Capítulo: ANNISAI 

Verso : 92

وَمَا كَانَ لِمُؤۡمِنٍ أَن يَقۡتُلَ مُؤۡمِنًا إِلَّا خَطَـٔٗاۚ وَمَن قَتَلَ مُؤۡمِنًا خَطَـٔٗا فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖ وَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَصَّدَّقُواْۚ فَإِن كَانَ مِن قَوۡمٍ عَدُوّٖ لَّكُمۡ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ وَإِن كَانَ مِن قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞ فَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ وَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ تَوۡبَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na haiwi kwa Muumini (Muis-lamu) yeyote kumuua Muumini (mwingine) isipokuwa tu kwa kukosea. Na yeyote aliyemuua Muumini kwa kukosea, basi (adhabu yake) ni kuacha huru mtumwa Muumini (Muislamu) na Dia (fidia)[1] itakayokabidhiwa kwa ndugu zake (warithi wake), isipokuwa tu kama (ndugu hao) watafanya Dia hiyo sadaka (kwa kusamehe). Na kama (aliyeuliwa) ni kutoka kwa watu maadui wenu (makafiri), na yeye (marehemu) ni Mumini (Muislamu), basi (adhabu ya muuaji) ni kuacha huru mtumwa Muislamu tu.[2] Na kama (aliyeuliwa) ni kutoka kwa watu (makafiri) ambao kuna mkataba kati yenu na wao (wa kuishi kwa amani) basi (adhabu ya muuaji) ni Dia (fidia) itakayokabidhiwa kwa ndugu zake na kuacha huru mtumwa Muislamu[3]. Basi ambaye hakupata (mtumwa wa kumuacha huru adhabu yake) ni kufunga miezi miwili mfululizo. (Hii) Ndio toba kutoka kwa Allah, na Allah ni Mjuzi sana, Mwenye hekima nyingi


1- - Dia au fidia ya kuua ni ngamia mia moja (100) kama alivyoainisha Mtume, Allah amshushie rehema na amani, katika waraka alioutuma kwa watu wa Yemen. Ameyanukuu haya Imamu Malik katika kitabu chake cha Muwattwai.


2- - Hapa aya inamaanisha kuwa aliyeuliwa ni Muislamu lakini ndugu zake ni makafiri. Hivyo hakuna fidia itakayotolewa isipokuwa tu kuacha huru Mtumwa Muislamu. Kwa nini fidia hapa haipo? Ni kwa sababu fidia kama itatolewa itakwenda kwa makafiri wenye uadui na Uislamu. Kuwapa fidia makafiri maadui ni kuwapa nguvu dhidi ya Waislamu.


3- - Pamoja na kwamba ndugu wa Muislamu aliyeuliwa ni makafiri lakini hapa Uislamu unawapa fidia kwa sababu fidia hiyo haitarajiwi kutumika katika kuwadhuru Waislamu kwa sababu makafiri hawa wamo katika mkataba wa kuishi kwa amani. Hapa tunajifunza namna Uislamu unavyothamini amani na utulivu katika jamii. Ndugu wa marehemu kama ni makafiri wasioingia mkataba wa amani na Waislamu hawapewi Dia. Ama kama ni makafiri walioingia mkataba wa amani na Waislamu wanapewa Dia kwa kuzingatia amani.


Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 45

وَكَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفۡسَ بِٱلنَّفۡسِ وَٱلۡعَيۡنَ بِٱلۡعَيۡنِ وَٱلۡأَنفَ بِٱلۡأَنفِ وَٱلۡأُذُنَ بِٱلۡأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلۡجُرُوحَ قِصَاصٞۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٞ لَّهُۥۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na humo (ndani ya Taurati) tumewaandikia ya kwamba, roho kwa roho na jicho kwa jicho na pua kwa pua na sikio kwa sikio na jino kwa jino na majeraha ni kisasi. Basi atakayetoa sadaka (ya kusamehe haki yake kulipa kisasi) hiyo ni kafara yake (ya madhambi yake). Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio madhalimu



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 89

لَا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ ٱلۡأَيۡمَٰنَۖ فَكَفَّـٰرَتُهُۥٓ إِطۡعَامُ عَشَرَةِ مَسَٰكِينَ مِنۡ أَوۡسَطِ مَا تُطۡعِمُونَ أَهۡلِيكُمۡ أَوۡ كِسۡوَتُهُمۡ أَوۡ تَحۡرِيرُ رَقَبَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖۚ ذَٰلِكَ كَفَّـٰرَةُ أَيۡمَٰنِكُمۡ إِذَا حَلَفۡتُمۡۚ وَٱحۡفَظُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Allah hakuchukulieni hatua kwa viapo vyenu vya kipuuzi, lakini anakuchukulieni hatua kwa (viapo) mlivyovikusudia kweli kweli. Basi Kafara (adhabu) yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacholisha familia zenu au kuwavalisha (kuwapa nguo) au kumkomboa mtumwa. Asiyepata hayo, basi afunge siku tatu. Hiyo ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini (lindeni) viapo vyenu. Namna hivyo Allah anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru



Capítulo: AL-MAIDA 

Verso : 95

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡتُلُواْ ٱلصَّيۡدَ وَأَنتُمۡ حُرُمٞۚ وَمَن قَتَلَهُۥ مِنكُم مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآءٞ مِّثۡلُ مَا قَتَلَ مِنَ ٱلنَّعَمِ يَحۡكُمُ بِهِۦ ذَوَا عَدۡلٖ مِّنكُمۡ هَدۡيَۢا بَٰلِغَ ٱلۡكَعۡبَةِ أَوۡ كَفَّـٰرَةٞ طَعَامُ مَسَٰكِينَ أَوۡ عَدۡلُ ذَٰلِكَ صِيَامٗا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمۡرِهِۦۗ عَفَا ٱللَّهُ عَمَّا سَلَفَۚ وَمَنۡ عَادَ فَيَنتَقِمُ ٱللَّهُ مِنۡهُۚ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ

Enyi mlioamini, msiue wanya-mapori na hali mmeharimia (mmo ndani ya ibada ya Hija au Umra). Na yeyote miongoni mwenu atakayemuua mnyama huyo kwa makusudi, basi malipo (yake) ni (kuchinja) mnyama wa kufuga mfano wa aliyemuua. Watahukumu hayo waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama (huyo) apelekwe Al-Kaaba (Makkah ili achinjwe huko na nyama yake kugaiwa sadaka kwa maskini wa huko) au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini au badala ya hayo ni kufunga ili (aliyefanya kosa hilo la kuwinda) aonje ubaya wa jambo lake (baya alilolifanya). Allah amekwishafuta yaliyopita (lakini) atakayerudia (kufanya tena kosa hilo) Allah atamuadhibu. Na Allah ni Mwenye nguvu sana, Mwenye kutesa



Capítulo: AL-MUJAADILA 

Verso : 3

وَٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمۡ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُواْ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مِّن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۚ ذَٰلِكُمۡ تُوعَظُونَ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na wale ambao wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allah kwa yale myatendayo ni Mwenye khabari kwa yale mnayo yatenda



Capítulo: AL-MUJAADILA 

Verso : 4

فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينٗاۚ ذَٰلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Na yule asiyepata uwezo, basi afunge Swiyaam miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo