وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّـٰكِرِينَ
Na simamisha swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huo ni ukumbusho kwa wale wanaokumbuka
وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na subiri (kuwa mvumilivu), kwani Allah hapotezi ujira wa wafanyao wema
فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Na lau ingekuwepo katika karine za kabla yenu masalia ya watu wa kheri wanakataza maovu ardhini, (lakini hawakuwepo miongoni mwa watu wa kheri) isipokuwa wachache tu. Miongoni mwa (walioamini) tuliowaokoa kutoka kwenye adhabu. Na wale waliodhulumu wakafuata starehe zao walizoneemeshwa, na wakawa waovu
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ
Na hakuwa Mola wako mlezi ni mwenye kuangamiza watu wa miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema
وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخۡتَلِفِينَ
Na lau angetaka Mola wako mlezi ange wafanya watu wote kuwa umma mmoja. Na hawaachi kukhitalifiana,
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa tu wale Mola wako mlezi amewarehemu (wakaamini); na Allah amewaumba hivyo. Na neno la Mola wako mlezi litatimia: Kwe hakika nitaijaza Jahannam miongoni mwa majini na watu wote kwa pamoja
وَكُلّٗا نَّقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَۚ وَجَآءَكَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَقُّ وَمَوۡعِظَةٞ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Na yote haya tunakusimulia miongoni mwa habari za Mitume yale yanayoupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa waumini
وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنَّا عَٰمِلُونَ
Na waambie wale wasio amini: Fanyeni muwezavyo, nasi pia tunafanya (tuwezavyo)
وَٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ
Na ngojeni, na sisi tunangoja
وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُ ٱلۡأَمۡرُ كُلُّهُۥ فَٱعۡبُدۡهُ وَتَوَكَّلۡ عَلَيۡهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Na ni vya Allah tu vyote vilivyo fichikana mbinguni na ardhini, na mambo yote yatarudishwa kwake tu. Basi muabudu yeye na umtegemee yeye. Na Mola wako mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda
الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Alif Laam Raa[1]. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha
1- - Allah ndiye ajuaye zaidi maana ya herufi mkato hizi.
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Hakika, sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu ili mpate kuelewa
نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa (huu) Wahyi tuliokufunulia wa hii Qur’ani, na ingawa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua
إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ
(Kumbuka) Wakati Yusuf alipomwambia baba yake (Yakubu kwamba): Ewe Baba yangu, hakika mimi niliona (usingizini) nyota kumi na moja na jua na mwezi; nimeziona zikinisujudia
قَالَ يَٰبُنَيَّ لَا تَقۡصُصۡ رُءۡيَاكَ عَلَىٰٓ إِخۡوَتِكَ فَيَكِيدُواْ لَكَ كَيۡدًاۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٞ مُّبِينٞ
(Yakubu) Alisema: Ewe kijana wangu, usiwasimulie ndugu zako ndoto yako, wasije wakakufanyia hila (husuda). Hakika, shetani kwa mwanadamu ni adui wa wazi
وَكَذَٰلِكَ يَجۡتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعۡقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيۡكَ مِن قَبۡلُ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Na kama hivyo anakuteua Mola wako Mlezi na akakufundisha tafsiri za matukio (ndoto) na anatimiza neema zake kwako na kwa familia ya Yakubu, kama alivyozitimizia (neema hizo) kwa Baba zako wawili hapo kabla; Ibrahimu na Is-haka[1]. Hakika, Mola wako Mlezi ni Mjuzi, Mwenye hekima
1- - Hawa ni mababu wa Nabii Yusuf. Katika lugha ya Qur’ani babu anahisabika ni baba.
۞لَّقَدۡ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخۡوَتِهِۦٓ ءَايَٰتٞ لِّلسَّآئِلِينَ
Kwa yakini kabisa, katika (kisa cha) Yusuf na ndugu zake zipo ishara (nyingi) kwa wanaouliza
إِذۡ قَالُواْ لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰٓ أَبِينَا مِنَّا وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ
(Kumbukeni) Wakati (ndugu wa Yusuf) waliposema: Kwa hakika kabisa, Yusuf na nduguye (wa mama mmoja) wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, na ilihali sisi ni wengi. Hakika, Baba yetu yumo kwenye upotevu ulio wazi (anafanya kosa la wazi)
ٱقۡتُلُواْ يُوسُفَ أَوِ ٱطۡرَحُوهُ أَرۡضٗا يَخۡلُ لَكُمۡ وَجۡهُ أَبِيكُمۡ وَتَكُونُواْ مِنۢ بَعۡدِهِۦ قَوۡمٗا صَٰلِحِينَ
(Ndugu wa Yusuf walisema): Muueni Yusuf au mtupeni ardhi (ya mbali) ili uso (na upendo) wa Baba yenu utakuelekeeni nyinyi tena baada yake (baada ya kumuua Yusuf mtatubu dhambi hiyo na) mtakuwa watu wema
قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ لَا تَقۡتُلُواْ يُوسُفَ وَأَلۡقُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّ يَلۡتَقِطۡهُ بَعۡضُ ٱلسَّيَّارَةِ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Alisema msemaji kati yao: Msimuue Yusuf (lakini) mtupeni kwenye kina cha kisima (kirefu) ataokotwa na baadhi ya wasafiri kama nyinyi mna azma ya kufanya (jambo la kumtenganisha na baba yake)
قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأۡمَ۬نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَٰصِحُونَ
(Nduguze baada ya kuafikiana) Walisema: Ewe Baba yetu, una nini hata hutuamini kwa Yusuf na ilihali sisi, kwa hakika, ni wenye kumtakia mema?
أَرۡسِلۡهُ مَعَنَا غَدٗا يَرۡتَعۡ وَيَلۡعَبۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Mruhusu kesho (atoke) pamoja nasi (kwenda malishoni) atakula na kucheza kwa furaha, nakwa yakini kabisa, sisi tutamlinda
قَالَ إِنِّي لَيَحۡزُنُنِيٓ أَن تَذۡهَبُواْ بِهِۦ وَأَخَافُ أَن يَأۡكُلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَأَنتُمۡ عَنۡهُ غَٰفِلُونَ
(Yakubu) Alisema: Kwa hakika kabisa, inanihuzunisha nyinyi kwenda naye (na kuniacha peke yangu) na nachelea asije akaliwa na mbwa mwitu ilihali nyinyi mkiwa mmeghafilika
قَالُواْ لَئِنۡ أَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّآ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ
Walisema (kumwambia Baba yao): Iwapo ataliwa na mbwa mwitu na ilihali sisi ni wengi (kundi lenye nguvu), bila ya shaka sisi wakati huo tutakuwa hasarani (hatuna faida)
فَلَمَّا ذَهَبُواْ بِهِۦ وَأَجۡمَعُوٓاْ أَن يَجۡعَلُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمۡرِهِمۡ هَٰذَا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Basi walipokwenda naye na kukubaliana kumtumbukiza (kumtosa) katika kina cha kisima kirefu, na tulimfunulia Wahyi Yusuf (hapo kisimani kwamba): Hapana shaka yoyote utakuja kuwaambia (siku za usoni) kuhusu jambo lao hili, na wala wao hawatahisi (kama wewe ni Yusuf)
وَجَآءُوٓ أَبَاهُمۡ عِشَآءٗ يَبۡكُونَ
Walimjia Baba yao (wakati wa) usiku huku wakiangua kilio (cha uongo)
قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبۡنَا نَسۡتَبِقُ وَتَرَكۡنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤۡمِنٖ لَّنَا وَلَوۡ كُنَّا صَٰدِقِينَ
Walisema: Ewe Baba yetu, hakika sisi tulikwenda kushindana na tulimuacha Yusuf kwenye vitu vyetu, basi akaliwa na mbwa mwitu (lakini wewe hutatuamini na hata kama tunasema kweli
وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٖ كَذِبٖۚ قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٞۖ وَٱللَّهُ ٱلۡمُسۡتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ
Walikuja na kanzu yake huku ikiwa na damu ya uongo. (Yakubu alipobaini geresha yao) (Yakubu) Alisema: “Bali nafsi zenu zimekushawishini (kutenda) jambo (baya). Basi subira ni jambo zuri, na Allah ndiye wa kuombwa msaada kwa huu (uongo) mnaoueleza”
وَجَآءَتۡ سَيَّارَةٞ فَأَرۡسَلُواْ وَارِدَهُمۡ فَأَدۡلَىٰ دَلۡوَهُۥۖ قَالَ يَٰبُشۡرَىٰ هَٰذَا غُلَٰمٞۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَٰعَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ
Na uliwasili msafara, na ukamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake (ili kuchota maji). Alisema: Furaha iliyoje! Huyu hapa mvulana! Na walimficha akiwa (kama) bidhaa. Na Allah ni Mjuzi wa wanayoyatenda
وَشَرَوۡهُ بِثَمَنِۭ بَخۡسٖ دَرَٰهِمَ مَعۡدُودَةٖ وَكَانُواْ فِيهِ مِنَ ٱلزَّـٰهِدِينَ
Na (wale wasafiri) walimuuza (Yusuf) kwa thamani duni; pesa chache. Na hawakuwa na haja naye