Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 43

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wanaorukuu



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 83

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ

Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi kwa Wana wa Israeli kwamba, hamtamuabudu yeyote Ila Allah tu, na mtawatendea wema wazazi, na ndugu na yatima na maskini, na mseme na watu kwa maneno mazuri. Na simamisheni Swala na toeni Zaka, kisha mkakengeuka isipokuwa wachache tu kati yenu, na ilhali nyinyi mnapuuza



Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 110

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka, na heri yoyote muitanguliziayo kwa ajili yenu mtaikuta mbele ya Allah. Hakika, Allah anayaona mno mnayoyatenda



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 12

۞وَلَقَدۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَبَعَثۡنَا مِنۡهُمُ ٱثۡنَيۡ عَشَرَ نَقِيبٗاۖ وَقَالَ ٱللَّهُ إِنِّي مَعَكُمۡۖ لَئِنۡ أَقَمۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَيۡتُمُ ٱلزَّكَوٰةَ وَءَامَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرۡتُمُوهُمۡ وَأَقۡرَضۡتُمُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّكُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ فَمَن كَفَرَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Na kwa yakini kabisa, Allah alifunga ahadi na Wana wa Israil, na tukatuma miongoni mwao viongozi kumi na mbili (ili wawafundishe utekelezaji wa ahadi hiyo ya Allah) na Allah akasema: Kwa yakini mimi niko pamoja nanyi. Kwa yakini kabisa, kama mkisimamisha Swala na mkitoa Zaka na mkiwaamini Mitume wangu na mkiwapa nguvu (mkiwaunga mkono) na mkimkopesha Allah mkopo mzuri, bila shaka yoyote nitakufutieni maovu yenu na nitakuingizeni katika Pepo zipitazo mito mbele yake. Basi atakayekufuru miongoni mwenu baada ya (makubaliano) hayo, bila shaka amepotea njia ya sawa



Capítulo: AL-AARAAF 

Verso : 156

۞وَٱكۡتُبۡ لَنَا فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِنَّا هُدۡنَآ إِلَيۡكَۚ قَالَ عَذَابِيٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنۡ أَشَآءُۖ وَرَحۡمَتِي وَسِعَتۡ كُلَّ شَيۡءٖۚ فَسَأَكۡتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ

Na tuandikie mazuri katika hii dunia na akhera (pia tuandikie mazuri). Hakika, sisi tumerejea kwako. (Allah) Akasema: Adhabu yangu ninamlenga nimtakaye, na rehema yangu imekienea kila kitu. Basi nitaiandika (hiyo rehema yangu) kwa ambao wanamcha Allah na wanaotoa Zaka na (kwa) wale ambao Aya zetu wanaziamini



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 11

فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِۗ وَنُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Basi (Makafiri) wakitubu (wakiacha ukafiri na kuingia katika Uislamu) na wakasimamisha Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazifafanua Aya kwa watu wanaojua



Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 60

۞إِنَّمَا ٱلصَّدَقَٰتُ لِلۡفُقَرَآءِ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡعَٰمِلِينَ عَلَيۡهَا وَٱلۡمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمۡ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَٱلۡغَٰرِمِينَ وَفِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۖ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Kwa hakika kabisa, sadaka (Zaka) ni za mafakiri[1] na maskini[2] na watumishi[3], na mnaowazoesha nyoyo zao[4] na katika kukomboa watumwa na wenye madeni na katika Njia ya Allah na msafiri. Huu ni wajibu uliofaradhishwa na Allah. Na Allah ni Mwenye kujua, Mwenye hekima sana


1- - Fakiri au fukara ni mtu ambaye hana kabisa uwezo wa kipato kinachoweza kukidhi mahitaji yake ya kila siku.


2- - Maskini ni mtu ambaye anacho kipato lakini hakikidhi kwa asilimia mia moja mahitaji yake ya kila siku.


3- - Ni wale watumishi walioajiriwa kwa kazi ya ukusanyaji wa Zaka.


4- - Hawa ni watu wanaopewa Zaka ili kuzilainisha na kuzivuta nyoyo zao ziukubali na kuupenda Uislamu.


Capítulo: ATTAUBA 

Verso : 103

خُذۡ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡ صَدَقَةٗ تُطَهِّرُهُمۡ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٞ لَّهُمۡۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Chukua sadaka (Zaka) kutoka katika mali zao (waumini ili) uwasafishe na uwatakase kwazo na waombee rehema. Hakika dua yako ni (sababu ya) utuvu kwao. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua



Capítulo: AL-HAJJ 

Verso : 78

وَجَٰهِدُواْ فِي ٱللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِۦۚ هُوَ ٱجۡتَبَىٰكُمۡ وَمَا جَعَلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلدِّينِ مِنۡ حَرَجٖۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمۡ إِبۡرَٰهِيمَۚ هُوَ سَمَّىٰكُمُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ مِن قَبۡلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ ٱلرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيۡكُمۡ وَتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِۚ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱعۡتَصِمُواْ بِٱللَّهِ هُوَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ فَنِعۡمَ ٱلۡمَوۡلَىٰ وَنِعۡمَ ٱلنَّصِيرُ

Na piganeni jihadi katika njia ya Allah kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya Baba yenu Ibrahim. Yeye (Allah) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur’ani) pia, ili Mtume awe shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Allah. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa



Capítulo: ALMUUMINUUN 

Verso : 4

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِلزَّكَوٰةِ فَٰعِلُونَ

Na ambao wanatoa Zaka



Capítulo: ANNUUR 

Verso : 56

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa



Capítulo: ARRUUM 

Verso : 39

وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن رِّبٗا لِّيَرۡبُوَاْ فِيٓ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ فَلَا يَرۡبُواْ عِندَ ٱللَّهِۖ وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن زَكَوٰةٖ تُرِيدُونَ وَجۡهَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُضۡعِفُونَ

Allah ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Allah afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye



Capítulo: ALMUZZAMMIL 

Verso : 20

۞إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Allah ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamuwezi kuweka hesabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qurani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila za Allah, na wengine wanapigana katika Njia ya Allah. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Allah mkopo ulio mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Allah, nayo imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Allah. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu



Capítulo: AL-BAYYINAH 

Verso : 5

وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلۡقَيِّمَةِ

Nao hawakuamrishwa kitu isipokuwa wamuabudu Allah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti