كَذَّبَتۡ ثَمُودُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kina Thamud waliwakanusha Mitume
Tarayya :
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchi Allah?
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Allah, na nitiini
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
أَتُتۡرَكُونَ فِي مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ
Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
فِي جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٖ
Katika mabustani, na chemchem?
وَزُرُوعٖ وَنَخۡلٖ طَلۡعُهَا هَضِيمٞ
Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva
وَتَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا فَٰرِهِينَ
Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi
Basi mcheni Allah, na nitiini mimi
وَلَا تُطِيعُوٓاْ أَمۡرَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Wala msitii amri za walio pindukia mipaka,
ٱلَّذِينَ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ
Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi
قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa
مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا فَأۡتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli
قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٞ لَّهَا شِرۡبٞ وَلَكُمۡ شِرۡبُ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابُ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa
فَعَقَرُوهَا فَأَصۡبَحُواْ نَٰدِمِينَ
Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta
فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Watu wa Lutwi waliwakanusha Mitume
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Lutwi: Je! Hamumchi Allah?
Basi mcheni Allah na nitiini mimi
Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
أَتَأۡتُونَ ٱلذُّكۡرَانَ مِنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Je! mnawaingilia wanaume katika walimwengu?
وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٌ عَادُونَ
Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka!
قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُخۡرَجِينَ
Wakasema: Ewe Lutwi! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!
قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلۡقَالِينَ
Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu
رَبِّ نَجِّنِي وَأَهۡلِي مِمَّا يَعۡمَلُونَ
Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo
فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,