Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 101

وَكَيۡفَ تَكۡفُرُونَ وَأَنتُمۡ تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ وَفِيكُمۡ رَسُولُهُۥۗ وَمَن يَعۡتَصِم بِٱللَّهِ فَقَدۡ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na vipi mnakufuru na ilhali mnasomewa Aya za Allah na mnaye Mjumbe wake? Na yeyote atakayeshikamana na Allah, basi hakika ameongozwa katika njia iliyonyooka



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 44

إِنَّآ أَنزَلۡنَا ٱلتَّوۡرَىٰةَ فِيهَا هُدٗى وَنُورٞۚ يَحۡكُمُ بِهَا ٱلنَّبِيُّونَ ٱلَّذِينَ أَسۡلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ بِمَا ٱسۡتُحۡفِظُواْ مِن كِتَٰبِ ٱللَّهِ وَكَانُواْ عَلَيۡهِ شُهَدَآءَۚ فَلَا تَخۡشَوُاْ ٱلنَّاسَ وَٱخۡشَوۡنِ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗاۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Hakika, sisi tumeiteremsha Taurati (ambayo) ndani yake kuna muongozo na nuru. Wanahukumu kwayo Manabii ambao wamejisalimisha (kwa Allah) wakiwahukumu Wayahudi. Na pia (wanahukumu kwa Taurati hiyo) wachamungu (wa Kiyahudi) na wanazuoni (wa Kiyahudi), kwa sababu ya kitabu cha Allah walichotakiwa kukilinda na wakawa mashahidi juu ya hilo. Basi msiwaogope watu na niogopeni Mimi. Na msinunue (msibadilishe) Aya zangu kwa thamani chache. Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio makafiri[1]


1- - Aya hapa inawahusu wenye mamlaka ya utekelezaji wa hukumu na sio kila mtu anahusika. Pia baadhi ya watu wanaichukua Aya hii kwamba ni hoja ya kumtuhumu kuwa ni kafiri kila atendaye dhambi. Watu wa Suna (Ahlu Sunna Wal Jamaa) wanamhesabu mtu ni kafiri endapo atayakataa yaliyomo ndani ya Qur’ani kwa moyo wake na mdomo wake. Ama anayeamini kwa moyo wake na kutamka kwa mdomo wake kwamba yaliyomo ndani ya Qur’ani ni maneno ya Allah na ni sahihi ila tu hatekelezi kwa vitendo huyu haingii katika hukumu ya ukafiri.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 45

وَكَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفۡسَ بِٱلنَّفۡسِ وَٱلۡعَيۡنَ بِٱلۡعَيۡنِ وَٱلۡأَنفَ بِٱلۡأَنفِ وَٱلۡأُذُنَ بِٱلۡأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلۡجُرُوحَ قِصَاصٞۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٞ لَّهُۥۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na humo (ndani ya Taurati) tumewaandikia ya kwamba, roho kwa roho na jicho kwa jicho na pua kwa pua na sikio kwa sikio na jino kwa jino na majeraha ni kisasi. Basi atakayetoa sadaka (ya kusamehe haki yake kulipa kisasi) hiyo ni kafara yake (ya madhambi yake). Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio madhalimu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 47

وَلۡيَحۡكُمۡ أَهۡلُ ٱلۡإِنجِيلِ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فِيهِۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na wahukumu Watu wa Injili kwa sheria alizoziteremsha Allah humo. Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah basi hao ndio waovu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 48

وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَمُهَيۡمِنًا عَلَيۡهِۖ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۖ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ لِكُلّٖ جَعَلۡنَا مِنكُمۡ شِرۡعَةٗ وَمِنۡهَاجٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ

Na tumekuteremshia Kitabu kwa haki kikisadikisha vitabu vilivyokuwepo kabla yake na kikivitawala. Basi hukumu baina yao kwa (sheria) aliyokuteremshia Allah, na usifuate utashi wa nafsi zao ukaacha haki iliyokujia. Kila kundi katika nyinyi tumeliwekea sharia na njia. Na lau Allah angelitaka angekufanyeni (nyote) umma mmoja, lakini (amefanya hivyo) ili akujaribuni katika aliyokupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Allah tu ndio marejeo yenu nyote, na atakuambieni yale mliyokuwa mkitofautiana



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 49

وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ

Na hukumu baina yao kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, na usifuate utashi wa nafsi zao, na jihadhari nao wasije kukufitini[1] ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Allah. Na wakigeuka, basi jua kwamba, hakika Allah anataka kuwaadhibu kwa (sababu ya) baadhi ya dhambi zao. Na kwa hakika kabisa watu wengi ni waovu


1- - Kukupotosha na kujikuta unafuata na kutekeleza wayatakayo wao.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 50

أَفَحُكۡمَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ يَبۡغُونَۚ وَمَنۡ أَحۡسَنُ مِنَ ٱللَّهِ حُكۡمٗا لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Je, ni hukumu za Kijahiliya tu wanazozitaka? Na ni nani mwenye sheria nzuri zaidi kuliko Allah, kwa watu wenye yakini?



Capítulo: AL-QASWAS 

Verso : 50

فَإِن لَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكَ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيۡرِ هُدٗى مِّنَ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu



Capítulo: AL-JAATHIYA 

Verso : 23

أَفَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلۡمٖ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمۡعِهِۦ وَقَلۡبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةٗ فَمَن يَهۡدِيهِ مِنۢ بَعۡدِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Allah akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Allah? Je! Hamkumbuki?