Capítulo: MUHAMMAD 

Verso : 3

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَٰلَهُمۡ

Hayo ni kwasababu waliokufuru wamefuata upotevu na walio amini wamefuata haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Allah anavyo wapigia watu mifano yao



Capítulo: AL-FAT-HI 

Verso : 28

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Allah anatosha kuwa Shahidi



Capítulo: QAAF 

Verso : 19

وَجَآءَتۡ سَكۡرَةُ ٱلۡمَوۡتِ بِٱلۡحَقِّۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنۡهُ تَحِيدُ

Na uchungu wa mauti (wa kutoka roho) utakapomjia kwa haki. (Itasemwa): Hayo ndiyo yale uliyokuwa ukiyakimbia



Capítulo: ANNAJMI 

Verso : 28

وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا

Na wala hawana ujuzi wowote ule wa hayo; hawafuati isipokuwa dhana, na hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki



Capítulo: AL-WAAQIA’H 

Verso : 95

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Hakika hii bila shaka ni haki yenye yakini.[1]


1- - Hakika haya yaliotajwa katika Sura hii tukufu bila shaka ni kiini cha yakini ilio thabiti, isiyo ingiliwa na shaka hata kidogo.


Capítulo: ASSWAFF 

Verso : 8

يُرِيدُونَ لِيُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Wanataka kuizima nuru ya Allah kwa vinywa vyao. Na Allah atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia



Capítulo: ASSWAFF 

Verso : 9

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia



Capítulo: ALHAAQQA 

Verso : 51

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na hakika hii (Qur’an) ni haki ya yakini



Capítulo: AL-ASWRI 

Verso : 3

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡحَقِّ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ

Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri