Capítulo: AL-BAQARAH 

Verso : 222

وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡمَحِيضِۖ قُلۡ هُوَ أَذٗى فَٱعۡتَزِلُواْ ٱلنِّسَآءَ فِي ٱلۡمَحِيضِ وَلَا تَقۡرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطۡهُرۡنَۖ فَإِذَا تَطَهَّرۡنَ فَأۡتُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَكُمُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلتَّوَّـٰبِينَ وَيُحِبُّ ٱلۡمُتَطَهِّرِينَ

Na wanakuuliza kuhusu Hedhi. Sema: Huo ni uchafu. Basi waepukeni wanawake (wake zenu) katika kipindi cha Hedhi, na msiwasogelee (msifanye nao jimai) mpaka watoharike. Na watakapojitoharisha, basi waendeeni kwa kupitia alipokuamrisheni Allah. Hakika, Allah anawapenda wenye kujitoharisha na anawapenda wenye kutubu sana



Capítulo: ANNISAI 

Verso : 43

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡرَبُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمۡ سُكَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعۡلَمُواْ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغۡتَسِلُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا

Enyi mlioamini, msiisogelee swala (msiswali) ilhali mmelewa, hadi mjue mnachosema.[1] Na (msiingie msikitini kwa ajili ya kuswali) mnapokuwa na janaba isipokuwa tu kama mtapita njia (kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine) hadi muoge. Na kama mkiwa wagonjwa (na hamuwezi kutawadha au kuoga kwa maji) au mkiwa safarini au mmoja wenu ametoka chooni (kukidhi haja) au mkigusana (mkiingiliana) na wake zenu na mkakosa maji, basi tayamamuni mchanga mzuri (safi); basi pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika, Allah amekuwa Msamehevu sana, Mfutaji dhambi


1- - Hapa ilikuwa pombe haijaharamishwa. Ama baada ya pombe kuharamishwa kabisa kwa aya ya 90 ya Sura Almaida (5), suala la mtu kuswali akiwa amelewa halipo, hata kama atakuwa anaelewa anachokisema na anachokifanya.