وَزَكَرِيَّا وَيَحۡيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلۡيَاسَۖ كُلّٞ مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na Zakaria na Yahaya na Issa na Iliasa. Wote ni miongoni mwa watu wema
Compartir :
وَإِنَّ إِلۡيَاسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume
إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia watu wake: Hamuogopi?
أَتَدۡعُونَ بَعۡلٗا وَتَذَرُونَ أَحۡسَنَ ٱلۡخَٰلِقِينَ
Mnamwomba Baali na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
ٱللَّهَ رَبَّكُمۡ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Allah, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Allah walio safishwa
وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye
سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلۡ يَاسِينَ
Iwe salama kwa Ilyas
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema
إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini