Sura: YUSUF 

Aya : 51

قَالَ مَا خَطۡبُكُنَّ إِذۡ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفۡسِهِۦۚ قُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمۡنَا عَلَيۡهِ مِن سُوٓءٖۚ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡـَٰٔنَ حَصۡحَصَ ٱلۡحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

(Mfalme) Alisema (akiwauliza wale wanawake): Mlikuwa na kadhia gani mlipomtongoza Yusuf bila ya ridhaa yake? Walisema: “Allah apishe mbali! Sisi hatukujua baya lolote kwake”. Mke wa Mheshimiwa alisema: Sasa haki imedhihiri (acha niseme kweli). Mimi ndiye niliyemtongoza (Yusuf) bila ya ridhaa yake na hakika yeye ni katika wakweli



Sura: YUSUF 

Aya : 52

ذَٰلِكَ لِيَعۡلَمَ أَنِّي لَمۡ أَخُنۡهُ بِٱلۡغَيۡبِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي كَيۡدَ ٱلۡخَآئِنِينَ

(Yusuf alisema): Hayo (nimeyaombea ufafanuzi) ili (Mheshimiwa) apate kujua ya kwamba mimi sikudhamiria kumfanyia khiyana wakati hayupo na ya kwamba Allah haziongozi hila za watu wenye khiyana