وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نَّصۡبِرَ عَلَىٰ طَعَامٖ وَٰحِدٖ فَٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُخۡرِجۡ لَنَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۢ بَقۡلِهَا وَقِثَّآئِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَاۖ قَالَ أَتَسۡتَبۡدِلُونَ ٱلَّذِي هُوَ أَدۡنَىٰ بِٱلَّذِي هُوَ خَيۡرٌۚ ٱهۡبِطُواْ مِصۡرٗا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلۡتُمۡۗ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ وَٱلۡمَسۡكَنَةُ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ
Na (kumbukeni) mliposema: Ewe Musa, hatutaweza kuvumilia (kula) chakula cha aina moja tu. Basi tuombee kwa Mola wako atutolee katika vile ambavyo ardhi inaotesha, ikiwa ni pamoja na mboga mboga zake na matango yake na vitunguu saumu vyake na dengu zake na vitunguu maji vyake. Musa akasema: Hivi, mnataka kubadilisha ambacho ni duni sana kwa ambacho ni bora zaidi? Shukeni mjini. Huko mtapata hivyo mlivyovitaka. Na wakapigwa chapa ya udhalili na umaskini na wakastahiki ghadhabu za Allah. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikufuru Aya za Allah na wakiwaua Mitume pasina haki yoyote. Hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao, na walikuwa wakichupa mipaka
وَلَمَّا جَآءَهُمۡ كِتَٰبٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٞ لِّمَا مَعَهُمۡ وَكَانُواْ مِن قَبۡلُ يَسۡتَفۡتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُواْ كَفَرُواْ بِهِۦۚ فَلَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na kilipowafikia Kitabu kito-kacho kwa Allah, kinachothibitisha (yale) waliyokuwa nayo, na huko kabla walikuwa wakiomba nusra dhidi ya wale waliokufuru, basi alipowajia huyo waliye mjua, walimkataa. Basi laana ya Allah iwe juu ya makafiri
بِئۡسَمَا ٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡ أَن يَكۡفُرُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغۡيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Ni kibaya mno walichojiuzia[1] cha kukataa yale aliyoyateremsha Allah kwa husuda ya kuwa Allah anamteremshia fadhila zake amtakaye miongoni mwa waja wake. Kwa sababu hiyo, walistahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu yenye kudhalilisha
1- - Walichojichagulia
ضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ أَيۡنَ مَا ثُقِفُوٓاْ إِلَّا بِحَبۡلٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَحَبۡلٖ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَبَآءُو بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَضُرِبَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَسۡكَنَةُۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ
Wamepigwa chapa ya udhalili popote wanapokutwa, isipokuwa (kama) watakuwa wameshika kamba (dini) ya Allah au kamba (misaada) ya watu (wengine). Na wamestahiki ghadhabu za Allah na pia wamepigwa chapa ya umaskini. Hiyo ni kwasababu walikuwa wakizikataa Aya za Allah na kuua Mitume pasina haki yoyote. Hiyo ni kwa sababu ya uasi wao na walikuwa wakichupa mipaka ya sheria (za Allah)
أَفَمَنِ ٱتَّبَعَ رِضۡوَٰنَ ٱللَّهِ كَمَنۢ بَآءَ بِسَخَطٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأۡوَىٰهُ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Je aliyefuata yanayomridhisha Allah, ni kama yule aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allah na makazi yake kuwa jahannamu? Na hayo nimarejeo mabaya mno
وَمَن يَقۡتُلۡ مُؤۡمِنٗا مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَٰلِدٗا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمٗا
Na yeyote anayemuua Muumini (Muislamu) kwa kukusudia basi malipo yake ni Jahanamu, ataishi humo milele na Allah amemghadhibikia na amemlaani na amemuandalia adhabu kubwa kabisa
تَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يَتَوَلَّوۡنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ لَبِئۡسَ مَا قَدَّمَتۡ لَهُمۡ أَنفُسُهُمۡ أَن سَخِطَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَفِي ٱلۡعَذَابِ هُمۡ خَٰلِدُونَ
Utawaona wengi wao wana-wafanya makafiri marafiki (wao) wa ndani. Kwa yakini kabisa, ni maovu sana hayo yaliyotangulia kufanywa na nafsi zao hadi Allah amewakasirikia, na watadumu milele katika adhabu
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ سَيَنَالُهُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَذِلَّةٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُفۡتَرِينَ
Hakika, wale waliomfanya ndama (Mungu) itawapata adhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha ya duniani. Na kama hivyo ndivyo tunavyowalipa wazushi
وَمَن يُوَلِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ دُبُرَهُۥٓ إِلَّا مُتَحَرِّفٗا لِّقِتَالٍ أَوۡ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٖ فَقَدۡ بَآءَ بِغَضَبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأۡوَىٰهُ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo (atakayewakimbia) isipokuwa kama (amefanya hivyo kama) mbinu za vita (geresha) au kuungana na kikosi (cha wapiganaji wenzake), basi atakuwa amestahiki ghadhabu kutoka kwa Allah na makazi yake ni Jahanamu, na huo ni mwisho mbaya mno
مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Hakika anayezusha uongo ni Yule aliyetamka neno la ukafiri baada ya imani isipokuwa tu yule aliyeshurutishwa, ilhali moyo wake unabaki imara katika imani. Lakini wale ambao mioyo yao imeridhika na ukafiri, basi ghadhabu za Allah zitawashukia, na watapata adhabu kubwa
كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَلَا تَطۡغَوۡاْ فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبِيۖ وَمَن يَحۡلِلۡ عَلَيۡهِ غَضَبِي فَقَدۡ هَوَىٰ
Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni, wala msiruke mipaka katika hayo, isije ikakushukieni ghadhabu yangu. Na anayeshukiwa na ghadhabu yangu basi huyo ameangamia
وَٱلۡخَٰمِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَآ إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Allah iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli
هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَـٰٓئِفَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيۡهِ كُفۡرُهُۥۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ إِلَّا مَقۡتٗاۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ كُفۡرُهُمۡ إِلَّا خَسَارٗا
Yeye ndiye aliye kufanyeni manaibu katika ardhi. Na anaye kufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila khasara
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنَادَوۡنَ لَمَقۡتُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُ مِن مَّقۡتِكُمۡ أَنفُسَكُمۡ إِذۡ تُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلۡإِيمَٰنِ فَتَكۡفُرُونَ
Kwa hakika wale walio kufuru watanadiwa: Bila ya shaka Allah kukuchukieni ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipo kuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mkakataa
ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡۖ كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلۡبِ مُتَكَبِّرٖ جَبَّارٖ
Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Allah pasipo ushahidi wowote ulio wafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Allah na mbele ya walio amini. Hivi ndivyo Allah apigavyo muhuri juu ya kila moyo wa jeuri anaye jivuna
وَٱلَّذِينَ يُحَآجُّونَ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ٱسۡتُجِيبَ لَهُۥ حُجَّتُهُمۡ دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمۡ وَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ وَلَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٌ
Na wanaohojiana juu ya Allah baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni baatili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali
فَكَيۡفَ إِذَا تَوَفَّتۡهُمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ
Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُواْ مَآ أَسۡخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُواْ رِضۡوَٰنَهُۥ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Hayo ni kwasababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Allah na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao
وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ ٱلظَّآنِّينَ بِٱللَّهِ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۖ وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَلَعَنَهُمۡ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرٗا
Na awape adhabu wanafiki wanaume na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanao mdhania Allah dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Allah awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahannamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa
كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُواْ مَا لَا تَفۡعَلُونَ
Imekuwa chukizo kubwa mno mbele ya Allah kwamba mnasema msiyoyafanya