كُتِبَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ إِن تَرَكَ خَيۡرًا ٱلۡوَصِيَّةُ لِلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ
Mmeandikiwa mmoja wenu kutoa wasia kwa wazazi na ndugu kwa namna nzuri anapofikwa na mauti kama akiacha mali, ikiwa ni haki kwa wa mchao Allah
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا وَصِيَّةٗ لِّأَزۡوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٖۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِي مَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٖۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ
Na wale wanaokufa miongoni mwenu na wakaacha wake, waache Usia kwa ajili ya wake zao wapatiwe matunzo kwa mwaka mzima bila ya kuwatoa (majumbani). Na kama watatoka wenyewe, basi hakuna ubaya kwenu kwa kile walichokifanya kwenye nafsi zao. Na Allah ni Mwenye nguvu mno, Mwingi mno wa hekima
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنۡهُ أَوۡ كَثُرَۚ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا
(Watoto) wanaume wana fungu kutokana na kile alichoacha (mmoja wa) wazazi wawili na ndugu wa karibu (pia wanafungu). Na wanawake wanafungu kutokana na alichoacha (mmoja wa) wazazi wawili na ndugu wa karibu (sawa) kiwe kingi au kichache ni fungu lililofaradhishwa
وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا
Na kama (katika kikao cha) kugawa watahudhuria ndugu na Yatima na masikini basi waruzukuni humo chochote, na waambieni kauli nzuri
وَلۡيَخۡشَ ٱلَّذِينَ لَوۡ تَرَكُواْ مِنۡ خَلۡفِهِمۡ ذُرِّيَّةٗ ضِعَٰفًا خَافُواْ عَلَيۡهِمۡ فَلۡيَتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡيَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدًا
Na waogope wale ambao lau kuwa na wao wangeacha nyuma yao kizazi (watoto) wanyonge wakiwahofia (kudhulumiwa na kunyanyaswa), basi wamuogope Allah na waseme neno la kweli
يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِيٓ أَوۡلَٰدِكُمۡۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءٗ فَوۡقَ ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَۖ وَإِن كَانَتۡ وَٰحِدَةٗ فَلَهَا ٱلنِّصۡفُۚ وَلِأَبَوَيۡهِ لِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُۥ وَلَدٞۚ فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلَدٞ وَوَرِثَهُۥٓ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُۚ فَإِن كَانَ لَهُۥٓ إِخۡوَةٞ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِي بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍۗ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ لَا تَدۡرُونَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ لَكُمۡ نَفۡعٗاۚ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Allah anawapeni agizo kwa watoto wenu (kwamba); (mtoto) mwanaume fungu lake ni sawa na mafungu ya (watoto) wanawake wawili na kama watakuwa (watoto) wanawake zaidi ya wawili basi fungu lao ni thuluthi mbili ya alicho kiacha marehemu[1]. Ikiwa binti mmoja basi fungu lake ni nusu tu (ya mali). Na wazazi wake (marehemu baba na mama) kila mmoja wao apate sudusi ikiwa ameacha mtoto (pamoja na wazazi) na ikiwa hakuwacha mtoto akarithiwa na wazazi wawili tu basi mama yake atapata thuluthi na ikiwa (ameacha pamoja na wazazi) ndugu basi mama atapata sudusi, baada ya (kutekeleza) wasia (alioacha marehemu) au deni (analodaiwa). Baba zenu na mama zenu hamjui ni yupi kati yao mwenye maslahi yaliyo karibu mno na nyinyi huo ni uwajibu kutoka kwa Allah, hakika Allah ni mjuzi mno mwenye hekima nyingi
1- - Hapa Aya imeeleza kuwa fungu la watoto wanawake wakiwa zaidi ya wawili itakuwa theluthi mbili swali ni kwamba kama watakuwa wawili? Jibu ni kwamba theluthi mbili ni fungu la mabinti kuanzia wawili na kuendelea kutokana ijimai ya wanazuoni kuwa baada ya kutaja hilo akasema akiwa mmoja fungu lake nusu bila ya kutaja fungu la wawili hiyo inamaanisha kuwa wawili watapata theluthi mbili.
۞وَلَكُمۡ نِصۡفُ مَا تَرَكَ أَزۡوَٰجُكُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٞ فَلَكُمُ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡنَۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِينَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۚ وَلَهُنَّ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّكُمۡ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَكُمۡ وَلَدٞ فَلَهُنَّ ٱلثُّمُنُ مِمَّا تَرَكۡتُمۚ مِّنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ تُوصُونَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۗ وَإِن كَانَ رَجُلٞ يُورَثُ كَلَٰلَةً أَوِ ٱمۡرَأَةٞ وَلَهُۥٓ أَخٌ أَوۡ أُخۡتٞ فَلِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُۚ فَإِن كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمۡ شُرَكَآءُ فِي ٱلثُّلُثِۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصَىٰ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍ غَيۡرَ مُضَآرّٖۚ وَصِيَّةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَلِيمٞ
Na nyinyi mna nusu ya kile walichoacha wake zenu kama hawakuwa na mtoto na kama wakiwa na mtoto, basi fungu lenu ni robo tu ya walichoacha baada ya kutekeleza wasia wanaoweka au deni. Na wake zenu wana robo ya mlicho kiacha ikiwa tu hamkuacha mtoto, na mkiwa na mtoto basi watapata thumni ya mlichokiacha baada ya kutekeleza wasia mnaoweka au deni. Na ikiwa mtu yeyote mwanaume au mwanamke atarithiwa na kaka yake au dada yake kwa kutoacha baba na mtoto, basi kila mmoja wao anafungu la sudusi, na kama watakuwa (ndugu) zaidi ya mmoja basi hao watashirikiana katika thuluthi[1] baada ya kutoa fungu la wasia uliowekwa au deni bila ya madhara. (hili) ni agizo kutoka kwa Allah na Allah ni Mjuzi sana Mpole mno
1- - Kaka na dada waliokusudiwa hapa ni wa upande wa mama kwa dalili kwamba kaka wa baba na mama au wa baba wanachukua kilichobaki baada ya watu wa mafungu na kama hakuna basi anachukua chote. Pia dada anarithi nusu ya mali hana fungu la theluthi, hivyo ni dhahiri hapa waliolengwa ni kaka au dada wa upande wa mama.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَرِثُواْ ٱلنِّسَآءَ كَرۡهٗاۖ وَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ لِتَذۡهَبُواْ بِبَعۡضِ مَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِن كَرِهۡتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَيَجۡعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيۡرٗا كَثِيرٗا
Enyi mlioamini haifai kwenu kumrithi mke bila ridhaa yake[1] na msiwazuie kuolewa (sehemu nyingine) ili wasiondoke na mali mliyowapa ispokuwa kama watafanya zinaa ya wazi na ishini nao kwa wema, na endapo hamtawapenda basi (eleweni kuwa) huenda mkachukia kitu na Allah akajaalia kitu hicho kuwa na kheri nyingi
1- - Kwa kumuoa ndoa mpya na mahari mapya kinyume na ndoa ya mumewe aliyekufa. Wakati wa jahilia wanawake walilirithiwa kama zinavyorithia mali na vitu. mtu alipokufa kaka ama mtoto wa marehemu waliwafanya wake wa marehemu kuwa wake zao bila kuwaoa ndoa mpya au wao ndio waliwaozesha sehemu nyingine kwa kuchukua mahari au waliwazuia kuondoka hata kama hawakuwapenda kuishi nao kama mke ili wasiondoke na mali walizopata wakiwa kwao.
وَلِكُلّٖ جَعَلۡنَا مَوَٰلِيَ مِمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡ فَـَٔاتُوهُمۡ نَصِيبَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا
Na kila mtu tumemuwekea warithi katika vile ambavyo vimeachwa na wazazi na ndugu. Na wale mliofunga nao mikataba ya viapo (kuwa mtakuwa ndugu) wapeni sehemu yao (ya mirathi)[1]. Hakika, Allah ni Shahidi wa kila kitu
1- - Aya hii inazungumzia udugu wa kupanga (udugu wa Yamini). Udugu huu ulikuwepo mwanzo wa Uislamu, na ndugu wa udugu huu walikuwa wakirithiana. Urithi huu ulifutwa na Aya 11 - 12 za Sura hii.
يَسۡتَفۡتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِي ٱلۡكَلَٰلَةِۚ إِنِ ٱمۡرُؤٌاْ هَلَكَ لَيۡسَ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَهُۥٓ أُخۡتٞ فَلَهَا نِصۡفُ مَا تَرَكَۚ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهَا وَلَدٞۚ فَإِن كَانَتَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَۚ وَإِن كَانُوٓاْ إِخۡوَةٗ رِّجَالٗا وَنِسَآءٗ فَلِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۗ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ أَن تَضِلُّواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ
Wanakutaka Fat’wa. Sema: Allah anakupeni Fat’wa kuhusu Kalala.[1] Ikiwa mtu aliyekufa hakuacha mtoto na amemuacha dada, basi huyo dada anastahiki kupata nusu ya mali aliyoacha. Na yeye atamrithi dada yake kama (dada naye) hakuacha mtoto. (Dada) Wakiwa wawili watapata thuluthi mbili katika mali aliyoacha (marehemu kaka yao). Na (warithi) wakiwa ndugu; wanaume na wanawake basi mwanaume mmoja anastahiki kupata fungu lililo sawa na la wanawake wawili. Allah anakubainishieni nyinyi (sheria zake) ili msipotee. Na Allah ni Mjuzi wa kila kitu
1- - Kalala ni mtu aliyekufa akiwa hakuacha mzazi wala mtoto.
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ شَهَٰدَةُ بَيۡنِكُمۡ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ حِينَ ٱلۡوَصِيَّةِ ٱثۡنَانِ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ أَوۡ ءَاخَرَانِ مِنۡ غَيۡرِكُمۡ إِنۡ أَنتُمۡ ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَأَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةُ ٱلۡمَوۡتِۚ تَحۡبِسُونَهُمَا مِنۢ بَعۡدِ ٱلصَّلَوٰةِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ لَا نَشۡتَرِي بِهِۦ ثَمَنٗا وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰ وَلَا نَكۡتُمُ شَهَٰدَةَ ٱللَّهِ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلۡأٓثِمِينَ
Enyi mlioamini, ushahidi wa baina yenu kinapomfikia mmoja wenu kifo wakati wa kuusia ni (mashahidi) wawili waadilifu miongoni mwenu au wawili wengine wasiokuwa katika nyinyi, mnapokuwa safarini na ukakusibuni msiba wa kifo. Mtawazuia wawili hao baada ya Swala. Waape kwa (jina la) Allah mkiwa na shaka (wakisema): Hatununui (hatupokei) thamani yoyote kwa haya (tunayoyatolea ushahidi) hata kama (tunaowatolea ushahidi dhidi yao) wakiwa ndugu wa nasaba, na hatufichi ushahidi wa Allah. Hakika, sisi tukifanya hivyo kwa yakini kabisa tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi
فَإِنۡ عُثِرَ عَلَىٰٓ أَنَّهُمَا ٱسۡتَحَقَّآ إِثۡمٗا فَـَٔاخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَحَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَوۡلَيَٰنِ فَيُقۡسِمَانِ بِٱللَّهِ لَشَهَٰدَتُنَآ أَحَقُّ مِن شَهَٰدَتِهِمَا وَمَا ٱعۡتَدَيۡنَآ إِنَّآ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ikigundulika kwamba, (mashahidi) wawili hao wametenda dhambi, basi (mashahidi) wawili wengine watasimama mahali pa wale wa mwanzo; hivyo wataapa kwa (jina la) Allah (kwamba): Hakika kabisa, ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wale wawili (wa kwanza) na hatujachupa mipaka; Hakika, wakati huo (tutakapoficha Ushahidi) sisi kwa yakini kabisa tutakuwa miongoni mwa madhalimu
ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِٱلشَّهَٰدَةِ عَلَىٰ وَجۡهِهَآ أَوۡ يَخَافُوٓاْ أَن تُرَدَّ أَيۡمَٰنُۢ بَعۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡمَعُواْۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Hilo linaelekea karibu zaidi watoe ushahidi kwa usahihi wake au wahofie viapo kukataliwa baada ya viapo vyao. Na mcheni Allah na sikieni. Na hakika, Allah hawaongoi watu waovu