۞وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مَنۡ إِن تَأۡمَنۡهُ بِقِنطَارٖ يُؤَدِّهِۦٓ إِلَيۡكَ وَمِنۡهُم مَّنۡ إِن تَأۡمَنۡهُ بِدِينَارٖ لَّا يُؤَدِّهِۦٓ إِلَيۡكَ إِلَّا مَا دُمۡتَ عَلَيۡهِ قَآئِمٗاۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لَيۡسَ عَلَيۡنَا فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ سَبِيلٞ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Na miongini mwa Watu wa Kitabu wapo ambao endapo utamuamini (ukaweka kwake amana ya) mali nyingi, atakutekelezea (kwa kukurejeshea). Na miongoni mwao wapo ambao ukimuamini kwa dinari moja tu, haitekelezi (hairejeshi) isipokuwa tu kwa kumsimamia (kumdai na kumfuatilia). Hilo ni kwa sababu walisema: Hakuna lawama kwetu kwa (tunachowafanyia) Umiyina (wasiojuwa kuandika wala kusoma kilichoandikwa)[1] na wanamzulia Allah uongo ilhali wanajua
1- - Wanaokusudiwa hapa ni Waislamu Waarabu ambao kwa wakati huo hawakuwa wanajua kuandika wala
kusoma kilichoandikwa. Ni aina fulani ya dharau, ubaguzi, kejeli na udhalilishaji wa Wayahudi dhidi ya
jamii ya Waislamu; sifa ambazo Wayahudi na washirika wao wanaziendeleza hadi leo.
بَلَىٰۚ مَنۡ أَوۡفَىٰ بِعَهۡدِهِۦ وَٱتَّقَىٰ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ
Ni hakika; ambaye ametekeleza kikamilifu ahadi yake na akamcha Allah, kwa hakika Allah anawapenda wacha Mungu
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَشۡتَرُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَأَيۡمَٰنِهِمۡ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَـٰٓئِكَ لَا خَلَٰقَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيۡهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Hakika, wale wanaouza ahadi ya Allah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawatakuwa na fungu (la kheri yoyote) Akhera, na Allah hatazungumza nao (mazungumzo ya huruma) na hatawaangalia (kwa huruma) Siku ya Kiama na hatowatakasa (kwa kusamehe dhambi zao) na watapata adhabu kali mno
وَإِنَّ مِنۡهُمۡ لَفَرِيقٗا يَلۡوُۥنَ أَلۡسِنَتَهُم بِٱلۡكِتَٰبِ لِتَحۡسَبُوهُ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَمَا هُوَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ وَمَا هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Na kwa hakika kabisa, miongoni mwao lipo kundi linalopindisha ndimi zao kwenye kitabu (cha Taurati) ili mdhani hayo (wayapindishayo) yanatoka kitabuni, na (ukweli) si sehemu ya kitabu. Na wanasema: Hayo yanatoka kwa Allah na kamwe hayatoki kwa Allah, na wanamzulia Allah uongo huku wakijua
مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤۡتِيَهُ ٱللَّهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُواْ عِبَادٗا لِّي مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن كُونُواْ رَبَّـٰنِيِّـۧنَ بِمَا كُنتُمۡ تُعَلِّمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ وَبِمَا كُنتُمۡ تَدۡرُسُونَ
Haiwi kwa mwanadamu yeyote ambaye Allah amempa kitabu na hukumu (elimu na mamlaka) na Utumekisha awaambie watu: “Niabuduni mimi badala ya Allah”, na lakini (anatakiwa kuwaambia): “Kuweni watiifu kwa Mola mlezi, kutokana na yale mliyokuwa mnayafundisha (yatokanayo na) kitabu na kutokana na yale mliyokuwa mkiyasoma
وَلَا يَأۡمُرَكُمۡ أَن تَتَّخِذُواْ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ أَرۡبَابًاۚ أَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡكُفۡرِ بَعۡدَ إِذۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ
Na (pia haiwi kwa yeyote ambaye Allah amempa Kitabu, elimu, mamlaka na Utume) akuamrisheni muwafanye Malaika na Manabii kuwa Miungu. Hivi (inawezekana) akuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi ni Waislamu?
وَإِذۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ لَمَآ ءَاتَيۡتُكُم مِّن كِتَٰبٖ وَحِكۡمَةٖ ثُمَّ جَآءَكُمۡ رَسُولٞ مُّصَدِّقٞ لِّمَا مَعَكُمۡ لَتُؤۡمِنُنَّ بِهِۦ وَلَتَنصُرُنَّهُۥۚ قَالَ ءَأَقۡرَرۡتُمۡ وَأَخَذۡتُمۡ عَلَىٰ ذَٰلِكُمۡ إِصۡرِيۖ قَالُوٓاْ أَقۡرَرۡنَاۚ قَالَ فَٱشۡهَدُواْ وَأَنَا۠ مَعَكُم مِّنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Na (kumbuka) Allah alipochukua ahadi ya Manabii ya kuwa kitabu chochote na hekima yoyote niliyokupeni kisha akakujieni Mtume anayesadikisha kile mlichonacho kwamba kwa yakini kabisa mtamkubali na kumnusuru. (Allah) Akasema: Je, mmekubalina mmechukua ahadi yangu juu ya hilo? Wakasema: Tumeikubali. (Allah) Akasema: Shuhudieni kwamba, na mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kushuhudia
فَمَن تَوَلَّىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ
Basi watakaokengeuka baada ya (makubaliano) hayo basi hao ni waovu tu
أَفَغَيۡرَ دِينِ ٱللَّهِ يَبۡغُونَ وَلَهُۥٓ أَسۡلَمَ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ
Hivi wanataka dini isiyokuwa ya Allah, na ilhali vinamtii yeye vyote vilivyomo mbinguni na ardhini kwa hiari na lazima? Na kwake yeye tu watarejeshwa
قُلۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ
Sema: Tumemuamini Allah na kile tulichoteremshiwa na alichoteremshiwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haka na Yakubu na Asbaati (watoto wa Yakubu) na alichopewa Musa na Isa na Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao. Hatumbagui yeyote kati yao. Nasisi tumejisalimisha kwake tu
وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Na yeyote atakayetaka dini isiyokuwa Uislamu, hatakubaliwa na Akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara
كَيۡفَ يَهۡدِي ٱللَّهُ قَوۡمٗا كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ وَشَهِدُوٓاْ أَنَّ ٱلرَّسُولَ حَقّٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Vipi Allah atawaongoa watu waliokufuru baada ya kuamini, na wameshuhudia pasipo shaka kwamba Mtume (Muhammad) ni hakina wamejiwa na ubainifu mbalimbali? Na Allah hawaongoi watu madhalimu
أُوْلَـٰٓئِكَ جَزَآؤُهُمۡ أَنَّ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةَ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Hao malipo yao ni kwamba, watashukiwa na laana ya Allah na ya Malaika na ya watu wote
خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Watabaki milele humo (kwenye laana); hawatapunguziwa adhabu na hawatangojwa (hawatapewa muda wa kujitetea au kuomba msamaha)
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Isipokuwa (watakaoepuka laana ni) wale waliotubu baada ya hapo na wakafanya mema. Basi kwa hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّن تُقۡبَلَ تَوۡبَتُهُمۡ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلضَّآلُّونَ
Hakika, wale waliokufuru baada ya kuamini kisha wakazidisha ukafiri, toba zao hazitakubaliwa, na hao ndio hasa wapotevu
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡ أَحَدِهِم مِّلۡءُ ٱلۡأَرۡضِ ذَهَبٗا وَلَوِ ٱفۡتَدَىٰ بِهِۦٓۗ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Hakika, wale waliokufuru na wakafa wakiwa makafiri, kamwe hatakubaliwa mmoja wao hata kama atajikomboa kwa kutoa fidia ya dhahabu ujazo wa ardhi yote. Hao watapata adhabu yenye maumivu makali mno na hawatakuwa na watetezi (wowote)
لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ
Hamtaupata wema hadi mtoe katika mnavyovipenda. Na kitu chochote mtakachokitoa, hakika Allah anakijua sana