ
Na Wayahudi na Wanaswara (Wakristo) walisema: “Sisi ni Wana wa Allah (Mungu) na vipenzi vyake”. Sema: “Basi ni kwa nini anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu (tu) miongoni mwa (watu wengine) aliowaumba. (Allah) Anamsamehe amtakaye (anapotubu) na anamuadhibu amtakaye (asipotubu). Na ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo baina yake, na marejeo ni kwake tu
لَئِنۢ بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقۡتُلَنِي مَآ أَنَا۠ بِبَاسِطٖ يَدِيَ إِلَيۡكَ لِأَقۡتُلَكَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ukininyooshea mkono wako ili kuniua, mimi sitakunyooshea mkono wangu nikuue. Kwa hakika, mimi ninamuogopa Allah, Mola wa walimwengu wote
إِنِّيٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثۡمِي وَإِثۡمِكَ فَتَكُونَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِۚ وَذَٰلِكَ جَزَـٰٓؤُاْ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Mimi ninataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako ili uwe miongoni mwa watu wa motoni. Na hayo ndio malipo ya madhalimu
فَطَوَّعَتۡ لَهُۥ نَفۡسُهُۥ قَتۡلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Basi nafsi yake ikamshawishi kumuua ndugu yake na akamuua na akajikuta ni miongoni mwa waliokula hasara
وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ
Na hukumu baina yao kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, na usifuate utashi wa nafsi zao, na jihadhari nao wasije kukufitini[1] ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Allah. Na wakigeuka, basi jua kwamba, hakika Allah anataka kuwaadhibu kwa (sababu ya) baadhi ya dhambi zao. Na kwa hakika kabisa watu wengi ni waovu
1- - Kukupotosha na kujikuta unafuata na kutekeleza wayatakayo wao.
فَإِنۡ عُثِرَ عَلَىٰٓ أَنَّهُمَا ٱسۡتَحَقَّآ إِثۡمٗا فَـَٔاخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَحَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَوۡلَيَٰنِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ لَشَهَٰدَتُنَآ أَحَقُّ مِن شَهَٰدَتِهِمَا وَمَا ٱعۡتَدَيۡنَآ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ikigundulika kwamba, (mashahidi) wawili hao wametenda dhambi, basi (mashahidi) wawili wengine watasimama mahali pa wale wa mwanzo; hivyo wataapa kwa (jina la) Allah (kwamba): Hakika kabisa, ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wale wawili (wa kwanza) na hatujachupa mipaka; Hakika, wakati huo (tutakapoficha Ushahidi) sisi kwa yakini kabisa tutakuwa miongoni mwa madhalimu
أَلَمۡ يَرَوۡاْ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٖ مَّكَّنَّـٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَا لَمۡ نُمَكِّن لَّكُمۡ وَأَرۡسَلۡنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡهِم مِّدۡرَارٗا وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَنۡهَٰرَ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِينَ
Hivi hawakuona; ni karne ngapi tumeziangamiza kabla yao? Tuliwapa uwezo mkubwa ardhini ambao (nyinyi) hatujakupeni (uwezo kama huo), na tuliwapelekea mawingu yanayotiririsha mvua nyingi (za heri) na tulifanya mito ikipita chini yao. Tuliwaangamiza kwa (sababu ya) madhambi yao na tukaanzisha baada yao karne nyingine
وَذَرُواْ ظَٰهِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَبَاطِنَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡسِبُونَ ٱلۡإِثۡمَ سَيُجۡزَوۡنَ بِمَا كَانُواْ يَقۡتَرِفُونَ
Na acheni dhambi za dhahiri na za siri. Kwa hakika wale ambao wanachuma (wanatenda) dhambi watalipwa yote waliyokuwa wanayatenda
قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Sema: Hakika, ilivyo ni kwamba, Mola wangu Mlezi ameharamisha (mambo) machafu; ya dhahiri katika hayo na ya siri na dhambi na dhuluma bila ya haki yoyote,[1] na kuvishirikisha na Allah vitu ambavyo hakuviteremshia dalili (hoja) yoyote na (pia Allah ameharamisha) kumsemea Allah msiyoyajua
1- - Dhuluma bila ya haki ni dhuluma isiyokuwa na msingi wa kisheria. Ama kutekeleza haki kwa msingi wa sheria sio dhuluma wala ukandamizaji, ila tu limetumika neno dhuluma kwa ulinganifu wa lugha. Inayo onekana kama ni dhuluma kwenye macho ya wapingaji wa sheria za Allah ni kama kuuawa kwa mtu aliyethibitika kuua, kukatwa mkono mtu aliyethibitika kuiba n.k. Lakini hii sio dhuluma ila ni haki kwa sababu ni utekelezaji wa sheria.