إِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٖ مِّنۡهُ ٱسۡمُهُ ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ وَجِيهٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
(Kumbuka) Malaika waliposema: Ewe Mariamu, hakika Allah anakubashiria (mtoto atakayepatikana) kwa neno kutoka kwake. Jina lake ni Masihi Isa bin Mariamu. Ni mwenye heshima duniani na akhera, na ni miongoni mwa watakaokurubishwa
وَيُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗا وَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na atazungumza na watu akiwa mtoto mchanga na akiwa mtu mzima, na atakuwa miongoni mwa watu wema
قَالَتۡ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞۖ قَالَ كَذَٰلِكِ ٱللَّهُ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Mariamu akasema: Ewe Mola wangu, nitapataje mtoto na ilhali hajanigusa mtu yeyote na sikuwa mzinifu? Akasema: Hivyo ndivyo Allah anaumba atakavyo; pindi anapohukumu jambo huliambia: Kuwa na linakuwa
وَيُعَلِّمُهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ
Na atamfundisha kitabu na hekima na Taurati na Injili
وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ أَنِّي قَدۡ جِئۡتُكُم بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ أَنِّيٓ أَخۡلُقُ لَكُم مِّنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ وَأُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأۡكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
Na ni Mjumbe kwa Wana wa Israili (akiwa na ujumbe kwamba) hakika: Mimi nimekuleteeni muujiza kutoka kwa Mola wenu; hakika mimi nawaumbieni kutoka katika udongo umbile kama la ndege kisha na mpulizia na anakuwa ndege kwa idhini ya Allah. Na ninaponya kipofu na mwenye ukoma, na ninafufua wafu kwa idhini ya Allah, na nitawaambia kile mnachokula na mnachoweka akiba majumbani mwenu. Hakika, katika haya yote kuna ishara kwenu mkiwa ni wenye kuamini
وَمُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعۡضَ ٱلَّذِي حُرِّمَ عَلَيۡكُمۡۚ وَجِئۡتُكُم بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Na ni mwenye kusadiki Taurati iliyoteremshwa kabla yangu, na ili ni kuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu, na nimekujieni na ishara kutoka kwa Mola wenu. Basi mcheni Allah na mnitii
إِنَّ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ
Hakika Allah ndiye Mola wangu na Mola wenu, basi muabuduni. Hii ndiyo njia iliyonyooka
۞فَلَمَّآ أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنۡهُمُ ٱلۡكُفۡرَ قَالَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَٱشۡهَدۡ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ
Isa alipohisi ukafiri kwao alisema: Ni nani watakaonisaidia katika kuelekea kwa Allah (kwa kuinusuru dini yake)? Wafuasi watiifu wakasema: Sisi niwatetezi wa (dini ya) Allah; tumemuamini Allah nashuhudia kwamba sisi ni Waislamu
رَبَّنَآ ءَامَنَّا بِمَآ أَنزَلۡتَ وَٱتَّبَعۡنَا ٱلرَّسُولَ فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Ewe Mola wetu, tumeyaamini yote uliyoyateremsha na tumemfuata Mtume, basi tuandike (kuwa) pamoja na Mashahidi
وَمَكَرُواْ وَمَكَرَ ٱللَّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ
Na wamepanga njama (dhidi ya Mtume wa Allah) na Allah amepanga njama (dhidi yao) na Allah ni zaidi ya wenye kupanga njama
إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَىٰٓ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَجَاعِلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوكَ فَوۡقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ فِيمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
(Kumbuka) Allah aliposema: Ewe Isa, hakika mimi ni Mwenye kukufisha[1] na ni Mwenye kukupaisha kwangu na ni Mwenye kukutakasa dhidi ya waliokufuru, na ni Mwenye kuwafanya waliokufuata wawe juu ya waliokufuru mpaka Siku ya Kiama. Kisha, kwangu tu ndio marejeo yenu, na nitahukumu baina yenu katika yale ambayo mmetofautiana
1- - Wanazuoni katika kutafsiri neno “kufisha” katika Kurani wana kauli mbili. Shekh Twantwawiy amezieleza kauli hizi katika tafsiri yake ya Alwasiitw alipoizungumzia Aya hii kwa kusema kuwa:
Neno “Kufisha” limekuja kwa maana ya kufikwa na mauti, kwa maana kwamba kiumbe anavuliwa roho yake na kutenganishwa na kiwiliwili chake. Allah anasema kuwa: “Hakika wale ambao wamefishwa na Malaika (kwa kutenganishwa roho na viwili wili vyao) …”. Sura Annisaa (4), Aya ya 97.
Neno “kufisha” lina maana ya kulaza usingizini. Hii ina maana kwamba, Allah alimwambia Nabii Isa kuwa atamlaza usingizi na kumpaisha kwake mbimguni.
Hii ndio maana iliyokusudiwa kati Aya hii kwa kuzingatia ushahidi ufuatao:
Neno “kufisha” limetumika katika Kurani kwa maana ya kufa na kwa maana ya kulala katika maeneo tofauti. Kati ya maeneo hayo ni pale Allah aliposema katika Sura Azzumar (39), Aya ya 42 . Hapa kufisha kumetumika kwa maana mbili; ya kutoa uhai na ya kulaza
usingizini.
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَأُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Ama waliokufuru nitawaadhibu adhabu kali duniani na Akhera, na hawatakuwa na yeyote wa kuwanusuru
وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ama walioamini na wakatenda mema, basi (Allah) atawalipa malipo yao kamili, na Allah hawapendi madhalimu
ذَٰلِكَ نَتۡلُوهُ عَلَيۡكَ مِنَ ٱلۡأٓيَٰتِ وَٱلذِّكۡرِ ٱلۡحَكِيمِ
Hayo tunayokusomea ni katika Aya na ukumbusho wenye hekima mno
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَۖ خَلَقَهُۥ مِن تُرَابٖ ثُمَّ قَالَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Hakika mfano (wa uumbwaji) wa Isa kwa Allah ni mfano wa (kuumbwa kwa) Adamu; (Allah) amemuumba kwa udongo, kisha akamwambia: Kuwa na akawa
ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ
Haki inatoka kwa Mola wako tu, basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka
فَمَنۡ حَآجَّكَ فِيهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ فَقُلۡ تَعَالَوۡاْ نَدۡعُ أَبۡنَآءَنَا وَأَبۡنَآءَكُمۡ وَنِسَآءَنَا وَنِسَآءَكُمۡ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمۡ ثُمَّ نَبۡتَهِلۡ فَنَجۡعَل لَّعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰذِبِينَ
Na yeyote atakayekuhoji katika hili baada ya kukufikia elimu, basi sema: Njooni, tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi na nyinyi, kisha tuombe kwa unyenyekevu ili laana ya Allah iwashukie waliokadhibisha
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡقَصَصُ ٱلۡحَقُّۚ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Hakika, hivi ndivyo visa vya kweli, na hakuna wakuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu, na hakika Allah ni Mwenye nguvu sana, Mwenye hekima nyingi
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ
Na endapo watapuuza basi Allah anawajua mno waharibifu
قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ كَلِمَةٖ سَوَآءِۭ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمۡ أَلَّا نَعۡبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشۡرِكَ بِهِۦ شَيۡـٔٗا وَلَا يَتَّخِذَ بَعۡضُنَا بَعۡضًا أَرۡبَابٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُولُواْ ٱشۡهَدُواْ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu: Njooni kwenye neno la sawa kati yetu na kati yenu ya kuwa, tusimuabudu isipokuwa Allah tu, wala tusimshirikishe na chochote, na tusiwafanye baadhi yetu Miungu badala ya Allah. Na kama watapuuza, basi semeni (muwaambie): Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تُحَآجُّونَ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَمَآ أُنزِلَتِ ٱلتَّوۡرَىٰةُ وَٱلۡإِنجِيلُ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Enyi Watu wa Kitabu, kwanini mnaleta mijadala kuhusu Ibrahimu na ilhali Taurati na Injili hazikuteremshwa isipokuwa baada yake? Hivi hamtumii akili?
هَـٰٓأَنتُمۡ هَـٰٓؤُلَآءِ حَٰجَجۡتُمۡ فِيمَا لَكُم بِهِۦ عِلۡمٞ فَلِمَ تُحَآجُّونَ فِيمَا لَيۡسَ لَكُم بِهِۦ عِلۡمٞۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
E nyinyi hawa! Mlihoji yale mnayoyajua, basi kwanini mnahoji msiyoyajua? Na Allah anajua na nyinyi hamjui
مَا كَانَ إِبۡرَٰهِيمُ يَهُودِيّٗا وَلَا نَصۡرَانِيّٗا وَلَٰكِن كَانَ حَنِيفٗا مُّسۡلِمٗا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Ibrahimu hakuwa Myahudi na wala (hakuwa) Mnaswara, lakini alikuwa Muongofu, Muislamu na hakuwa miongoni mwa Washirikina
إِنَّ أَوۡلَى ٱلنَّاسِ بِإِبۡرَٰهِيمَ لَلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ وَهَٰذَا ٱلنَّبِيُّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۗ وَٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika, watu walio na haki zaidi kwa Ibrahimu ni wale tu waliomfuata yeye na (kumfuata) Mtume huyu na wale walioamini. Na Allah ni Msimamizi wa Waumini
وَدَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يُضِلُّونَكُمۡ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ
Kundi katika Watu wa Kitabu limetamani kukupotezeni, na hawatampoteza (yeyote) isipokuwa wao wenyewe tu na ilhali hawatambui
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَأَنتُمۡ تَشۡهَدُونَ
Enyi Watu wa Kitabu, kwanini mnazipinga Aya za Allah ilhali mnashuhudia?
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَلۡبِسُونَ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Enyi Watu wa Kitabu, kwanini mnachanganya haki na batili na mnaificha haki na ilhali nyinyi mnajua (kuwa mnachofanya sio sahihi)?
وَقَالَت طَّآئِفَةٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ ءَامِنُواْ بِٱلَّذِيٓ أُنزِلَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَجۡهَ ٱلنَّهَارِ وَٱكۡفُرُوٓاْ ءَاخِرَهُۥ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na kundi katika Watu wa Kitabu lilisema: Aminini mwanzo wa mchana (asubuhi) kile kilichoteremshwa kwa wale walioamini na kikataeni mwisho wake (jioni), huenda watarudi (nyuma)
وَلَا تُؤۡمِنُوٓاْ إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمۡ قُلۡ إِنَّ ٱلۡهُدَىٰ هُدَى ٱللَّهِ أَن يُؤۡتَىٰٓ أَحَدٞ مِّثۡلَ مَآ أُوتِيتُمۡ أَوۡ يُحَآجُّوكُمۡ عِندَ رَبِّكُمۡۗ قُلۡ إِنَّ ٱلۡفَضۡلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ
Na msimuamini (yeyote) isipokuwa tu yule aliyefuata dini yenu Sema: Muongozo (sahihi) ni muongozo wa Allah tu, kwamba kuna yeyote atakayepewa mfano wa mlichopewa au atakuhojini kwacho mbele ya Mola wenu. Sema: Hakika, fadhila zote ziko mkononi mwa Allah, na Allah ni Mkunjufu, Mjuzi mno
يَخۡتَصُّ بِرَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ
Anamhusisha kwa (kumpa) rehema zake amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa