أَتَدۡعُونَ بَعۡلٗا وَتَذَرُونَ أَحۡسَنَ ٱلۡخَٰلِقِينَ
Mnamwomba Baali na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
Tarayya :
ٱللَّهَ رَبَّكُمۡ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Allah, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Allah walio safishwa
وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye
سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلۡ يَاسِينَ
Iwe salama kwa Ilyas
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema
إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini
وَإِنَّ لُوطٗا لَّمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na hakika Lutwi bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume
إِذۡ نَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Tulipo mwokoa yeye na watu wake wote,
إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ
Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma
ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawaangamiza wale wengineo
وَإِنَّكُمۡ لَتَمُرُّونَ عَلَيۡهِم مُّصۡبِحِينَ
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
وَبِٱلَّيۡلِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume
إِذۡ أَبَقَ إِلَى ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُدۡحَضِينَ
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa
فَٱلۡتَقَمَهُ ٱلۡحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٞ
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa
فَلَوۡلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُسَبِّحِينَ
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Allah,
لَلَبِثَ فِي بَطۡنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa